Alichojitabiria Zitto kimemtokea haraka

Alichojitabiria Zitto kimemtokea haraka

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Mwaka jana mwishoni Zitto alifanya mahojiano na gazeti la mwananchi na alihojiwa mambo mbali mbali likiwemo la mstakabari wake kisiasa. Mwandishi pamoja na mambo mengine alitaka kujua Zitto kwa nini asihame toka Chadema na kuhamia vyama vingine. Zitto alisema kuhama chama siyo jambo rahisi, akasema ukihama chama utapata headlines za magazeti kwa wiki mbili mpaka mwezi mmoja alafu unakufa kisiasa.

Kiukweli alichotabiri Zitto ndicho kilichomtokea, baada ya kufanya ziara ambayo haikuwa na mafanikio makubwa pamoja na kuhudhuriwa na watu wengi. Zitto alipata headlines kweli kwenye magazeti na mitandao ya kijamii, lakini baada ya mikutano hiyo Zitto hasikiki tena. Mikutano yake mikubwa sijui kama ilikuwa na faida maana alishindwa kumchukua hata mwenyekiti wa mtaa awe wa Chadema hata CCM.

Nashawishika kukubaliana naye kwamba alichokuwa anaogopa 'kupata headlines za wiki mbili na kufa kisiasa' alikuwa sahihi kabisa. Kujenga chama si mchezo, hata angepewa miaka mitano kujenga chama chake Kigoma tu bado ni kazi ngumu sana. Zitto ni kijana ninayemwamini kwamba ana akili na uwezo mkubwa, ilikuwaje akaingia mkenge wa wapiga dili kwamba wanaazisha chama ambacho 'eti' wabunge wengi watajiunga nacho baada ya bunge kuvunjwa? Si amuulize Mpendazoe alivyoingizwa mkenge na CCJ 2010?
 
Zitto ni kijana ninayemwamini kwamba ana akili na uwezo mkubwa, ilikuwaje akaingia mkenge wa wapiga dili kwamba wanaazisha chama ambacho 'eti' wabunge wengi watajiunga nacho baada ya bunge kuvunjwa? Si amuulize Mpendazoe alivyoingizwa mkenge na CCJ 2010?
ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga.
ulisaliti nawe utasalitiwa!
 
Hii ndiyo imemfanya kula matapishi yake kwa wale aliokuwa anawaita wasakatonge. ndio sasa anapigia magoti
angalau wamsaidie apate ubunge wake tena. Hii ni Tanzania bwana haina mwenyewe.
 
kujengachama ni kazi kweli x2. Ni Mrema tu aliyefanikisha kwani watu walikuwa na kiu kubwa ya demokrasia. kwa sasa ni Chadema/ Ukawa tu. pole zake. akafundishe vyuoni.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti..., huyu naye ndo anafikwa na mauti ya kisiasa. Baada ya uchaguzi atakuwa sawa na msaliti Kaburu madevu!
 
Hii ndiyo imemfanya kula matapishi yake kwa wale aliokuwa anawaita wasakatonge. ndio sasa anapigia magoti
angalau wamsaidie apate ubunge wake tena. Hii ni Tanzania bwana haina mwenyewe.

Kama hana agenda nyingine anajua pia kwamba UKAWA haiwezi kumpokea, na kama wakimpokea siyo leo.
 
Kitila Mkumbo anaweza kuwa muhusika mkuu katika kupotoka kwake. Kule kumpamba kuwa yeye ni mashuhri sana ilikuwa njia ya kuvuta mshiko toka kwake kwani alikuwa anajua zzk lazima atapewa pesa na watawala wakati yeye hawezi pewa.
 
kujengachama ni kazi kweli x2. Ni Mrema tu aliyefanikisha kwani watu walikuwa na kiu kubwa ya demokrasia. kwa sasa ni Chadema/ Ukawa tu. pole zake. akafundishe vyuoni.

Mrema hakujenga chama bali alikuwa na ufuasi, kujenga chama ni kuwa na mtandao kuanzia kitongoji cha mwisho nchi hii hadi Dar
 
Kuna wakala wake kule facebook juzi katupia post anasema "watu hawadanganyiki, ni CDM kwa kwenda mbele tu", wakati wa mikutano ya Zitto alikuwa anaponda CDM kila siku.
 
Last edited by a moderator:
Ni kama Shekhe Yahaya alivyotabiri kuwa mtu mmoja maarufu angekufa, kumbe alikuwa ni yeye mwenyewe.

Kiukweli alichotabiri Zitto ndicho kilichomtokea, baada ya kufanya ziara ambayo haikuwa na mafanikio makubwa pamoja na kuhudhuriwa na watu wengi. Zitto alipata headlines kweli kwenye magazeti na mitandao ya kijamii, lakini baada ya mikutano hiyo Zitto hasikiki tena. Mikutano yake mikubwa sijui kama ilikuwa na faida maana alishindwa kumchukua hata mwenyekiti wa mtaa awe wa Chadema hata CCM.

Nashawishika kukubaliana naye kwamba alichokuwa anaogopa 'kupata headlines za wiki mbili na kufa kisiasa' alikuwa sahihi kabisa. Kujenga chama si mchezo, hata angepewa miaka mitano kujenga chama chake Kigoma tu bado ni kazi ngumu sana. Zitto ni kijana ninayemwamini kwamba ana akili na uwezo mkubwa, ilikuwaje akaingia mkenge wa wapiga dili kwamba wanaazisha chama ambacho 'eti' wabunge wengi watajiunga nacho baada ya bunge kuvunjwa? Si amuulize Mpendazoe alivyoingizwa mkenge na CCJ 2010?
 
ZZK kaingia choo cha kike....! Inakula kwake taaratiiibu
 
kwa akili alizonazo simlaumu wala simsifii anajua anachokifanya na anajua mwisho wake TUKUTANE OCTOBER
 
Back
Top Bottom