Alichojibu Hammy B kwa AY | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alichojibu Hammy B kwa AY

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Simba Mkali, Jun 13, 2012.

?

What this?

Poll closed Jun 23, 2012.
 1. 1

  100.0%
 2. 2

  100.0%
 3. 3

  100.0%
 4. 4

  100.0%
 1. Simba Mkali

  Simba Mkali JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 589
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  "Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa kuhusu uhusiano wangu na swahiba wangu A.Y.

  Ningependa ifahamike kwamba mimi na A.Y kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi nyingine za biashara. Ni kawaida na inaeleweka kwamba mahali popote watu wanapofanya kazi pamoja kugongana katika mawazo au lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.

  Hivyo, nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha bila kujibu madhara yake yatakuwa mabaya. Kwanza napenda ieleweke sijawahi kuwa msimamizi wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza tu muziki wake. Maswala mengine yoooote amekuwa akifanya mwenyewe tena bila msaidizi.

  Pia, bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi kutengeneza muziki wao nisingekua hapa nilipo. Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie kwa mtu fulani au mkondo fulani. Si ajabu kama kipaji changu cha kuproduce muziki kimeweza kufahamika kwa kupitia kwa A.Y. Mimi sio mungu labda ningekua sehemu nyingine na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,lakini nachojua rafiki yangu amenipa ngazi ya kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha hilo na hata wao wenyewe wanajua na bado nashukuru kwa hilo.

  A.Y hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote na kampuni ya BHits Music Group Limited wala mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na sio mtu mwingine yoyote. Nimetengeneza nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili ya albamu yake katika kipindi cha mwaka 2008 mpaka 2011. Baadhi ya nyimbo hizo zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri uhitaji wake. Wote tulikua na lengo la kutengeneza muziki kwa wingi na kuuza kwenye soko zuri la muziki ili tufaidike kwa pamoja.

  Muda wote muziki ulikua unatolewa na unafanya vizuri kwa radio na T.V na show zilikua zinafanyika na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au nje ya nchi hii hata malipo nilikua nafahamu ni kiasi gani na sijawahi kufichwa na A.Y kuhusu hilo.

  Kutoelewana kwetu kibiashara ilikuwa mwezi February mwaka huu yakihusu malipo ya album hiyo. Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu mimi na rafiki yangu tu.

  Nimeamua kuongea sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa mara ya pili kuhusu makubaliano haya na mara ya kwanza niliamua kukaa kimya.

  Kwanza nataka mfahamu Katika kipindi cha kutokea 2008 mpaka leo hii (miaka 4) kwa matumizi ya nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show nje na ndani ya nchi na nyingine kumpatia nominations na tuzo tofauti, nilichowahi kulipwa hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa malipo ya awamu tofauti kwa miaka minne.

  Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa kawaida anaehangaika kutoka.

  Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi, ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja niliomba nilipwe millioni 2.

  Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na niliona biashara hii itavunja urafiki wetu

  Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya. Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo bado hazijamixiwa, ila ampatie producer mwingine amfanyie hiyo kazi.

  Mpaka hii makala A.Y hajaja kuchukua hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi

  Swala la mimi kuwa na wivu na kinyongo na mafanikio ya A.Y ni uongo na nashangaa umetoka wapi . Kama kulipwa kidogo, huku nikiona A.Y anaingiza fedha nyingi kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi ningekua nimegombana nae toka mwaka 2009 labda

  Narudia kwamba nilikua najua kila show yake inapofanywa na sikuwahi kujisikia vibaya. Nataka utambue pia nilikua na akili timamu wakati nafanya kazi na A.Y na muda wowote nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na kutaka tuandike makubaliano kwa karatasi ila sikufanya hivyo na wala sijutii chochote kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi bila mkataba wa maandishi na ndio maana nipo radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure kama nlivomwambia hapo mwanzo

  Nina meseji zote na email za mazungumzo yetu ambazo nilihifadhi nikijua ipo siku nitaonekana mimi ndie mkorofi, hivyo nachokisema nina hakika nacho asilimia 100

  Picha nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu kuonyesha kuna kutopendana kati ya maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali ni marafiki wazuri tu na mpaka leo hii nikiwa na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master Jay nitampigia simu bila aibu kwani hakuna ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay na Marco Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika kipindi cha miaka minne akiwa Bhits kwa hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa mimi nimeenda na A.Y na mara kadhaa nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya shughuli zangu binafsi.

  Pia ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua akitumia muda mwingi MJ Records kuliko Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake binafsi. A.Y hajawahi kuzuiwa kufanya kazi na mtu mwingine kwani ni msanii huru.

  Ndugu yangu mimi ni mtu mpole nisiye na ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika sana kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi kuonyesha kwamba mimi na swahiba wangu tumejenga uadui.
   
 2. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  bongo flava ina vichomi vingi sana.
   
 3. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  Pole kaka. Hata hivyo nakukubali sana.
   
 4. Bufa

  Bufa JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 4,167
  Likes Received: 3,371
  Trophy Points: 280
  AY inabidi ajue kwamba sasa yeye ni msanii mkubwa hawezi nunua nyimbo kwa bei ya undergrounds, record labels zinaendeshwa na wasanii wakubwa kwa kufanya nao kazi kwa gahrama kubwa kidogo kama anaona hiyo sio fair kwake basi achukue nyimbo zake aende kwa studio zingine.
   
 5. Don Mangi

  Don Mangi JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,206
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hermy B is a gentleman, nimekubali the way he responded to the matter, hakunaga haja ya kugombana, especially na celebrities. He handed the matter like how a gentleman should have.
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mabitonga tu hao wote..
   
 7. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Hammy B would be the perfect person for ccm's Ideology and Publicity Post. He is positive, comprehensive and humble in his message. Anyone who judge fairly will note that Hammy is on the highest level of civilization

  Kwa Nape Hammy B ni Profesa.
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Sijaelewa hiyo poll hapo juu inahusu nini!? au unataka kuonesha kwamba na wewe unaweza kucreate poll?
   
 9. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Huyu jamaa kwa jinsi nilivyomsoma ni smart sana..
   
 10. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,791
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Absolutely
   
 11. Hashm

  Hashm Member

  #11
  Jun 15, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 47
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Always bongo Celebrities are in love wth cheap materials even though they get profty,,,,,ay ,,madee etc waz born in ths ****ng way
  Hermy b gud,time wl tell everthng brthr
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,740
  Trophy Points: 280
  Sifahamu sana
   
 13. Cestus

  Cestus JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 1,000
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Now thats a good english for a learner!!
   
 14. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #14
  Jun 15, 2012
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, jamaa ameonesha ukomavu mkubwa sana ktk kujibu hoja ya AY, mi naona Hammy naye anamchango mkubwa ktk mafanikio ya AY kwani alishaanza kupotea ktk game hivyo waheshimiane.
   
 15. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #15
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,969
  Likes Received: 2,963
  Trophy Points: 280
  Hawa wasanii wa bongo wapuuzi kweli. Ay anafurahi kupokea shoo tu.
   
 16. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #16
  Jun 17, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Pole hermy! Hizo ndio challenge za maisha.. Wasanii wakishatoka hujisahau sana walitokea wapi..
   
 17. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #17
  Jun 17, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hammy B ni bonge la brain minded
   
 18. bg_dg_dy

  bg_dg_dy JF-Expert Member

  #18
  Jun 17, 2012
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 60
  FA & AY ni wangese tu hao
   
 19. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #19
  Jun 17, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  duh.....................:D
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kumbe AY nae mbabaishaji...
   
Loading...