Alibaba ni matapeli au? Msaada please

faby

JF-Expert Member
Feb 18, 2011
2,214
765
Habari wakuu,Kuna mashine nataka kuagiza through alibaba lakini nashangaa bei zipo chini sanaaa kulinganisha na market price! Naogopa nisije tapeliwa wenye uzoefu na alibaba msaada please.
 
Alibaba ni kampuni ya China(by origin) unategemea bei zao ziwe sawa na products za German au Italy? We nunua but kuwa makini kama ni kweli Alibaba wenyewe.
 
Habari wakuu,Kuna mashine nataka kuagiza through alibaba lakini nashangaa bei zipo chini sanaaa kulinganisha na market price! Naogopa nisije tapeliwa wenye uzoefu na alibaba msaada please.

Kwanza hakuna kutapeliwa Alibaba wanafanya biashara na mamilioni ya wateja dunia yote! Hii biashara ya online ndiyo inayotawala duniani hivi sasa na mtaji wao mkubwa hawa watu ni uaminifu! Nadhani kinachokutisha wewe ni ugeni wa hii aina ya kununua au kuagiza vitu kwa mtandao! Kuhusu bei usiseme ni bei chee sana, bei halisi utaijua baada ya kunegotiate na supplier, hizo unazoona wanadisplay usifikiri ni bei halisi. Hata hivyo bei zao kiujumla ni nafuu! Sasa hiyo market price unayosema ni ya wapi? Kariakoo? Hiyo si ndiyo marketi ya China, au unalinganisha na market price ya Ulaya, Marekani na Japan?

Kunakamzigo nimeagiza Alibaba kako njiani kakifika nitakujulisha raha nilizozipata, unaonyeshwa kila hatua zote zinavyoendelea huko toka kuweka order hadi mzigo unapokuwa tayari kutumwa unajionea mwenyewe! Unajua mzigo wangu uko wapi hadi sasa. Yaani naona dunia inasonga mbele hata sisi wa udongini Tanzania unaagizia mzigo China kirahisi kuliko ambavyo ukiwa Dar huwezi ukaagizia mzigo toka Chalinze ukafika bila BP kupanda na kushuka! Watu wamezidi sana kuwadharau wachina, wameshadanganywa sana kuhusu ubaya wa wachina! Wachina wanauza mizigo lukuki Marekani kwa kutumia Alibaba!
 
tunashukuru mzee kwa maelezo mazuri
Unajua watu wengi wana wrong perception na wachina pamoja na wawekezaji kwa ujumla, wanachujua wachina ni watu wa feki kila kitu. hivi sasa wachina wanatisha dunia kote, makampuni mengi makubwa yanawekeza huko japo hali imeanza kubadilika kidogo kulingana na kuongezeka kwa labor cost. mm nipo nchi fulani japo imeendelea kulika china lakini asilimia kubwa ya bidhaa zinatoka china na wao makampuni yao mengi walishahamishia huko
watanzania cc ni waoga sana cjui kwanini na kitu mtu akijisikia tuy basi ataeneza na watu wanaamini
 
Ni kweli kabisa nakubaliana na wewe. Fpam cha kufanya tu tahadhari unapolipa usimlipe supplier direct, utaliwa, kwenye online payment mara nyingi huwa kuna controller ambaye anadhibiti payments ili kuepuka suppliers wabaya ambao wakilipwa hawatumi vitu, kwa hiyo nadhani utakuwa unasikia ebay, paypal, escrow n.k Ukitaka kununua Alibaba weka order yako kupitia escrow, hii inajinalingine Alipay, ukilipa hela inadhibitiwa na hao Alipay, hailipwi kwa supplier hadi wewe mnunuzi uidhinishe malipo baada ya kupokea Bill of landing toka kwa muuzaji wako huko China. Mawasiliano hayo yote yanafanyika kwenye akaunti yako utakayofungua kwenye mtandao wa Alibaba. Kuna chaji kidogo kama dola 28 kwa ajili ya huduma hiyo.
 
kiongozi nashukuru siku nikitaka kufanya transaction ntaku consult ili unielekeze vizuri
 
Ni kweli kabisa nakubaliana na wewe. Fpam cha kufanya tu tahadhari unapolipa usimlipe supplier direct, utaliwa, kwenye online payment mara nyingi huwa kuna controller ambaye anadhibiti payments ili kuepuka suppliers wabaya ambao wakilipwa hawatumi vitu, kwa hiyo nadhani utakuwa unasikia ebay, paypal, escrow n.k Ukitaka kununua Alibaba weka order yako kupitia escrow, hii inajinalingine Alipay, ukilipa hela inadhibitiwa na hao Alipay, hailipwi kwa supplier hadi wewe mnunuzi uidhinishe malipo baada ya kupokea Bill of landing toka kwa muuzaji wako huko China. Mawasiliano hayo yote yanafanyika kwenye akaunti yako utakayofungua kwenye mtandao wa Alibaba. Kuna chaji kidogo kama dola 28 kwa ajili ya huduma hiyo.

Asante kaka nataka kuagiza used caterpillar excavators sasa nikaona bei alibaba ipo chini sana tofauti na europe! Inabidi nijifunze zaidi kuhusu hiyo alipay
 
Hawa jamaa wengi wao matapeli kuwa makini! Kama unanunua kitu cha dhaman zaid ya $2000 sikushauri watakuibia hao!
Habari wakuu,Kuna mashine nataka kuagiza through alibaba lakini nashangaa bei zipo chini sanaaa kulinganisha na market price! Naogopa nisije tapeliwa wenye uzoefu na alibaba msaada please.
 
mkuu ingia gharama uende huko mwenyewe, kuna mtu kaagiza hilo excavator, huu ni mwezi wa saba bado analisubiria, biashara ya pesa nyingi ni vizuri ukafunga safari kwenda, yani unageuza ukishaona imepakiwa at least kwenye container, kuna mambo ya utapeli sana china, mapopo wamejaaa

Asante kaka nataka kuagiza used caterpillar excavators sasa nikaona bei alibaba ipo chini sana tofauti na europe! Inabidi nijifunze zaidi kuhusu hiyo alipay
 
mkuu ingia gharama uende huko mwenyewe, kuna mtu kaagiza hilo excavator, huu ni mwezi wa saba bado analisubiria, biashara ya pesa nyingi ni vizuri ukafunga safari kwenda, yani unageuza ukishaona imepakiwa at least kwenye container, kuna mambo ya utapeli sana china, mapopo wamejaaa

Ndio nilichokua naogopa! Ushauri wako mzuri sana bora nifunge tu safari kuliko kupigwa changa la macho
 
Mkuu kuna watu wana coment utazani walisha wahi kununua kupitia huo mtandao, Wabongo kwa kukatishana tamaa hawajambo,

Kuna mdao mmoja kasema kweli hapo, Kuna kitu inaitwa Escrow, hawa ndo wana contro systeam ya payment na pesa unatuma kwao wao ndo wana mpa muuzaji pesa pale atakapo kuwa ametuma mzigo kwako, na kuna hadi Inspectors ukitaka unapata mkaguzi wa kukagua product kabla ya Kusafirishwa,

Na mara nyingi inashauriwa kuwasilian na kampuni husika na sio supplaya, na hata ukiwalipa directly kwa sasa kule china kuna sheria kari sana na wakibainika wanafungiwa mazima na wao kufungwa jela,

Kikubwa inatakiwa Ujiridhishe na kampuni husika na uhakikishe inaelewaka, ukishindwa hapo basi tumia Escro make hawa ndo kiboko yao na kama ni matapeli watakataa usiwalipe kupitia Escrow make wanajua hapo inakula kwao

Katika Dunia ya sasa huhitaji kupanda ndege na kwenda kufuata mzigo, kwani unaweza ona ghalama za kupanda ndege, kula, kulala na kazaila zinatosha kutafuta Inspectors huko huko na akainspect product yako na wewe ukatumiwa mzigo na kuja kuuchukua Dar,
 
kiukweli nilishawahi lizwa alibaba.com 800$ , alibaba wako supplier wengi sana matapeli, nakiri sikutumia escrow wala alipay but baada ya hapo hunishauri kununua chochote alibaba.com na hata hizo alipay / escrow siziamini na zenyewe!!! anyway wanaokushauri ununue but utumie alipay / escrow jaribu na uangalie matokeo, huwezi kuwa mjanja wa mahali mpaka uingizwe mjini. Now natumia Ebay sana na ni salama sana na paypal ni ya kuaminika sana, kama mzigo hujafikia au defective unarudishiwa pesa zako.
 
Hawa jamaa wengi wao matapeli kuwa makini! Kama unanunua kitu cha dhaman zaid ya $2000 sikushauri watakuibia hao!
Kwenye ununuzi wa magari used ya Japan kwenye Cartradeview.com wanaoption ya kupokea malipo kupitia PayTrade na utaratibu wao ni kama Alipay ya Alibaba.com na pesa inayolipwa mara nyingi ni kubwa zaidi ya USD 2000! Kama huwezi kuwaamini hao huwezi kunufaika na biashara hii ya kuagiza vitu nje! Kwa hiyo ndugu yangu ushauri wako watu wasiagize magari na mitambo nje maana kumlipa muuzaji direct hiyo ndiyo hatari zaidi! Ingefaa zaidi kama ungeshauri alternative na siyo kutisha watu, mbona Bandarini mali zinamiminika, wewe uzoefu wako kuhusu hili ukoje au ndiyo ulishaumizwa ukaogopa kabisa, sisi ni wajasilia mali bwana!
 
Back
Top Bottom