Alianza Heri James, sasa ni Gambo na Makonda atafuata

Elimu iliisha kitambo sasa hivi kama una tupesa unajifanya kukaa chuoni kisha unawahonga tu wahadhiri wenye njaa ambao wamejaa mavyuoni kisha unatunukiwa tu cheti.

Hicho ndicho atakacho fanya Bashite kwa sababu akili za darasani hana huyo na wa hivyo wamejaa ktk nchi hii wengine hadi ni ma-profesa kabisa.
 
Elimu iliisha kitambo sasa hivi kama una tupesa unajifanya kukaa chuoni kisha unawahonga tu wahadhiri wenye njaa ambao wamejaa mavyuoni kisha unatunukiwa tu cheti.

Hicho ndicho atakacho fanya Bashite kwa sababu akili za darasani hana huyo na wa hivyo wamejaa ktk nchi hii wengine hadi ni ma-profesa kabisa.
kweli lakini
 
Kwahiyo kaenda kusoma masters ili akirudi aje kuajiriwa?? Aliyekuwa mkuu wa wilaya 4yrs akawa Mkuu wa mkoa 5yrs??
Baadae anaweza kuwa rais wako huyo!

Kwani kuna shida gani siku ukisikia ni balazi katika nchi flani?!

Kuna shida gani siku ukisikia ni mkuu wa shirika flani kubwa la umma?

Makonda ana akili sana mkuu hakuna bavicha anafikia akili ya Makonda
 
Vijana waliofaidika na kutamba vilivyo na mfumo kandamizi wa mwendazake ni pamoja na:-
  • Makonda,
  • Sabaya,
  • Heri James,
  • Mrisho Gambo,
  • Ali Hapi na
  • Mnyeti
Ilikuwa huwaambii kitu hawa. Walifanya na kusema walitakalo hata kama linagharimu maisha, mali na utu wa mtanzania hawakujali. Walikuwa malaika wakuu wa utawala ule.

Mara tu baada ya mwendazake kutwaliwa na Allah, simanzi nzito na majuto yalidhihirika usoni kwa Sabaya. Alichuruzika michozi mithili ya mtoto yatima. Alikuwa anaomba radhi kwa Muumba na watanzania kiaina

Siku hazikupita nyingi, Heri James aliyekuwa na ujasiri wa kutishia kuutoa uhai wa mtanzania yeyote muda wowote mbele ya kamera wakati wa uhai wa mwendazake, aiibuka mbele ya kamera zile zile akaomba radhi mchana kweupee bila kutaja kosa lake. Watu wakabakia na maswali Heri James anaomba radhi kwa lipi? Wenye akili wakakumbuka.

Hapi. Huyu aliongea kwa kukunja ndita usoni pake ili kuonesha vitisho vyake na kuwatusi wazee wenye nyadhifa kubwa waliostaafu bila kujali umuhimu na haiba yao kwenye jamii. Hivi Sasa amejaa wahaka ijapokuwa bado ni RC.

Mrisho Gambo enzi zake alinena maneno ya makufuru dhidi ya wafuasi na mbunge wa chadema. Alitema nyongo kila uchwao kama joka la kuzimu. Alisimamia zoezi la uporaji katika maduka ya fedha za kigeni. Lakini sasa zigo la maovu aliyosimamia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa jiji la Arusha ameanza kulitua kwa kutubu kiaina bungeni. Anadai ulikuwa ni uonevu na aliyasimamia hayo kwa kupewa maagizo. Hii yote ni toba. Anatubu.

Mnyeti enzi zake aliharibu mali za aliowaona kikwazo kwenye kuyapata madaraka makubwa zaidi. Na kweli punde tu akaukwaa u-RC wa Manyara. Hivi sasa ni mbunge asiyekuwa na raha wala furaha. Amejawa na zigo la dhambi moyoni mwake. Huyu soon ataongea kama Mrisho Gambo.

Makonda aliyekuwa na kishindo kikubwa kuliko waziri mkuu na makamu wa rais mpk leo anaogopa hata kusalimia kwenye kamera, ambazo hapo awali alimudu kuzitumia kuonya hata wazee wenye umri sawa na babu yake kwamba wawe na adabu. Hata ikibidi Makonda alitembeza sonyo (alisonya) mbele ya kamera hizo. Huyu naye siku si nyingi yuko mbioni kutoka hadharani kama Heri James kuwaomba radhi watanzania. Kama unabisha, muda utaongea.

Ndugu zangu wahenga walisema dunia duara. Inazunguka na kuuzungusha ubaya ama wema. Leo ubaya/wema unaomfanyia mwenzako kesho utakurudia.
Kwenye orodha umewasahau wengi wakiwemo akina Chalamila, na Gelasius Byakamwa yule alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara
 
Baadae anaweza kuwa rais wako huyo!

Kwani kuna shida gani siku ukisikia ni balazi katika nchi flani?!

Kuna shida gani siku ukisikia ni mkuu wa shirika flani kubwa la umma?

Makonda ana akili sana mkuu hakuna bavicha anafikia akili ya Makonda
ushuzi mtupu
 
Back
Top Bottom