Alianza Heri James, sasa ni Gambo na Makonda atafuata

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,407
Vijana waliofaidika na kutamba vilivyo na mfumo kandamizi wa mwendazake ni pamoja na:-
  • Makonda,
  • Sabaya,
  • Heri James,
  • Mrisho Gambo,
  • Ali Hapi na
  • Mnyeti
Ilikuwa huwaambii kitu hawa. Walifanya na kusema walitakalo hata kama linagharimu maisha, mali na utu wa mtanzania hawakujali. Walikuwa malaika wakuu wa utawala ule.

Mara tu baada ya mwendazake kutwaliwa na Allah, simanzi nzito na majuto yalidhihirika usoni kwa Sabaya. Alichuruzika michozi mithili ya mtoto yatima. Alikuwa anaomba radhi kwa Muumba na watanzania kiaina

Siku hazikupita nyingi, Heri James aliyekuwa na ujasiri wa kutishia kuutoa uhai wa mtanzania yeyote muda wowote mbele ya kamera wakati wa uhai wa mwendazake, aiibuka mbele ya kamera zile zile akaomba radhi mchana kweupee bila kutaja kosa lake. Watu wakabakia na maswali Heri James anaomba radhi kwa lipi? Wenye akili wakakumbuka.

Hapi. Huyu aliongea kwa kukunja ndita usoni pake ili kuonesha vitisho vyake na kuwatusi wazee wenye nyadhifa kubwa waliostaafu bila kujali umuhimu na haiba yao kwenye jamii. Hivi Sasa amejaa wahaka ijapokuwa bado ni RC.

Mrisho Gambo enzi zake alinena maneno ya makufuru dhidi ya wafuasi na mbunge wa chadema. Alitema nyongo kila uchwao kama joka la kuzimu. Alisimamia zoezi la uporaji katika maduka ya fedha za kigeni. Lakini sasa zigo la maovu aliyosimamia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa jiji la Arusha ameanza kulitua kwa kutubu kiaina bungeni. Anadai ulikuwa ni uonevu na aliyasimamia hayo kwa kupewa maagizo. Hii yote ni toba. Anatubu.

Mnyeti enzi zake aliharibu mali za aliowaona kikwazo kwenye kuyapata madaraka makubwa zaidi. Na kweli punde tu akaukwaa u-RC wa Manyara. Hivi sasa ni mbunge asiyekuwa na raha wala furaha. Amejawa na zigo la dhambi moyoni mwake. Huyu soon ataongea kama Mrisho Gambo.

Makonda aliyekuwa na kishindo kikubwa kuliko waziri mkuu na makamu wa rais mpk leo anaogopa hata kusalimia kwenye kamera, ambazo hapo awali alimudu kuzitumia kuonya hata wazee wenye umri sawa na babu yake kwamba wawe na adabu. Hata ikibidi Makonda alitembeza sonyo (alisonya) mbele ya kamera hizo. Huyu naye siku si nyingi yuko mbioni kutoka hadharani kama Heri James kuwaomba radhi watanzania. Kama unabisha, muda utaongea.

Ndugu zangu wahenga walisema dunia duara. Inazunguka na kuuzungusha ubaya ama wema. Leo ubaya/wema unaomfanyia mwenzako kesho utakurudia.
 
Wakati Gambo anaongea kuhusu uporaji wa fedha za kigeni Arusha ghafla nikajiskia kuomba kumpa taarifa muongeaji

Nilijiskia kutamka maneno haya:

"Muheshimiwa naibu Spika naomba kumpa taarifa mchangiaji kuwa wakati uporaji huo unafanyika yeye ndiye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Zoezi lile alilisimamia yeye mwenyewe Kama mwenyekiti wa vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa

Mh. Spika, naomba kumpa taarifa mchangiaji kuwa viongozi wanaosimamia uvunjifu wa sheria za nchi ni wahaini na kwa kitendo kile alihujumu uchumi wa nchi yetu hivyo anastahili kuwa gerezani kwa sasa na sio kwenye Bunge lako tukufu"

Wakati nawaza hivyo ghafla usingizi ukaishi nikijikuta kumbe Mimi ni Uncle Jei Jei tu hata mtaa ambapo jengo la bunge lipo sijui unaitwaje. Nikajisonya tu Kama Makonda alivyowasonya Waziri Mkuu na wastaafu enzi zile akiwa Paul Makonda kweli kweli sio leo anavyotambulika kama Baba Keagan
 
Wakati Gambo anaongea kuhusu uporaji wa fedha za kigeni Arusha ghafla nikajiskia kuomba kumpa taarifa muongeaji......
Don_Mbowe_on_Instagram:_“15_February_2019..%0A.%0AVitu_vya_kuogopa_Sana_Hapa_Duniani_ni_Mungu_...jpg
 
Back
Top Bottom