Alianza Heri James, sasa ni Gambo na Makonda atafuata

Ana akili sana huyo!

Unaona anavyoambana? Akija kupata ulaji huko mbele kutokana na juhudi zake hizo za kupata elimu mataahira yataanza kumtukana wakati mwenzenu anapambana kama hivyo huku nyie mnapiga porojo humu mitandaoni.
anapambana wapi ameenda kupunguza stress. Aliyekuwa mkuu wa mkoa anaenda kusoma masters aje kupata ajira?? Hii nchi imejaa matahira.

si ajiajiri??
 
Vijana waliofaidika na kutamba vilivyo na mfumo kandamizi wa mwendazake ni pamoja na:-
-Makonda,
-Sabaya,
-Heri James,
-Mrisho Gambo,
-Ali Hapi na
-Mnyeti.

Ilikuwa huwaambii kitu hawa. Walifanya na kusema walitakalo hata kama linagharimu maisha, mali na utu wa mtanzania hawakujali. Walikuwa malaika wakuu wa utawala ule.

Mara tu baada ya mwendazake kutwaliwa na Allah, simanzi nzito na majuto yalidhihirika usoni kwa Sabaya. Alichuruzika michozi mithili ya mtoto yatima. Alikuwa anaomba radhi kwa Muumba na watanzania kiaina

Siku hazikupita nyingi, Heri James aliyekuwa na ujasiri wa kutishia kuutoa uhai wa mtanzania yeyote muda wowote mbele ya kamera wakati wa uhai wa mwendazake, aiibuka mbele ya kamera zile zile akaomba radhi mchana kweupee bila kutaja kosa lake. Watu wakabakia na maswali Heri James anaomba radhi kwa lipi? Wenye akili wakakumbuka.

Hapi. Huyu aliongea kwa kukunja ndita usoni pake ili kuonesha vitisho vyake na kuwatusi wazee wenye nyadhifa kubwa waliostaafu bila kujali umuhimu na haiba yao kwenye jamii. Hivi Sasa amejaa wahaka ijapokuwa bado ni RC.

Mrisho Gambo enzi zake alinena maneno ya makufuru dhidi ya wafuasi na mbunge wa chadema. Alitema nyongo kila uchwao kama joka la kuzimu. Alisimamia zoezi la uporaji ktk maduka ya fedha za kigeni. Lkn sasa zigo la maovu aliyosimamia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa jiji la Arusha ameanza kulitua kwa kutubu kiaina bungeni. Anadai ulikuwa ni uonevu na aliyasimamia hayo kwa kupewa maagizo. Hii yote ni toba. Anatubu.

Mnyeti enzi zake aliharibu mali za aliowaona kikwazo kwenye kuyapata madaraka makubwa zaidi. Na kweli punde tu akaukwaa u-RC wa Manyara. Hivi sasa ni mbunge asiyekuwa na raha wala furaha. Amejawa na zigo la dhambi moyoni mwake. Huyu soon ataongea kama Mrisho Gambo.

Makonda aliyekuwa na kishindo kikubwa kuliko waziri mkuu na makamu wa rais mpk leo anaogopa hata kusalimia kwenye kamera, ambazo hapo awali alimudu kuzitumia kuonya hata wazee wenye umri sawa na babu yake kwamba wawe na adabu. Hata ikibidi Makonda alitembeza sonyo (alisonya) mbele ya kamera hizo. Huyu naye siku si nyingi yuko mbioni kutoka hadharani kama Heri James kuwaomba radhi watanzania. Kama unabisha, muda utaongea.

Ndugu zangu wahenga walisema dunia duara. Inazunguka na kuuzungusha ubaya ama wema. Leo ubaya/wema unaomfanyia mwenzako kesho utakurudia.
Umewasahau Ndugai, DPP Mganga na Mwigulu
 
Ana akili sana huyo!

Unaona anavyoambana? Akija kupata ulaji huko mbele kutokana na juhudi zake hizo za kupata elimu mataahira yataanza kumtukana wakati mwenzenu anapambana kama hivyo huku nyie mnapiga porojo humu mitandaoni.
Kwamba Masters degree ndiyo itampa ulaji? Hakuna wengine wenye masters degree wako mtaani tu? Anasoma kwa kuboresha wasifu wake tu siyo kwaajili ya ulaji, kitu anbacho ni kizuri na mtu yeyote akiwa na uwezo na sifa ya kusoma afanye hivyo.
 
Wakati Gambo anaongea kuhusu uporaji wa fedha za kigeni Arusha ghafla nikajiskia kuomba kumpa taarifa muongeaji

Nilijiskia kutamka maneno haya:

"Muheshimiwa naibu Spika naomba kumpa taarifa mchangiaji kuwa wakati uporaji huo unafanyika yeye ndiye aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Zoezi lile alilisimamia yeye mwenyewe Kama mwenyekiti wa vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa

Mh. Spika, naomba kumpa taarifa mchangiaji kuwa viongozi wanaosimamia uvunjifu wa sheria za nchi ni wahaini na kwa kitendo kile alihujumu uchumi wa nchi yetu hivyo anastahili kuwa gerezani kwa sasa na sio kwenye Bunge lako tukufu"

Wakati nawaza hivyo ghafla usingizi ukaishi nikijikuta kumbe Mimi ni Uncle Jei Jei tu hata mtaa ambapo jengo la bunge lipo sijui unaitwaje. Nikajisonya tu Kama Makonda alivyowasonya Waziri Mkuu na wastaafu enzi zile akiwa Paul Makonda kweli kweli sio leo anavyotambulika kama Baba Keagan
Bahati mbaya hakuna bunge ni genge la waharifu tupu
 
Kwamba Masters degree ndiyo itampa ulaji? Hakuna wengine wenye masters degree wako mtaani tu? Anasoma kwa kuboresha wasifu wake tu siyo kwaajili ya ulaji, kitu anbacho ni kizuri na mtu yeyote akiwa na uwezo na sifa ya kusoma afanye hivyo.
PhD zimejaa kitaa lakini nao wanalia ajira kama sisi vilaza
 
Ana akili sana huyo!

Unaona anavyoambana? Akija kupata ulaji huko mbele kutokana na juhudi zake hizo za kupata elimu mataahira yataanza kumtukana wakati mwenzenu anapambana kama hivyo huku nyie mnapiga porojo humu mitandaoni.
Anafaa kuwa baba yako huyo, wew na yeye mna akili sawa, bisha?
 
Sina record na Mnyeti, hao wengine nawakumbuka walivyojikweza juu ya binadamu wenzao na kujiona ni miungu. Binadamu ni mnyama hatari sana.
 
Vijana waliofaidika na kutamba vilivyo na mfumo kandamizi wa mwendazake ni pamoja na:-
-Makonda,
-Sabaya,
-Heri James,
-Mrisho Gambo,
-Ali Hapi na
-Mnyeti.

Ilikuwa huwaambii kitu hawa. Walifanya na kusema walitakalo hata kama linagharimu maisha, mali na utu wa mtanzania hawakujali. Walikuwa malaika wakuu wa utawala ule.

Mara tu baada ya mwendazake kutwaliwa na Allah, simanzi nzito na majuto yalidhihirika usoni kwa Sabaya. Alichuruzika michozi mithili ya mtoto yatima. Alikuwa anaomba radhi kwa Muumba na watanzania kiaina

Siku hazikupita nyingi, Heri James aliyekuwa na ujasiri wa kutishia kuutoa uhai wa mtanzania yeyote muda wowote mbele ya kamera wakati wa uhai wa mwendazake, aiibuka mbele ya kamera zile zile akaomba radhi mchana kweupee bila kutaja kosa lake. Watu wakabakia na maswali Heri James anaomba radhi kwa lipi? Wenye akili wakakumbuka.

Hapi. Huyu aliongea kwa kukunja ndita usoni pake ili kuonesha vitisho vyake na kuwatusi wazee wenye nyadhifa kubwa waliostaafu bila kujali umuhimu na haiba yao kwenye jamii. Hivi Sasa amejaa wahaka ijapokuwa bado ni RC.

Mrisho Gambo enzi zake alinena maneno ya makufuru dhidi ya wafuasi na mbunge wa chadema. Alitema nyongo kila uchwao kama joka la kuzimu. Alisimamia zoezi la uporaji ktk maduka ya fedha za kigeni. Lkn sasa zigo la maovu aliyosimamia akiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa jiji la Arusha ameanza kulitua kwa kutubu kiaina bungeni. Anadai ulikuwa ni uonevu na aliyasimamia hayo kwa kupewa maagizo. Hii yote ni toba. Anatubu.

Mnyeti enzi zake aliharibu mali za aliowaona kikwazo kwenye kuyapata madaraka makubwa zaidi. Na kweli punde tu akaukwaa u-RC wa Manyara. Hivi sasa ni mbunge asiyekuwa na raha wala furaha. Amejawa na zigo la dhambi moyoni mwake. Huyu soon ataongea kama Mrisho Gambo.

Makonda aliyekuwa na kishindo kikubwa kuliko waziri mkuu na makamu wa rais mpk leo anaogopa hata kusalimia kwenye kamera, ambazo hapo awali alimudu kuzitumia kuonya hata wazee wenye umri sawa na babu yake kwamba wawe na adabu. Hata ikibidi Makonda alitembeza sonyo (alisonya) mbele ya kamera hizo. Huyu naye siku si nyingi yuko mbioni kutoka hadharani kama Heri James kuwaomba radhi watanzania. Kama unabisha, muda utaongea.

Ndugu zangu wahenga walisema dunia duara. Inazunguka na kuuzungusha ubaya ama wema. Leo ubaya/wema unaomfanyia mwenzako kesho utakurudia.
System iliyowapa kiburi bado ipo na inawalinda. Hayo maneno ya kuomba radhi ni unafiki tu mbona wengine wanaadhibiwa halafu wengine wanabadilishiwa ulaji tu?

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Makonda kama kamwagiwa maji vile......ha haha Mzee wa IST kimyaa yaani kama hayupo town vile !! Dunia hii ndugu zangu acha kabisa!!
 
Kweni vile vyeti vyake feki alivyovinunua pale Chuo cha Samaki Nyegezi havitomsaidia tena?
Endelea kuwaza propaganda za vyeti feki huku mwenzio anapeta maisha safi huku ukoo wako ukiendelea kuliwa na umasikini
 
Kwamba Masters degree ndiyo itampa ulaji? Hakuna wengine wenye masters degree wako mtaani tu? Anasoma kwa kuboresha wasifu wake tu siyo kwaajili ya ulaji, kitu anbacho ni kizuri na mtu yeyote akiwa na uwezo na sifa ya kusoma afanye hivyo.
Makonda yupo kwenye mfereji tayari wa hela!

Hao wengine wapambane na hali zao
 
Endelea kuwaza propaganda za vyeti feki huku mwenzio anapeta maisha safi huku ukoo wako ukiendelea kuliwa na umasikini
Maisha safi gani wakati pesa yenyewe ya kuzulumu Tassaf na Wafanyabiashara
 
Back
Top Bottom