Ali Mufuruki on ITV: Kilimo kwanza kiliishia wapi? Viwanda vya Saruji kupata hasara si ishara nzuri

kivava

JF-Expert Member
Apr 2, 2013
5,772
4,922
Yupo vizuri sana
Anahoji kilimo kwanza kiliishia wapi.
Asema faida za benki zimepungua sana
Viwanda vya saruji kupata hasara ni ishara mbaya
Anasifia viongozi wa Africa wanaoenda nje kutafuta wawekezaji
Amani na raslimali sio viegezo pekee cha kuvutia mitaji
GDP ya Tanzania ni 5% ya mapato ya Apples
Kujenga uchumi wa viwanda kama China kuchukua miaka si chini ya arobaini
Hakuna uwekezaji mkubwa nchini tangu ule wa migodi ya dhahabu
Kwa nondo hizi na nyingine nyingi nahisi watu wasiojulikana wanazuia sehemu ya pili wiki ijayo
 
Nimemsikiliza, ana mambo mazuri sana na uelewa mkubwa wa masuala ya uwekezaji na mitaji.

Alitolea mfano Singapore, wanapotafuta mwekezaji, wanakuwa wamefanya utafiti wa kutosha juu ya uwezo was Hugo mwekezaji wanayemtaka, na wao kama nchi wanakuwa pia wamekwisha Fanya utafiti wao na kuweka mazingira rafiki, pamoja na kumhakikishia faida atakayopata.

Pia wanamhakikishia Sera zisizobadilika badilika kwenye uwekezaji. Nimemfurahia sana, na watendaji wetu has a TIC na Waziri wa viwanda na biashara, wana kitu cha kujifunza.

Amedai, huwezi kusema tunataka kuwa nchi ya viwanda bila kuainisha aina ya viwanda, mkakati wa kupata wataalamu, mkakati wa kupata malighafi na masoko pia. Akatoa mfano, Tz kwa mwaka wahitimu mainjinia ni 1,200 nchi yenye watu milioni 50 wakati Singapore watu mil 30 inawahitimu zaidi ya laki moja kwa mwaka.
 
Back
Top Bottom