Ali Msham na Julius Nyerere

Ali Msham na Julius Nyerere

Hapa naona tatizo kubwa sana kila mtu kutaka aonekane kimchango wake.muanze kuawakumbuka na waliopigana vita majimaji basi na walionyongwa na wakoloni.watu walijitolea adi roho zao sembuse mtu katoa meza tu mnataka awekwe kwenye kumbukumbu y uhuru.jaman tuache kulalamika.we ukimkumbaka mtu kwa maudhui yake muweke kwenye kitabu au chapisho lako tutamjua¡¡¡hapa watu wanataka kuleta suala flani la udini na ukabila.mbna vitabu vipo vingi na vinaelezea watu tofauti tofauti.labda cjaelewa linakaziwa wap ili suala.

Trojaan,
Nimekusoma na nimeona kuwa huijui historia ya mapambano dhidi ya dhulma za wakoloni.

Historia hii ni moja wala haigawanyiki kati ya akina Abdulrauf Songea Mbano na Selemani
Mamba
majemadari wa Vita Vya Maji Maji waliotoa roho zao 1905 - 1907 na hawa akina Ali Msham
waliotoa fedha zao kupambana na ukoloni.

Hawa walikuwa wakipokezana kijiti.
Hebu soma hii:

ALI SONGEA MBANO
JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI

y8sYt7sUPUAGtsHd_pvfBmkzMH8tD4S1Nt3bMI0BJ3CBDQC2R42eBsmHMilReQaY7f-yf-EXUnjE48bGE15jckv4RtwbXBoDermsF8_VK-yBXVVBpb7HWz6npJPFYACHopo9Zd1KpFL0cN3dwejh4f6sQ6vrApiUKZbB_fDwDZe7EkJjpIeTjwgQB3ZW2jLVeZTfHtYuhgEUCpR40a1lkVZ9rbkJoJuS3qkDTDus1jG12r_A0FHrMbahd9QEdVuZhzOMAoVdeynjjKQpD3MhFHNNELxB5dEEsSSP7EvOXA7_iYt4pOsPtRG9zMmsVYXFq5P9F5rm-mFT_GCCNe24ap0A2D4OYc7mXTTvlelmfTWrZ9QPm0ftFuBoxx08mpJxXaA6mVNlKHa1EPedtGwDB1x8dlUGyPQuilUv8-YSxQtkeOyjo-qjFP-Os4dAOAv7CDDnSlMk5KGCy3QmPHdTiutvWWquBgctz8SbsKKugCSXN1uBzcPsN5dZX1EupF7UrxVwf8fO_lTF0jQ1cpze1d1JiTE0Mv6TybvywY0D2KuQiIRVC2i7_49LyDC3O7Ug_hp1uQ=w324-h480-no

Suleiman Mamba
​
Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale. Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah. Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao.

Ilunga Hassan Kapungu

Jumanne 19 Oktoba 2010

Kituko,
Tunaweza tukafanya mjadala wa kuheshimiana na ukumbi ukanawiri.

Ukitumia lugha kali kama hiyo tutawakaribisha watu mahodari wa hayo
mjadala utajaa matusi, kejeli nk. na tija itakosekana.

Ali Msham hadi naandika kitabu sikupatapo kujua habari zake.

Siku moja akanifuata mtu msikitini akaniambia kuwa kanisikia katika
Radio Kheri nikieleza historia ya uhuru wa Tanganyika.

Akanambia kuwa yeye jina lake ni Abdulrahman Ali Msham na baba
yake alikuwamo katika harakati za kupigania uhuru.

Abdulrahmani akaja na picha wakati ule baba yake yuko na Nyerere
akanionyesha na kunipa historia ya baba yake.

Mshume Kiyate hakuwa Mmanyema.

Lakini ningependa kukufahamisha kuwa kuhusu stori ya ''kitoweo,'' ni wewe
ndiye inakukera kwangu mimi ni katika kuonyesha ''the TANU spirit,''kama
Nyerere mwenyewe alivyoeleza.

Hapo chini ni baadhi ya picha alizonipa Ali Abdulrahman Msham zikionesha
harakati zilizokuwa katika tawi la TANU nyumbani kwao Mtaa wa Jaribu,
Magomeni Mapipa wakati wa kudai uhuru.

img259.jpg

img252.jpg
Sasa kama ulikuwa hulijui hilo tawi na lilikuwa maarufu kiasi hicho, hiyo historia yako uliyoiandika ina mapungufu makubwa na ni Historia ya kibaguzi tu,
Unalalamika wazee wako wa Gerezani wamesahaulika na ukaandika historia ya waliosahaaulika huku wewe mwenyewe ukimuweka Mzee Mshamu Kapuni, basi wapo wakina mzee mshamu wengi tu

Unatuandikia hapa uongo wako kuwa Mzee Mshamu alimfungulia mama Maria Duka La Mafuta ya Taa magomeni, lakini mwenye mama anakanusha, hii ni balaa
 
Unaandika huku umeghadhibika.
Ghadhabu inaondoa fikra njema na inakaribisha shari.

Historia niliyoandika si kuwa aina upungufu kwa kutokuandika habari za Ali Msham tu
ina upungufu kwa kuwa ni kazi ya mikono ya binadamu.

Kazi yoyote ya binadamu ina upungufu.

Hili la kasoro katika kitabu changu si jambo la ajabu katika kazi yoyote ya kitafiti.
Ikiwa wewe unajua zaidi yangu kuhusu historia ya TANU ahlan wa saalan andika tukosome.

Kuhusu ubaguzi.

Si kweli kuwa kuna ubaguzi katika historia niliyoandika na hili nina ushahidi wenye yakini
kabisa.

Kitabu hiki kimepitiwa na wasomi mashuhuri katika historia ya Afrika kama John Iliffe wa
Cambridge, Jonathon Glassman wa Northwestern University wa Chicago, Jim Brenan
wakati ule akiwa London School of Oriental and African Studies (SOAS) na wasomi wengi
wengine.

Hakuna hata mmoja katika hao aliepata kuandika na kusema kitabu changu kina ubaguzi.

Mimi sijapata kulalamika wala sijui unakusudia nini kwa kauli hiyo.

Mimi nimeona historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika imekosewa nimeshika kalamu na
kusahihisha kwa kuandika kitabu.

Huku si kulalamika.

Hakika wako akina Ali Msham wengi hawajaandikwa na ni wajibu wetu sasa tukaandika habari
zao.

Baada ya kutoka kitabu nililetewa habari za Rashid Ali Meli mmoja wa wanachama wa TANU
waliosaidia fedha katika safari ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955.

Hizo fedha zilikuwa na mkasa mkubwa sana.
Rashid Ali Meli alihudhuria kikao cha kwanza cha TANU Arnautoglo Hall, Dar es Salaam.

Baada ya kitabu kuchapwa nikapokea pia habari za Biti Kitete mama mpika uji wa Kariakoo
aliyetoa fedha si haba katika safari ya Nyerere UNO.

Michango ya wazalendo hawa wote inatakiwa kuandikwa.

Mwisho mimi sina haja ya kujibizana kuhusu duka la mafuta ya taa kwani hilo ni katika vitu
vidogo sana vilivyofanyika katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hatuwezi tukapoteza muda kwa kuvutana kwa vitu vidogo vidogo kama duka la mafuta ya taa
jirani ya kwa Mwalimu Fatina.

Mwalimu Fatina ni shangazi yetu.

Basi ikiwa mimi ni muongo na yeye ni muongo lakini napenda nikufahamishe kuwa alikuwa
mmoja wa wanawake wa Dar es Salaam walioona yote katika historia niliyoandika.

Haishangazi ikiwa duka la mafuta ya taa ni historia iliyosahaulika.

Historia nzima ya TANU iliandikwa mwaka wa 1981 na Kivukoni College na jina la Abdul Sykes
halikutajwa.

Hii ndiyo balaa kwa kuwa kadi yake ni namba 3 na mikutano ya siri yote ya kuasisi TANU ikifanywa
nyumbani kwake Mtaa wa Sikukuu na Aggrey na ndiye alikuwa mfadhili wa harakati zile.

Hakuna cha kustaajabisha sisi kukisau kiduka kidogo cha mafuta ya taa kilichokuwa nyumbani kwa
Ali Msham fundi seremala wa Kariakoo.
 
Kama hutojali naomba kupata kitabu chako ulichoandika Mohamed Said kuhusiana na historia hii ya uhuru wa Tanganyika,nipo Arusha nakipataje?
 
Nimejifunza kitu kikubwa sana, sheikh Mohamed Said, Mwenyezi Mungu akulipe kheri!
 
Kama hutojali naomba kupata kitabu chako ulichoandika Mohamed Said kuhusiana na historia hii ya uhuru wa Tanganyika,nipo Arusha nakipataje?
Kule Kwetu,
Kitabu kinapatikana katika maduka haya yafuatayo:
Slip Way Novel Idea
Tanzania Publishing House
Soma Bookshop
Ibn Hazim Media Centre, Msikiti wa Mtoro na Manyema

Maduka haya yote yako Dar es Salaam.

Jaribu na Kase Bookshop hapo Arusha kuna wakati walikuwa wakikiuza.
 
Nashukuru sana,ngoja nijaribu hapa Kase.
 
Trojaan,
Nimekusoma na nimeona kuwa huijui historia ya mapambano dhidi ya dhulma za wakoloni.

Historia hii ni moja wala haigawanyiki kati ya akina Abdulrauf Songea Mbano na Selemani
Mamba
majemadari wa Vita Vya Maji Maji waliotoa roho zao 1905 - 1907 na hawa akina Ali Msham
waliotoa fedha zao kupambana na ukoloni.

Hawa walikuwa wakipokezana kijiti.
Hebu soma hii:

ALI SONGEA MBANO
JEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI

y8sYt7sUPUAGtsHd_pvfBmkzMH8tD4S1Nt3bMI0BJ3CBDQC2R42eBsmHMilReQaY7f-yf-EXUnjE48bGE15jckv4RtwbXBoDermsF8_VK-yBXVVBpb7HWz6npJPFYACHopo9Zd1KpFL0cN3dwejh4f6sQ6vrApiUKZbB_fDwDZe7EkJjpIeTjwgQB3ZW2jLVeZTfHtYuhgEUCpR40a1lkVZ9rbkJoJuS3qkDTDus1jG12r_A0FHrMbahd9QEdVuZhzOMAoVdeynjjKQpD3MhFHNNELxB5dEEsSSP7EvOXA7_iYt4pOsPtRG9zMmsVYXFq5P9F5rm-mFT_GCCNe24ap0A2D4OYc7mXTTvlelmfTWrZ9QPm0ftFuBoxx08mpJxXaA6mVNlKHa1EPedtGwDB1x8dlUGyPQuilUv8-YSxQtkeOyjo-qjFP-Os4dAOAv7CDDnSlMk5KGCy3QmPHdTiutvWWquBgctz8SbsKKugCSXN1uBzcPsN5dZX1EupF7UrxVwf8fO_lTF0jQ1cpze1d1JiTE0Mv6TybvywY0D2KuQiIRVC2i7_49LyDC3O7Ug_hp1uQ=w324-h480-no

Suleiman Mamba
​
Nje kidogo ya mji wa Songea kuna kitongoji kinaitwa Mahenge, hapo kuna sehemu ya kumbukumbu ya vita vya Majimaji. Jambo kubwa la mahala hapo ni kaburi kubwa la halaiki ambamo askari zaidi ya sitini na… (sitini na saba) walizikwa kwa pamoja. Na kando ya kaburi hilo la pamoja kuna kaburi la Ally Songea Mbano ambae yeye alizikwa peke yake.

Kwa mara ya kwanza nilitembelea makumbusho hayo mwishoni mwaka 2007. Baada ya kusaini kitabu cha wageni na kulipa ada ya kituo muhudumu wa kituo hicho alitupa karatasi yenye orodha ya majina ya wale wote walionyongwa na kuzikwa hapo. Ukiitazama orodha hiyo na hasa ukiwa Mwislam jambo moja litakustuwa. Robo tatu ya walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam. Linaanza jina lake la Kiiislam, kisha kwenye mabano kuna jina la Kikristo na mwishoni linaishia jina la kiasili, mfano Abdulrahman [Dominic] Mputa Gama.

Muhudumu akatueleza kuwa hawa mashujaa wa vita vya Maji Maji kabla ya kunyongwa alikuwako padri ambae aliwabatiza na kuwapa majina ya Kikristo na baadae kunyongwa, wengi walibatizwa kwa hadaa kuwa wakibatizwa wataachiwa huru, wote katika hao walionyongwa walikuwa ni Waislam. Uzuri ni kwamba katika orodha hiyo kulikuwa na jina na sahihi ya yule padri aliyewabatiza, na kwa mkono wake [huyo padri] aliiyaandika hayo majina. Karatasi yenyewe ilihifadhiwa vizuri kwenye fremu ngumu ya kioo. Tuliomba kwa nguvu zote kupatiwa hiyo karatasi ya majina hata kwa kununua lakini haikuwezekana pamoja na kuwaona na kuwaona wakubwa wa kituo hicho. Niliporudi kwa mara ya pili mwezi July 2009 nilipata mstuko.

Karatasi iliyohifadhiwa kwenye fremu ngumu ya kioo, iliyokuwa na majina ya Kiislaam ya mashujaa wa vita vya Maji Maji, haikuwapo,na badala yake imewekwa karatasi nyingine ombayo ndani ya karatasi hiyo majina ya Kiislaam ya mashujaa hao wa vita vya Maji Maji yameondolewa na kuachwa majina ya ubatizo na yale ya kiasili tu, jina la padri, sahihi yake na wadhifa wake katika Kanisa Katoliki pia vimeondolewa na karatasi yenyewe haikuwa kwenye fremu ya kioo na ilikuwa katika fotokopi tu.

Nilimuuliza muhudu kulikoni? Akasema, “Songea pana mzee mmoja maarufu sana katika historia ya TANU na historia ya kuasisiwa Bakwata anaitwa kwa kifupi M. S. Mzee huyu ana binti yake ambaye ameolewa na Mzungu wa Kijerumani. Binti huyu na na mumewe wa Kijerumani walikuja hapa Songea matembezi. Hivyo kwa shinikizo la huyu mzee M.S. karatasi hiyo alipewa huyu Mzungu kwa ahadi kwamba anaipeleka Ujerumani na atairudisha. Hivyo ndivyo karatasi ile asilia ilivyotoweka. Kubwa katika karatasi ile ni ule ushahidi wa majina kuwa wote katika wale walionyongwa na kuzikwa hapo ni Waislaam, wengi katika hao walihadaiwa kuachwa huru hivyo wakabatzwa ispokuwa wachahe sana waligoma kama shujaa Ally Songea Mbano. Huyu kwa ushujaa wake wa kupambana na Wajerumani aligoma na akasumbua sana kiasi akanyongwa siku yake na peke yake na ndio sababu akazikwa peke yake.

Ukiingia ndani ya kinyumba cha ghorofa, unaanza kuona picha za mashujaa wa Maji Maji wakiwa wamevaa mavazi ya vita mithili ya mahujaji wanavyovaa Ihraam wakati wa hija. Kinachoongezeka kwao ni vilemba kichwani. Chini ya kila picha kuna jina la aliyekuwa kwenye picha ile. Ukipanda gorofani utaona silaha za kiajadi kama mikuki, pinde, ngao n.k. Kinachosisimua zaidi ni mavazi ya vita. Mavazi ya vita ya askari wa Maji Maji wengi walivaa kanzu za Kiislaam na vilemba. Jambo jingine linalosisimua ni kile ambacho watu wa kituo hicho wameandika ”rosary” hili ni jina la Kikristo, hasa la Kikatoliki, ni zile shanga ambazo huning’inia msalaba lakini unapotazama hicho kilichoitwa “rosary” utaona si “rosary,” bali ni tasbihi hasa ya Kiislaam yenye kupangika hasa shanga zake, 33, 33, 34. Maneno yaliyoandikwa kuelezea “rosary” hizo ambazo ni tasbihi ni:

“Hizi ni rosary ambazo wapiganaji wa majimaji walikuwa wakitumia KUTAMBIKA kabla ya kwenda vitani kwa kuamini kwamba zitawakinga na risasi.”

Ukweli ni kwamba hawa askari wa Maji Maji wengi walikuwa ni Waislaam hivyo hawakuwa WAKITAMBIKA bali walikuwa wakitumia tasbihi hizo kufanya dhikri kwa Allah kabla ya kwenda vitani. Midhali sisi Waislaam hatujawa tayari kuandika historia yetu kama Waislaam wanaotuandikia watapotosha na kupindisha na kutuzulia wanavyotaka. Hapo gorofani kuna jambo jingine la kusisimua. Kuna magudulia na makopo. Wameandika kuwa, haya ndio makopo ambayo askari wa Maji Maji walikuwa wakiyatumia KUNAWA kabla ya kwenda vitani [kushika udhu na sio kunawa] pia kwa kuamini kuwa maji hayo yatawakinga. Muhudumu alitueleza kuwa kumbukumbu nzuri na za kuaminika ziko Jimbo Kuu la Wakatoliki Peramiho.

Tulikwenda jimboni lakini hatufanikiwa kwa sababu za ki-urasimu tu.T ulitakiwa tupate kibali cha Askofu Mkuu. Hatukukipata. Kwa yale tuliyoyaona na kuyashudia yafuatayo:

Vita vya Maji Maji havikuwa ni vita vya kizalendo, kwamba wazalendo walikuwa wakipigania nchi yao. La. Vilikuwa ni vita vya Waislaam wakipigana na Wakristo wa Kijerumani waliovamia maeneo asilia ya Waislaam kwa lengo la kuuwa Uislam na kusimamisha Kanisa kwani mazingira yote utayoyaona ya mashujaa wa vita vya Maji Maji ni mazingira ya Kiislaam, kingine ni kwamba hukuti mahala yalipo makaburi ya askari wa Kijerumani ila katika miji ya Waislaam kama Kilwa, Bagamoyo n.k. Kwa nini wauliwe maeneo ya Waislaam tu? Walifuata nini huko?

Kuna upotoshaji mkubwa sana wa historia ya vita vya Maji Maji. Vinaoneshwa kama ni vita vya wazalendo wakipigana na wakoloni wa Kijerumani, wakati ukweli si hivyo. Ukweli ni kwamba vita vya Maji Maji vilikuwa ni vita baina ya Waislaam na Wakrito wa Kijerumani, Waafrika Wakristo wa Songea walijiunga na Wakristo wenzao wa Kijerumani dhidi ya Waafrika wenzao wa Kiislam.

Wakristo wameitafiti hakika hii na wakaijua kisha wameificha kwa maslahi yao.

Kuna haja ya wasomi wetu wa Kiislaam kufanya juhudi za makusudi za utafiti wa historia yetu ili kukifanya kizazi hiki cha Kiislaam kujitambua zaidi na kujenga ujasiri. Taasisi za Kiislaam na watu binafsi [matajiri] wawawezeshe kiuchumi wasomi hawa kufanya kazi hii.

Mwaka 2008 nimetembelea Kilwa Kisiwani, huko nikamkuta Mzungu wa Kifaransa akiandika historia ya Kilwa Kisiwani akiitwa Thiery, ameweka kambi na majenereta ya umeme, solar power na makompyuta. Kazi nyingine kubwa alokuwa akifanya ni kukarabati yale magofu ambayo mengi ni misikiti na majumba ya mawe ya wafalme wa kale. Kilwa Kisiwani ni moja kati ya dola kubwa za Kiislaam katika mwambao wa Afrika Mashariki, ndio dola ya mwanzo kuwa na sarafu yake ambayo iliandikwa jina la Allah. Tuliposoma kazi ile ya Yule Thiery Mfaransa tayari alikwisha ipotosha kwa kiasi kikubwa. Sikuwa na la kumfanya. Kizazi cha vijana wa Kiislaam hakitopata historia ya kweli ya Kiislaam kama tutawaacha akina Thiery waandike na hivyo vijana wetu hawatajitambua na hawatokuwa na ujasiri katika Uislam wao.

Ilunga Hassan Kapungu

Jumanne 19 Oktoba 2010

Dini haikupeleki mbinguni kwa mungu baba. Kutenda Yale aliyihaidi mungu ndio njia salama
 
Ze Keke,
Hayo uliyosoma ndiyo yaliyokifanya kitabu hiki kipate umaarufu katika vyuo vingi
na kipendeke na wengi hapa nyumbani.
 
Allen,
Huo haukuwa mchango mdogo.
Ulikuwa mchango mkubwa sana.

Achilia mbali thamani ya samani.
Wakati ule kujinasibisha na TANU ilikuwa kujitafutia matatizo na wakoloni.

Ali Msham alijitolea chumba kimoja nyumbani kwake kiwe ofisi ya TANU.
Hakuishia hapo alimfungulia Mama Maria Nyerere kijiduka kidogo cha
kuuza mafuta ya taa.

Jioni nyakati za Maghrib ishaingia mtoto wa Ali Msham alikuwa ndiye
akimsindikiza Mama Maria nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.

Wakati ule Magomeni miembe mitupu na kiza kikiingia panatisha kwa
mwanamke kutembea peke yake.
asante mwalimu saidi kwa haya tusiyoyajua wengine. M. Mungu akupe umri mrefu katika dunia hii na akupe makazi mema ya maisha ya akhera.
 
Harakati za kudai uhuru huwezi kufananisha na swala la ada,maana hata huyo nyerere kungekuwa na mtu kamlipia ada watu hawawezi kulalamika kwa kutomzungumzia huyo mfadhili wake wa ada,hapa swala ni harakati za kudai uhuru kuna watu hawatajwi kabisa kila jambo nyerere kitu ambacho sio kweli,nyerere hasingeweza kufanya chochote bila msaada wa hao watu.huo ndio ukweli hata kama hupendi kusikia habari za namna hiyo.
Historia haina muandishi maalum, hata wewe unaweza kuiandika, inategemeana na scope ya muandishi, na consumers wa historia hiyo!
Mfano historia ya nchi haiwezi kutaja hadi waliotoa meza, walimpangisha chumba huko Magomeni baada ya kufukuzwa pugu etc! Kama mwalimu angeandika au angeandikiwa kitabu cha maisha yake tunatarajia mazungumzo ya aina hiyo! Lkn kwa historia ya nchi sidhani kama lina umuhimu sana!
Kwa upande mwingine, watu wa pwani mnanafasi ya kuiandika historia inayoonesha mchango wenu ktk kuleta ukombozi Tanganyika, mnaweza kuweka hiyo historia ktk vitabu vyenu ili wajukuu zenu wajivunie hapo baadae! Madhumuni ya historia ya namna hii na consumers wake ni watu wa jamii fulani na hivyo haiwi historia ya taifa, lkn unaweza kuiweka ktk archives ambapo watu wanaotaka kuijua historia vema wanakusanya maandiko tofauti na kuyaunganisha ktk mtindo utakaowafaa wao!
So ndugu huna haja ya kumlaumu mtu, we nenda kakusanye taarifa za kina mzee mshamu na wengineo ili uandike vema historia ya nchi yako na mchango wa jamii yako ktk taifa!
 
2Kimo,
Bahati mbaya umenaswa na mtego uliowanasa wengi.
Ali Msham hakumbukwi kwa kutoa samani ofisi ya TANU.

Ali Msham alifungua tawi la TANU nyumbani kwake, kuuza kadi za TANU na kuhamasisha umma usimame kumkabili
Muingereza.

Hebu angalia hii picha hapo chini:

DSCN1797.JPG

Kulia: Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Julius Nyerere (amezibwa na John Rupia) na Zuberi Mtemvu (aliyeshika tama). Picha hii imepigwa kwenye tawi la TANU Magomeni Mapipa, Mtaa wa Jaribu nyumbani kwa Ali Msham.

img252.jpg

Hili la kwanza.

Pili.
Historia niliyoandika mimi si ya watu wa pwani peke yao ni historia ya uhuru wa Tanganyika.
Angalia picha hii nyingine hapo chini:

hFhtcnd0XuejvUxiptsfwKQ-40wes8LVcIt_dafssqqmfVl3gSGTAoehfPB4DbMhrvvl1sp8CyDjLjop6szzWOU0asptjzVL3V2Mn7JHySiqtYPVVhUuRNQCwEpTOCNVUBJOHtgYXiJHIHmyOgYP5K1lDTszPEpKSsXgbIfS_kgh43mwAyjCThNJJWoHgjnJI5nD6FRYXwJNuh0K63xdwGS0pFpLps-coPyHrC3ErWPmQd5z8nsUrlUTNgEie8txCrvCj0ksI3se1s359p_mUJwK-kn0__O_-w8KFZSVXnSF81OdFaENKmHo7vlZozJskUYaiF9xLbDvlKhMNXeyVcqkkE_ZWxKFNuyPU4cM6dQOxdaD0GnHc_OUjd0J-B_zoKOA4Rj5sZyeZGld1x_tYFP8loSwJWNXr0MSxnZM6PfkvR4PN06c4D_MchmZmm6M_kLwhKx9vHrikGf08ZvAURpkXULNJMXTE3xxZVCKj9oJWgXk0KC4PFuS8pkmrs-xWOSLx-ku8FauxBqo_cr3Bj5KrfkfuA8W4lq4QA7EBpS7W_WBu090OnyM0pe6T01-uilclQ=w480-h360-no

Kushoto: Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiya, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu wakiwa Dodoma Railway Station 1955/56​
 
Kaka Mohammed hakuna sehemu niliyobishia kazi yako!
Nimekuheshimu sana katika your initiative ndio maana nimesoma na kukuelewa vizuri tu!
Niliyekuwa namjibu ni Yule aliyekuwa akilalamika kuwa wapo watu hawakutendewa haki kwa kuwa hawakuandikwa!
Kuna ukweli huwezi kubishia, hii historia yako unayoiandika lengo lake kuu ni kuweka jamii iliyohusika ktk mchango wa kuijenga TANU na kuleta Uhuru lkn kwa bahati mbaya au makusudi haikukumbukwa ktk vitabu vya historia vya nchi hii!
Hapa unarejea zaidi jamii za pwani na waislam ambao mchango wao hauonekani kabisa kwa sasa na ipo dalili za kufutika!
Mimi pia ni mtu wa jamii hizo unazozingumzia hapo, babu yangu aliichangia sana TANU na nakumbukà wakati wa kifo chake walikuja kina Marehemu Thabit Kombo, Kitwana Kondo, bibi Titi, Kawawa, Abdul Jumbe na viongozi wengine wengi ambao Mimi siwajui kwa kuwa pia nilikuwa mdogo, Nyerere hakufika ktk msiba lkn Kawawa alimuwakilisha kama miongoni mwa viongozi wa TANU! Wasifu wake ktk mazishi alikuwa ni miongoni mwa wapambanaji wa TANU labda kwa kutokujua significance ya historia juu ya mchango wa mwanajamii hakuna aliyeangalia au kuzingatia details za mchango wa watu wengine, Ila wenyewe ktk level zao wanaweza kujua nani alikuwa na umuhimu upi!
Mimi najua wengi wetu hasa sisi waswahili huwa hatuna tabia ya kuandika historia, tunasimulia na kurithisha hadithi hizi Ila ukweli significance yake inapungua kizazi hadi kizazi! Mimi najua watoto wangu hawatojua kabisa kama ktk ukoo wao kuna watu wakipambana katika front line wakati wa ukombozi wa Mtanganyika na pia walishiriki ktk kusaidia mapinduzi ya Zanzibar!
Siwezi kulalamika, tulipaswa kukusanya hizi taarifa na kuziweka, tuziandike na tuzisambaze ili hata kama jamii nzima ya watanzania haitoona umuhimu, lkn jamii husika zijione kuwa zilikuwa na mchango ktk nchi yao!
@ Mohammed Said Mimi nauheshimu sana kazi yako, nauheshimu mchango wako kwa kundi hili la waliosahauliwa na historia! Nakuheshimu pia kwa kuweza kufanya yale ambayo sisi Wengine yametushinda! Ni kazi sana, Mimi nashindwa kupanga historia ya ukoo wangu kwa kujua vizazi vitatu tu vilivyonitangulia, wewe leo unaandika historia ya jamii pana ya watanganyika nitabeza vipi juhudi zako!
 
Wasioupenda ukweli kwa sababu tu wao hawamo katika huo ukweli na wao ndio wa kwanza kuwaponda waliomo kwenye huo ukweli wanaghadhibika kweli kweli.

Ukisoma uzi huu utawaona kweli.
 
Samahani sana ndugu yangu.
Inaelekea nimechanganya majina.

Niwie radhi kwa kosa hilo.
 
Wasioupenda ukweli kwa sababu tu wao hawamo katika huo ukweli na wao ndio wa kwanza kuwaponda waliomo kwenye huo ukweli wanaghadhibika kweli kweli.

Ukisoma uzi huu utawaona kweli.
Maalim Faiza,
Umekuwa kimya kwa muda mrefu.
 
Back
Top Bottom