Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,452
- 34,004
- Thread starter
- #21
Allen,Mzee Mohamed Said nakubaliana kama Ofisi ilikuwa haina meza bora kama hiyo na Ally Mshamu (Bila shaka ni mmatumbi) akaitoa Meza hiyo bila shaka ulikuwa ni mchango mkubwa sana, lakini kwa Mwalimu mwenyewe kwenda kuipokea badala ya kumtuma mtu mwingine inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa anathamini mchango wa kila mmoja. Lakini kwa wakati huo pia kama Mama maria alikuwa na duka hapo kwa Mshamu na lazima aende kulala kwake Magomeni Majumba sita si ajabu kwa mtoto wa Mshamu kumsindikiza bi mkubwa huyo.
Huijui historia ya TANU ndiyo maana unapata tabu kuelewa.
Halikadhalika hujui kwa nini mimi niliamua kuandika historia
ya TANU wakati ilishaandikwa na Chuo Cha Kivukoni.
Nyerere hakuwa na mtu wa kumtuma pale New Street.
Hiyo kuhamasisha ndiyo ilikuwa kazi ya wanaharakati wa TANU.
Angalia picha hii ya Ali Msham (waliosimama wa pili kushoto) na
Bibi Titi Mohamed wakiwa na wanachama wa mwanzo wa TANU
Magomeni 1955:
Kushoto katikati ni Bi. Titi Mohamed na binti yake Halima.
Naamini taratibu utaipata picha ya hali ilivyokuwa wakati wazee wetu
wanaanzisha harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.