Ali Kiba ahojiwa kifo cha Kanumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ali Kiba ahojiwa kifo cha Kanumba

Discussion in 'Celebrities Forum' started by KIM KARDASH, Apr 15, 2012.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Ali Kiba[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Ali Kiba, anadaiwa kuhojiwa na polisi kwa maelezo ndiye aliyempa Elizabeth Michael Lulu msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Steven Kanumba.

  Lulu ndiye anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.

  Kachelo aliyemhoji Lulu Jumatatu wiki hii, amedai kuwa msanii huyo alihojiwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye aliyempatia lifti baada ya kutoka kwa Kanumba.

  Mwanaspoti lilimtafuta Ali Kiba ili azungumzie taarifa hizo, alipopatikana kwa njia ya simu, msanii huyo alisema: �Samahani kaka siwezi kuzungumzia chochote kuhusu mambo hayo.� Kisha akakata simu.
  Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano wiki hii na kutotakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.

  Lulu alitoa maelezo yake polisi Jumatatu ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba., ambapo alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.

  Taarifa za uhakika ambazo Mwanaspoti limezipata kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) aliyetoka makao makuu alifanikiwa kufanya mahojiano na binti huyo ambaye awali aligoma.Imeelezwa kuwa, alitumia takribani sasa tatu kumlainisha Lulu azungumze.

  Katika mahojiano na gazeti la The Citizen Jumanne, kachero huyo ambaye alitoka katika Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai alisema tayari amemhoji mtuhumiwa namba moja Lulu pamoja na msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya kufuatia kifo cha Kanumba, aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi.

  Akimnukuu Lulu katika mazungumzo yake, kachero huyo alisema Lulu aliitwa na marehemu Kanumba ili waweze kutoka (out) kwenda kwenye bendi ya Mashujaa ambayo ilikuwa inapiga kwenye kiwanja chao cha nyumbani, Vingunguti.

  Mtuhumiwa alionekana kutokuwa tayari, lakini marehemu �akamlazimisha�.
  Kachero huyo alisema: �Lulu anadai alifika nyumbani kwa marehemu saa tano usiku, lakini akiwa ameweka msimamo wa kutokwenda sehemu yoyote usiku ule, lakini Kanumba alikuwa akilazimisha ndipo yakatokea mabishano na marehemu akafunga mlango kwa funguo.

  "Hata hivyo, baada ya ugomvi wa kama nusu saa hivi, Lulu alifanikiwa kuondoka chumbani humo na alifungua mlango kwa taharuki na kuondoka bila kujua kilichotokea nyuma, huku akimweleza ndugu wa marehemu kwamba Kanumba ameanguka."

  Mpashaji habari wetu huyo alisema, kumekuwa na jumbe fupi za maneno kutoka kwa wanasiasa ambazo zimekuwa zinaingia kwenye simu ya kiganjani ya Lulu, zikiahidi kumsaidia.

  Alionya kuwa kama wanasiasa wataanza kuingilia uchunguzi wa Polisi katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi, wanaweza kuharibu mambo. Lakini yeye mwenyewe akionyesha kwamba yuko imara na anafahamu anachokifanya.

  Kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, kachero huyo alisema kwamba alihojiwa kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kama mtu aliyempatia msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Kanumba.
  Kachero huyo alisema kutokana na taarifa ambazo wanaendelea kuzipata, kuna uwezekano watu wengi zaidi wakahojiwa ili kujiridhisha kabla ya �watuhumiwa� kuanza kupandishwa kizimbani baada ya upelelezi kukamilika.
   
 2. KISHOKA_ZUMBU

  KISHOKA_ZUMBU Senior Member

  #2
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Asante mtaalam kwa taarifa hii iliyoshibishwa ikashibika
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Mtani, Mnyisanzu says thank you for this useful post. Tusubiri.
   
 4. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hao wanasiasa wawe makini sana na hizo sms na ikiwezekana waache kabisa kutuma!
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  kim habari nono hii. sasa mbona maelezo ya LULU ni tofauti na yale yaliyosemwa mwanzo kuwa ni simu ilipigwa na lulu akaipokea akiwa nje, hivyo Kanumba akakasirika? sasa iliambiwa ni wivu wa mapenzi na hapa tunaambiwa ni outing, jamani haya mambo yataibua mengi. anglia na hao mashujaa band watakuwemo huko.

  huyu Ali kiba nayeye alimpeleka wapi? nyumbani kwa akina lulu au alimpeleka kwake (nyumbani kwa ali kiba) na lulu alikamatwa wapi akiwa anafanya nini na nani? naomba nijibiwe haya maswali manake nashindwa kupata connection.
   
 6. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #6
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wanasiasa wa bongo kwa vimbelembele......
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Bongo bana, ni zaidi ya uijuavyo: yaani mtu anachaguliwa na wananchi kuwawakllisha kutunga sera na kusimamia maendeleo yao- leo anarusha vi-text kwenye simu ya mtuhumiwa aliyechini ya ulinzi mkali kabisa huku na simu nayo ikiwa bado ni kielelezo muhimu!, katiba mpya itoe mwanya kwa wapiga kura kumkataa muwakilishi anaye-misbehave.
   
 8. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #8
  Apr 15, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Du imbombo ngafu
   
 9. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #9
  Apr 15, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Vipi kuhusu mzinga wa JACK DANIELS
   
 10. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #10
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,654
  Likes Received: 3,301
  Trophy Points: 280
  Wacha wanasheria waendeshwe na wanasiasa!wamezoeshwa rushwa hivyo kila panapokuwa na kesi kubwa huwa wanaacha nafasi ya kupenyezea rushwa!!hakuna lawyers tanzania!!wote njaa tupu,hayo maelezo ya huyu mnaemwita mtaalam nayo yanapingana na yale ya awali,nahisi harufu ya rushwa tena hapo!!sasa kumbe alifungua mlango na kutoka bila msukumano wowote!then kaenda kumweleza ndugu yaje kuwa SK kaanguka bila sababu!Mm,
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Apr 15, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,395
  Likes Received: 414,707
  Trophy Points: 280
  tuliwachagua watusaidie kwenye mema na rabsha...........waache waje tu.......
   
 12. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,692
  Likes Received: 12,737
  Trophy Points: 280
  mbona Alikiba alihojiwa na kituo fulan cha radio jana alikana kuhojiwa na polisi na alisema atasiku ya tukio hakuwepo nchini. Tujiulize nani mkweli? na aliendelea kuchezesha taya kwamba habari za kifo cha k alizipata kupitia simu,na yeye akahamua kumpigia lulu simu haikupokelewa!
  ???????????????????????????????????????????????
   
 13. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #13
  Apr 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Ali Kiba abinywe hadi amtaje aliyekuwa anampelekea ngozi, maana huyo ndo muuaji wa jembe letu!
   
 14. J

  JOJEETA Senior Member

  #14
  Apr 15, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sa hao wanasiasa!cjawaelewa jaman,,,,,,,,ama kweli maisha bora kwa kila mtanzania kazi ipo
   
 15. Lisa Rina

  Lisa Rina JF-Expert Member

  #15
  Apr 15, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 1,769
  Likes Received: 2,022
  Trophy Points: 280
  Vitu ata havieleweki,inamana alikiba alipigiwa cmu sangapi adi aje kwenda mchukua lulu kwa kanumba?au ye ndo alompeleka akawa anamsubiri nje amalize mambo yake afu ndo wasepe.mbn havieleweki ivi vitu unaeza pata kichaa da!kweli lulu mwaka huu katupata!
   
 16. I

  Independent Voter JF-Expert Member

  #16
  Apr 15, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 279
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini mimi kwenye dawati langu ninazo taarifa kwamba Ali na Lulu ni wapenzi na Lulu ndio anaempenda sana Ali k
   
 17. Interest

  Interest JF-Expert Member

  #17
  Oct 20, 2017
  Joined: Apr 11, 2015
  Messages: 934
  Likes Received: 1,258
  Trophy Points: 180
  Huyo lazima aitwe tena kuhojiwa aisee..
   
 18. Maxmizer

  Maxmizer JF-Expert Member

  #18
  Oct 20, 2017
  Joined: May 22, 2017
  Messages: 2,346
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  kaburi limefukuliwa
   
 19. magnifico

  magnifico JF-Expert Member

  #19
  Oct 20, 2017
  Joined: Jan 14, 2013
  Messages: 2,891
  Likes Received: 2,146
  Trophy Points: 280
  Kipindi hicho hana timu.
   
 20. Joshua kibale

  Joshua kibale Senior Member

  #20
  Oct 20, 2017
  Joined: May 9, 2017
  Messages: 105
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Hapa tutulie tuu. Ukweli utapatikana. Kama LULU na Alikiba ,Wanajua au wanaficha kilichotokea.
   
Loading...