Algeria ni salama zaidi kwa Simba kuliko Zanzibar

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Tunaojua Sanaa ya Vita tunajua kamwe usiruhusu adui yako akakuchagulia silaha. Daudi alipoingia uwanja wa vita kumkabili Goliath alikataa kuvaa na kubeba silaha alizopewa, akalazimisha kwenda na vikokoto vyake alivyovizoea kila siku. Watu wakamshangaa huyu vipi, ana akili kweli? Mwisho wa siku wote tunajua nani alilazwa chini.

Bado hatujajua hatma ya mechi ya pili ya fainali kati ya Simba na Berkane na inawezekana kabisa kwamba mechi inaweza kuchezwa Zanzibar na Simba kibishibishi ikachukua ubingwa ila narudi kule kule, kamwe usikubali adui yako akakuchagulia silaha ya kupambana naye.

Kama ile barua ya kuongea na Algeria watupe uwanja ni kweli, ni sahihi kabisa kwenda huko. Hapo tunaongea na serikali ya Algeria wasiruhusu mdudu yoyote shabiki wa Belkane kuingia kwenda kuangalia mechi, sisi tunajivua lawama zote za kitakachotokea huko. Na jezi zao zile zenye bendera ya Morocco hawataruhusiwa kuzivaa ndani ya Algeria. Fainali ichezwe bila mashabiki tuone kama hao CAF watafurahi.

Mwisho wa siku ni lazima tuheshimiane.
 
Hivi ulishatoa maelezo bwana mtabiri au ukikimbia🤣🤣🤣🤣
 
Kwenye mpira huwezi kumuadhibu mtu bila kosa labda kwenye nchi ya bundi yaani ccm.
 
Mlipoambiwa fanyeni usajili mkawa mna puuza, ona sasa mnavyo dhalilika!
 
Kuna timu Africa hii inayojua kutumia njia za panya na liuwanja lao kushinda kama TP Mazembe? CEO wao wa zamani mnaye huko utopoloni.
Mnahangaikaaaa maana mshaona hamtoboi. Mmeanza kutafuta visingizio🤣🤣🤣
Kipigo kiko pale paleeee.
 
Ukitoa kukukanda kwa upumbavu wako kuna kitu huwa nakwambia.

QUALITY.
QUALITY.
QUALITY.
 
😂😂😂😃 ujinga gani huu.... Kwahiyo Algeria ndio kutakuwa na mashabiki wengi kuliko Zanzibar? Au ndio home advantage kuliko Zanzibar?.
Au mnadhani mnaweza kunufaika na migogoro yao ya kisiasa?. 😃😃
 
Kama msitiaga fitina fainali ya Yanga kipindi kile, haya yasingetokea
 
Back
Top Bottom