Alert: Tujihadhari matapeli mlimani city | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alert: Tujihadhari matapeli mlimani city

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Kottler Masoko, Oct 29, 2011.

 1. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mambo mazito leo yamenitokea hapa mlimani city,nilitangaza hapa jamvini kwamba nauza laptop,kuna jamaa mmoja akaniambia kwamba yeye anaitaka.baada ya mawasiliano ya takriban siku 2,leo akanambia tukutane maeneo ya mlimani city,alikuja na mwenzake na carina ya silver yenye namba hizi T443 BHN,baada ya kuangalia mali na kuipenda,jamaa mmoja akasema anaenda ATM kuchukua pesa,ghafla alipofka ndani akanipigia simu niende pale Merry Brown,na me kwa imani na amani nikaacha machine ktk gari yao na yule dereva wake,lakini nikawa na wasiwasi nikaandika kwanza namba ya gari ktk simu then nikaenda,nilipofika pale merry brwn ckumuona jamaa na nikampigia simu akawa ananielekeza kule vyooni,me ckwenda na nikatoka nje nikakuta ile gari yao inatoka kwa kasi,kupiga simu(0719359573) jamaa akawa hapokei na muda si mrefu ikawa haipatikani.then nikawa nimeibiwa laptop yangu kizembe zembe tu.nimeriport hii issue polisi udsm na RB ninayo,nataka ni deal nao slowly na Mungu ni mwema nitawapata wakiwa hai au vinginevyo.
  Nikiwa kama mwana jamvi ninayetakia mema wanajamvi wenzangu,nimeleta hili swala hapa kwanza kama tahadhari kwa wale watu wanaouza vitu yasije yakawakuta,pili Jamii Forum iangalie kama kuna measures za kuweza kusaidia hawa matapeli kunaswa kwa kulitafuta hilo gari husika au simcard details na nikipita taarifa ktk PM niweze kushirikiana na mpelelezi kuwatia nguvuni hawa vijana wapenda jasho za wenzao.
  Naomba kuwakilisha na Msaada wenu nitaushukuru sana.
  Jihadharini Wadau!!
   
 2. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Kwa kumbe JF inasomwa hata na wahalifu sku izi? Sku ingine usifanye dili uchochoroni au njiani, waite ofisini kwako au pahali popote penye nidhamu, halafu ukiwa suspicious na kitu chochote call off the deal immediately!
   
 3. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Duh mkuu pole sana!
   
 4. Kottler Masoko

  Kottler Masoko Senior Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yaani,nimeapa nitakufa no hwa jamaa,nshukuru data zangu zote zpo ktk external. Nimeongea na wale maaskari wa parking wanasema jana yke kuna dada kalambwa million 5 alikua ananunua gari toka kwa watu wa design hiyo. Thanks Mkuu.
   
 5. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Pole..but
  1.Kilichokufanya kuwaamini hao jamaa namna hiyo ni nini ?
  2.Ulienda kumfuata wa nini ili hali kakwambia anaenda kuchukua pesa kwenye ATM?
  3.ungeshindwa kabisa ungechukua laptop yako kabisa badala ya kwenda na mizinga yako tu..(isingekugharimu kitu)
  4.Number za gari ulizochukua zinaweza zisisaidie sana maana wanaweza kuwa wamefunda za Toyo

  Jaribu kuomba msaada wa jamaa wa mitandao ya simu husika wacheki number mbili tatu za huyo aliyekuwa anakupigia inaweza kusaidia kuwapata jamaa zake wa karibu na ukafanikiwa kumdaka ..though ushirikiano wa hawa jamaa ni mdogo sana au jaribu kucheki na TCRA japo gharama unazoweza kutumia ni half price ya hiyo laptop..inahitaji subira kutekeleza hili,

  kama unaamini kuwa kuna nguvu za Mwanga/Nuru basi amini pia kuna Nguvu za diza..
  nikupe number ya jamaa aliyerithishwa mikoba ya shekh nanihii kisha laptop iwe tumboni kwa jamaa siku ya pili laptop umeletewa tena watakufuata...kama unaamini lakini

  In general say we ni mzembe sana na ungekuwa mwanangu lazima viboko kwanza ..huwezi kutapeliwa kirahisi namna hii
   
 6. Sokwe Mjanja

  Sokwe Mjanja JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu, kuna sehemu nyingine ulikuwa umetangaza au ni hapa JF tu kwa maana ya kuwa hao jamaa wametokea humu?

  Kama wametokea humu ni dhahiri JF is not safe imeingiliwa sasa, tuwe makini sana na hata pm tuanze kuwa na mashaka nazo au love connect.

  Hii kitu wazee hutokea jamani, haina maana kabisa kuanza kumlaumu kiongozi katika hiki kipindi kigumu alichopo. kama unaweza kumsaidia aipate laptop yake msaidie kama huwezi kaa kimya tu, azawaiz utuhakikishie wewe ni mjanja na msafi sana hujawahi kufanya uzembe maishani mwako hata mdogo kiasi gani.
  Cha kufanya ndugu muhanga jaribu kuulizia kuna vijiwe fulani huwa vitu vya hivyo vikiibiwa huuzwa nadhani ni mkwepu au sehemu fulani (wanaojua zaidi watatujuza) unaweza kuipata laptop yako japo zitakutoka fweza kidogo, kuwa mpole tu usiwe na hasira katika hili utaikosa moja kwa moja.

  Otherwise pole sana mkuu, kupoteza laptop sio mwisho wa maisha, Mungu atakuongoza utapata ingine
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu unajua nimeshtuka lakini nikakumbuka wabongo wengi ni wahalifu be it white or blue collar, ni sehemu ya maisha ya watanzania wa leo.
   
 8. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,171
  Trophy Points: 280
  Pole sana bro, huenda hata mie ningetapeliwa kama wewe. Sikulaumu wala sikucheki. Asante kwa kutujuza utapeli mpya
   
 9. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapa huna wa kumlaumu..hao jamaa umewaweka mwenyewe into temptetion. Utawaachiaje loptop watu ambao huwafahaamu? Laptop yako ilikuwa nzito kiasi cha kushindwa kwenda nayo hapo Marry brown kufanya exchange? Siwezi kukupa pole wa kutoa msaada wowote kwa hili. Inabdi ukubali umefanya uzembe na umeibiwa kijinga!
   
 10. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, Pole sana mkuu, hapo ndipo huwa naamini hawa jamaa huwa wanatumia mazingara maana mazingira wanayoibia yaani hata mwenyewe huwezi amini.
   
 11. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  EasyMutant siku ya kufa kwa nyani miti yote huteleza, unaweza kuibiwa uwizi wa kijinga kabisa. Kiini cha uwizi ni jamaa kuwaamini hao washikaji kupita kiasi.
   
 12. IGUDUNG'WA

  IGUDUNG'WA JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 22, 2011
  Messages: 1,998
  Likes Received: 887
  Trophy Points: 280
  pole sana mkuu jaribu kuwasiliana na makampuni ya simu anangalau wakupe jina la huyo jamaa maana najua atakua amesajiri hiyo line, baada ya hapo unakamata km kuku
   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ameshakubali jamani ila kwa jinsi yeye alivyotapeliwa bila kujali ni kizembe au laa ameleta kama angalizo kwa watu wengine maana leo yeye katapeliwa laptop kesho mtu mwingine atalizwa kitu kingine. Ni angalizo zuri sana.
   
 14. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Matapeli huwa hawatumii namba zilizosajiwa, kwa kuhofia kukamatwa kirahisi.
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,784
  Trophy Points: 280
  pole sana ila umejitakia ...bongo usimuamini mtu yoyote
   
 16. Chuck j

  Chuck j JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 1,986
  Likes Received: 416
  Trophy Points: 180
  m2mie mpesa,kiasi kiwe kikubwa zaidi ya ulichonacho kwenye acc yako ya mpesa,kuna sms itakuja kukujulisha huna salio la kutosha kwenda kwa ...utapata jina lake..after that waone wenye mtandao anaotumia watakusaidia kumpigia huyo mhalifu kwa ku2mia no yoyote aliyokuwa anawasiliana nayo.
   
 17. E

  Entare3 Member

  #17
  Oct 30, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzembe ulioje.Unastahili kuchapwa viboko.Huwezi kuacha laptop kwa mtu usiyemjua.Huu ni uzembe uliokithiri.Nikueleze kuwa inabidi utulie ukanunue laptop nyingine.Hata utume tigo pesa au mpesa haitakusaidia maana watu wana line zaidi ya moja.Hilo gari wamebandika namba za bajaj na yawezekana sio namba halali za TRA..zaweza kuwa zimetengenezwa mnazi mmoja.Unastahili kupigwa viboko
   
 18. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #18
  Oct 30, 2011
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mtani pole kwa kichapo
   
 19. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  pole sana mkubwa...
   
 20. D

  Derimto JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Pole mkuu ila nashangazwa na watu ambao humu ndani wanajidai wajanja hawajawahi tu kukutana size yao hawa jamaa hujipanga vizuri sana na wanakusoma zaidi ya vile ulivyojipanga. Ila kuwapata nadhani ni ndoto na story kwa jinsi polisi wetu walivyo na mfumo wa kipelelezi mbovu wanataka uwatafute mwenyewe halafu uwambie wako pale ndipo wakakamate then waanzie hapo upelelezi na kusimamia kwa mshtakiwa na kula hela pande zote mwisho unatumia gharama na muda na usifanikiwe.
   
Loading...