Leo tarehe 26.06.2014 nimepeleka maelezo yangu ofisi ya Uhamiaji Moshi kuhusu uraia wangu. Kwa maelezo niliyopewa awali kuna wanaosema mimi sio Mtanzania.
Kufuatia hiyo Mzee wangu, Gaspar Mwaria Msando na kaka yangu George Mwaria Msando wamehojiwa leo kama wananifahamu.
Miaka 34 baada ya kuzaliwa hospitali ya serikali, kusomeshwa shule msingi ya serikali, shule ya sekondari ya serikali na chuo kikuu cha serikali leo natakiwa kuelezea kama ni raia.
Najiuliza, kama sio raia narudisha gharama zote za serikali? Je naenda wapi kama leo hii mimi sio raia? Stateless person?