mkuu Earthmover ni kweli kabisa. Hawakutegemea kabisa hawa jamaa, dk slaa kawakata ngebe ktk safari yake hii ya kigoma
viva chadema
Muda mwingine kupitia misukosuko ndipo utaujua ufahamu wa mtu. Sikutegemea ZZK anaweza kutumia njia hii kutatua jaribu alilonalo. Anyway kama wapo waliomshauri kutumia vyombo vya habari katika utatuzi wa jambo dogo kama hili wana nia ya kumpoteza kisiasa. Vyombo vya habari havina urafiki na mtu ila kujipeleka ni kuwatengenezea biashara tu kwa headings nzito zenye utafiti kiduchu.
Mnyalu MsemakweliWakuu, nimetumiwa mwaliko huu wa uwepo wa mkutano na waandishi na wahariri kesho saa nne na nusu pale serena. ningependa nasi sote tuitikie wito huu kwa kuarifiana juu ya tukio hilo.
zaidi soma Taarifa za mwaliko
Mwaliko wa Mkutano na Waandishi wa habari: Ndugu Albert Msando
MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi).
Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu ya mashitaka 11 na majibu yake ambayo Mhe. Zitto Kabwe na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.
Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.
Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam
Albert Msando anatafuta umaarufu huyu, kuna kesi yangu alishindwa mpaka nikaishift kwa Advocate Materu
juzi nilikuwa nae ni kamuuliza akasema ni kazi na inapesa nzuri sana kutoka ccm..
Chadema Kanda ya Kaskazini Fuatilieni huyu Albert Msando.Anaonekana ni mamluki na Kibaraka wa CCM.
Siku zote anatukana viongozi wakuu wa CDm kupitia FB wall yake
Tutarajia matusi mengine kesho kwa chama na viongozi wake wakuu.
Uzuri jamii ishamjua ni mtu wa namna gani. Asubiri ubunge wa mahakama au wa viti maalum kama mama Rwakatare. Si wa kumuacha huyu ni kumfanya kama Malema wa ANC.
Ningewashauri hawa jamaa wakae kimya tu baada ya kupeleka utetezi wao Kamati kuu, wasubiri uamuzi!!!!!
Nasikia malipo ya huu ujinga wa kukashifu chama kesho analipwa na CCM.Njaa mbaya sana!
Zitto ashasahaulika .kwenye TZ politics gatz,aanzishe chama chake cha dini yake na kanda yake amchukue kafulila,habib,hamad rashid,kisandu na wasaliti wenzie.msando majibu si lazima kwenye media na hatuna interest nayo,tunasubiri maamuzi ya kamati a.k.a CC.u guys try to learn in politics being quite is also an answer.tushawachoka you too wabinafsi.
Mnyalu Msemakweli
===>Kweli nchi hii kuna ombwe la uongozi TeamZitto sisi hatutaki matamko ya kila siku,tunataka tuone nini kimefanyika kuhusu suala lenu,na ni vizuri tamko likatolewa na CDM Kurugenzi ya Habari,
===>Mnatukera na kutuchosha kwa kufanya mambo kama watoto,haya mambo ndio ambayo yamesababisha wew Zitto uchukiwe na wenzako,kwa nini huna uvumilivi na hupendi kufuata taratibu?
Tumia hekima huu uzi hauna mahusiano ya hoja zako. Kwa nini usizipeleke kwenye uzi husika.