Albert Msando, Mwanasheria wa Zitto, Kitila na Mwigamba Kuunguruma kesho Serena 4.30 asbh

Albert Msando anatafuta umaarufu huyu, kuna kesi yangu alishindwa mpaka nikaishift kwa Advocate Materu
 
Safi sana , ndugu Albert msando, kwa kuwa Tundu lissu alisema mashtaka yao yanatokana na Waraka, ni vyema Jamii ikafahamishwa wazi ni makosa gani hayo, na ni waraka gani( MAANA ULE WA MWANZO WALISEMA NI FEKI).SISI WALIPA KODI WA NCHI HII IAMBAYO INAVIPA VYAMA RUZUKU TUNATAKA HAKI ITENDEKE NDANI YA CHADEMA, NA SI HAKI KUTENDKA TU, TUNATAKA TUONE KUWA HAKI IMETENDEKA.
 
dogo atapoe vibaya sanaaaa, ataongea kama wakili lakini atatafisiliwa kama naye ni msariti na udiwani wake utakuwa na tabu sanaa, ushaur wajibu kamati kuu kwa maelezo sio wahandishi wa habar kwani aitasaidia kabisa ata walichoongoa kipindi kile kimeshapotea masikioni mwa watu.

Hivi wewe unafikiri, KAMATI KUU HAIJUI KWAMBA ZITTO ALIFANYIWA ZENGWE?
Halafu huoni pia ajabu, kamati kuu iwe mshitak halafu hiyo hiyo iwe hakimu?- INAHITAJIKA NGAZI NYINGINE YA CHAMA KUWEZA KUJADILI JAMBO HILI
 
..... kazi wanayo hawa ndugu.

wana tapa tapa sana lakini watanzania washawajua, wanajua kwamba hawa ni ndumila kuwili, wanafiki.

ukombozi wa nchi hii inahitani viongozi wenye maono, makini na wasio wabinafsi
 
Tumia hekima huu uzi hauna mahusiano ya hoja zako. Kwa nini usizipeleke kwenye uzi husika.

kuna mtu alianzisha hii kitu baada ya kubainika ni uzush mods wakaifuta naona ndo mana kaona apitie mgongo wa mwenzie sababu hata yeye anajua ni habari ya uongo.
 
Haaah!!! Hiv ukisimamishwa uongoz ndo unatafuta mwanasheria???? Na je waandishi wa habari ndo waliowasimamisha??? Yaan mfano ukataliwe na mwanamke we unatafuta wakili??? Hapa Kweli kuna kitu hawa majamaa kweli walitumwa kuiangamiza chadema,kwan chama cha siasa ni moja? usomi wao wa kuokota..mi nafikir ndo wanachochea hasira ya kufukuzwa kabisa.
 
Kama nia ya Zitto ni nzuri ndani ya chama, basi akajibu mashtaka yake na ufafanuzi wake ndani ya vikao vya chama na si kwa vyombo vya habari. Naomba kesho ndo iwe mwisho wake katika siasa za Chadema
 
Wakuu, nimetumiwa mwaliko huu wa uwepo wa mkutano na waandishi na wahariri kesho saa nne na nusu pale serena. ningependa nasi sote tuitikie wito huu kwa kuarifiana juu ya tukio hilo.

zaidi soma Taarifa za mwaliko

Mwaliko wa Mkutano na Waandishi wa habari: Ndugu Albert Msando

MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi).

Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu ya mashitaka 11 na majibu yake ambayo Mhe. Zitto Kabwe na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.

Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam

Hii press conference sina imani nayo kabisa. Unaweza kuta wale m@f@l@ wa Masalia Camp, a.k.a PM7 kina Mtela, Grayson, Mchange , Fyonza na wemgineo eti ndio waandaaji!!
 
Hawa watu walipewa mashtaka na waandishi wa Habari?

Mbona wanazidi kuonyesha ni watu wa hovyo kabisa?

Kwa ujinga huu inabidi Kamati Kuu ichukue maamuzi mara moja dhidi ya uhuni huu.
 
Muda mwingine kupitia misukosuko ndipo utaujua ufahamu wa mtu. Sikutegemea ZZK anaweza kutumia njia hii kutatua jaribu alilonalo. Anyway kama wapo waliomshauri kutumia vyombo vya habari katika utatuzi wa jambo dogo kama hili wana nia ya kumpoteza kisiasa. Vyombo vya habari havina urafiki na mtu ila kujipeleka ni kuwatengenezea biashara tu kwa headings nzito zenye utafiti kiduchu.
 
Wakuu, nimetumiwa mwaliko huu wa uwepo wa mkutano na waandishi na wahariri kesho saa nne na nusu pale serena. ningependa nasi sote tuitikie wito huu kwa kuarifiana juu ya tukio hilo.

zaidi soma Taarifa za mwaliko

Mwaliko wa Mkutano na Waandishi wa habari: Ndugu Albert Msando

MWANASHERIA wa Mhe Zitto Zuberi Kabwe (Mb), Dr. Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba, Ndugu Albert Msando, atazungumza na wahariri wa vyombo vya habari katika Hoteli ya Serena kuanzia saa nne na nusu asubuhi (saa 4.30 asubuhi).

Dhima ya mkutano huu itakuwa kutoa ufafafunuzi juu ya mashitaka 11 na majibu yake ambayo Mhe. Zitto Kabwe na washitakiwa wenzake walipewa na Kamati Kuu ya CHADEMA. Aidha, katika kikao hiki Ndugu Msando, kwa niaba ya wateja wake, ataeleza hatua ambazo wateja wake wanazichukua ndani ya chama katika kuhakikisha kwamba mgogoro uliopo unakwisha kwa amani na haraka iwezekanavyo bila kuleta athari zaidi kwa chama.

Tunatanguliza shukrani na tunaomba waalikwa wazingatie muda.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge Zitto Kabwe,
Jumanne, 10 Desemba 2013
Dar es Salaam

Chadema Kanda ya Kaskazini Fuatilieni huyu Albert Msando.Anaonekana ni mamluki na Kibaraka wa CCM.

Siku zote anatukana viongozi wakuu wa CDm kupitia FB wall yake
 
Back
Top Bottom