kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,305
- 12,600
Asichukuliwe poa kwani kitendo alichofanya ndugu Chalamila kina kila dalili zote kuwa sio cha bahati mbaya na hayuko peke yake.
Maongezi yake ukiyasikikiza vizuri yana kila dalili kuwa anawachochea watu wa kanda ile dhidi ya kifo cha mpendwa wetu. Bado haamini kuwa Mungu anaweza kufanya vile kwa mtu ambae ni Rais.
Chalamila anafahamu kuwa Tanzania ina kanda nyingi zikiwemo kanda za Mashariki, Kaskazini, Kati, Kuzini, Nyanda za juu Kusini, Magharibi na Kanda ya Ziwa. Alikuwa akifahamu kuwa kanda ya ziwa ilikuwa miongoni mwa kanda nchini ambazo zimerundikiwa kwa makusudi miradi mingi ya maendeleo ya matwilioni ya pesa kulinganisha na kanda nyingine nchini. Chalamila anataka kwenye miradi hiyo mama Samia asiondoe hata coma wala nukta kwenye ujenzi na utekelezwaji wake.
Chalamila inawezekana ana hasira iliyopitiliza juu ya awamu ya sita. Aliyoyasema hayakuwa kwa bahati mbaya, lazima ahojiwe zaidi ili kujua alimaanisha nini kusema pamoja na kwamba JPM amekufa lakini miradi ya kanda itatekelezwa kama ilivyo na mama Samia, huko ni kuwachonganisha wananchi wa kule na mama, maana hata JPM kuna miradi ya watangulizi wake aliifanyia tathmini ili kuona ipi aendelee nayo na ipi aicheleweshe na ipi aiache kabisa. Kwanini Chalamila anataka kuwaaminisha watu wake kuwa miradi na ahadi za JPM zitabaki palepale na vilevile kwa spidi ileile?