Alarm za magari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alarm za magari

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Mrembo, Sep 15, 2011.

 1. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  habari za jioni wanajanvi.
  jamani mimi ni mhanga wa huu wizi wa magari unaoendelea jijini. yani katika miezi mitatu nimeshabomolewa gari yangu mara mbili na kuibiwa power window, head rest, side mirrors etc.
  sasa mimi nimechoshwa na kuuziwa vifaa vyangu vilevile vilivyoibiwa tena kwa gharama kubwa.
  sasa basi... naomba kama kuna mtu anajua alarm nzuri za kufaa hapa mjini. maana nimeambiwa kuna alarm jamaa wanaweza kuzitegua, so hazisaidii kivile.
  na pi nitashukuru kama nitajulishwa zinapatikana wapi?

  asanteni na ninawatakia jioni njema.
   
 2. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #2
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  jamani watu mmeshalala?
  haya basi nawapeni homework mpaka kesho tena
  usingizi mwema
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2011
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280


  mrembo umesema upo mjini, mjini wapi?
   
 4. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  DSM Tanzania
   
 5. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ni PM umetumia alarm zipi hapo mwanzoni, na how much can you afford? they range beween 45,000-500,000Tshs.
  Lakini hiyo gari yako ni aina gani.
  Na je una park wapi mpaka wanafungua na kutegua alarm wewe bado hujasikia chochote.Kama ni nyumbani security ya gari yako can be much cheaper and guaranteed.
  Just PM me and let me know when you want it fixed.
  Lakini la ziada, wekea BIMA ya hivyo vitu, they end up paying you hata kama ni 3 month.
  Pole dada
   
 6. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkuu, lakini naona kusema kwamba umekuwa muhanga wa wizi kwenye gari yako mara tatu hiyo hiko on high side; kabla ya kukimbilia kwenye cutting age CAR ALARM fanya yafuatayo:
  • Inaelekea hauko makini unapo park gari yako, park mahali penye usalama hata ikibidi kutembea kwa mguu kuifuta gari yako kwenye parking lot yenye usalama fanya hivyo, na kama hakuna jinsi basi tafuta kijana au mtu ambaye ana shughulki ya kawaida karibu na ulipo park mwambie akulindei gari lako mpaka utakapo ludi muachie senti kidogo, this works like magic! I have been using this trick for years on end na sijawahi kupata matatizo yoyote.
  • Usiweke kwenye gari vitu vya kutamanisha kama vile simu, camera, laptop au brief case, vifungie kwenye boot inapobidi au uondoke navyo.
  • Alarm nyingi ni useless mtu mweledi anaweza kuzi-disable kirahisi tu, nilikuwa naona Ulaya wanafunzi wajanja wanatumia remote za ( siwezi kutaja hapa maanake wabogo wakali wanaweza kulidaka hilo na kuanza kuwaliza watu) hizo remote zinasoma code za alarm na kuzirecord baadae wanatumia code hizo kufungua hata kuiba gari lako - ni hatari sana. Naludia kusema kwamba mlinzi mkubwa wa gari yako ni wewe mwenyewe, kuwa makini mahali unapo park. Alarm ambayo inaweza kukusaidia kwa muda naludia "kukusaidia kwa muda" labda ujaribu kununua AUTO WATCH inayo tengenezwa Africa Kusini.
  Mimi ni mtaalamu wa mambo haya ya electronics kwa hiyo naelewa vizuri ninacho zungumza humu kuweni makini, siku za usoni ntajaribu kushauliana na wenzangu hili tuweze kuleta kwenye soko Alarm ambayo itakuwa vigumu kuinakili na ambayo inaweza kuwa affordable kwa kila MBONGO.
   
 7. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  nashukuruni sana kwa ushauri.
  swali: kuna mtu anataka kuniuzia alarm zinaitwa European anasema hizo wahuni bado hawajajua kuzitegua. je kuna mtu anazijua?
  @ bukyanagandi, mimi huwa muangalifu sana ninapopark gari mahali, ila mara ya mwisho vibaka waliruka ukuta hapa home wakaniibia, so nahitaji alarm ambayo mtu akigusa gari, inalia. kwa kifupi mi sijawahi kutumia alarm before, lakini kwa huu usumbufu naona niweke tu japakua insuarance huwa wananitengenezea, ila usumbufu na mda wangu mwingu napoteza.
   
 8. wende

  wende JF-Expert Member

  #8
  Sep 18, 2011
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Good advice,ni kweli nami naitumia hii aina ya kifaa! Ni nzuri sana,I dont regret the way it works perfectly. They are made by PFK Electronics (PTY) Ltd and Knightwatch (UK) Ltd.
   
 9. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #9
  Sep 23, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Oh splendid indeed kama huko muangalifu sana unapopark gari mahali. Kuhusu kuwadhibiti vibaka wanaoruka ukuta hapo home - dawa yao ni ndogo sana, fanya yafuatayo:
  • Nenda duka za mjini kakikati wanao uza vifaa vya umeme, kahulizie floodlight zenye sensor za infrared. Sensor za taa hizi huwa zinawaka tu wakati ziki-sense kwamba kuna binadamu anakaribia nyumba yako na zina huwezo wa kutambua binadamu akiwa mita kumi/ishirina kutoka nyumba/gereji yako.

  • Sasa unaweza kuiongezea huwezo wa ziada kwa kui-connect na ALARM ya bei nafuu tu hili inapo-sense binadamu siyo iwashe taa tu bali pia hi-raise ALARM; na kwa kuwa binadamu hawezi kuona mionzi ya infrared si rahisi vibaka kung'amua kwamba kwako kuna mtego. Cha muhimu hakikisha kwamba infrared sensor inacover zone area inayo pendelewa na vibaka. Mfumo huu huwa inawatisha vibaka sana maana huwa hawategemei kama taa zinaweza kuwashwa ghafla na kingora kulia kama ana ugonjwa wa moyo anaweza akazimia. Kuna mitego mingine lakini aha ngoja tuachane nayo ni hatari sana.

  Kuhusu ALARM ya gari mimi bado nakusistizia ufumbe macho ununue AUTO WATCH you won't regret, achana na hizi Mickey Mouse CRAP utakuja juta nazo ukizinunua. Goodluck.
   
 10. Mrembo

  Mrembo JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 392
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  @ bukyanagandi du, nakushukuru sana mkuu. Yaani iyo ya taa imenichekesha sana, i think i will go by that loh, infact that's what i need.

  Ubarikiwe
   
Loading...