My Power Windows Polisi wameshindwa kabisa kuzuia wizi wa kwenye magari?

Igwachnya

Member
Jan 5, 2011
80
20
Jana nilikuwa nimeegesha kagari kangu sehemu, Ndani ya muda usiopungua dk 15 gari yangu ilikuwa imebomolewa na kuibiwa kila kitu kilichokuwemo ndani yake ikiwepo power window zote pamoja na sight mirror moja ambayo tayari imechorwa namba.... Huu sio utamaduni mgeni hapa Dar. Hivi ni kweli kuwa Polisi wameshindwa kabisa kuzuia aina hii ya wizi? Leo nimeenda gerezani naambiwa nikachukue vitu vyangu kesho leo hawawezi kuuza vitu vya jana.... Wizi wenyewe umefanyika machana wa saa kumi jioni kweupeeee.... DSC08571.JPG DSC08564.JPG DSC08563.JPG DSC08561.JPG

UPDATES: KAtika kufuatilia fuatilia nimeambiwa na wezi kuwa naweza kupata vitu vyangu ila sharti niwe tayari kutoa 580000.... (Power window 4 na left wing mirror iliyoibiwa). Nipo nanegotiate nao kama wanaweza kunipunguzia. CAN U IMAGINE JINSI NINAVYONYANYASIKA? KOSA LANGU NI KUIBIWA......
DSC08622.JPG
Baada ya kujadiliana na wezi kwa muda... Nashukuru nimepata vitu vyangu, japo kwa gharama kubwa bila kuwahusisha hao polisi...... Kwa uzoefu wangu kila aliyemuhusisha polisi kwenye hili aliishia kupoteza vitu vyake moja kwa moja....
 
Pole mkuu, Polisi Tanzania wanasikitisha sana, miaka na miaka wauzaji wa vitu vya wizi wanafahamika mahali walipo na hakuna kinachoendelea, kila anayeibiwa huuziwa vitu vyake mahali palepale na POLISI Wapo mitaani kila siku, Na madefender, Pikipiki na miguu, Mpaka lini?
 
Duh pole sana mkuu .
Ahsante sana..... bt kuanzia jana nimeanza kutamani kuchoma moto wezi... Zamani nikiona watu wanapiga mwizi mi nilikuwa najaribu kusaidia ili wamwache from this time on, nitashiriki kupiga na kuchoma moto "I PROMISE"
 
Pole sana mdau, Naona hii kitu inakuwa kama mazoea sasa. Kwamba unaibwa halafu unaenda kununua vitu vyako na hauna la kuwafanya wezi. This is sad kwa nchi ambayo inasema kuna amani....................

Ni lini tutakuwa huru.?
 
Mbaya zaidi upate kosa na gari lako likalale kituoni siku mbili tu, ukienda kulichukua hutaamini macho yako, wanakwapua kila kitu kuanzia radio,power windows,sight mirror nk
Ukidai hayo majibu utakayo pewa hata shetani mwenyewe hapendi
This country bana
 
Kuna wakati badala ya kupiga wezi tutakuwa tunapiga Polisi.. Kwa sababu kazi yao ni kulinda usalama wa raia na mali zao na badala yake wao wamekuwa sehemu ya kuhatarisha usalama wa raia na mali zao
 
Duuh Pole sana Kaka... Dawa ni kutonunua vitu vilivyoibiwa ndio tutawakomesha.

Naweza kuamua kuto nunua, lakini nitazipata wapi nyingine kama hizi? Ki uhalisia power window sio bidhaa adimu na sio kitu amabacho mtu utahitaji kununua kila wakati bt hawa wezi wameongeza sana demand ya power window.
 
Nenda gerezani utaletewa hizo hizo zako pamoja site mirror
 
Pole mkuu,
Umeshapata ushahidi? Kama unao wapelekee maana hawawezi kufanya lolote mpaka wawe na ushahidi! Tumekwisha wabongo na jeshi la Mwema na Manumba....mpaka ushahidi ndiyo watafanya kazi, sijui ni kazi gani hiyo!

Kama wabongo mnadhani mna jeshi la polisi subiri upate shida ndipo utakapogundua hatuna polisi bali viosk vya watu kukusanyia fedha kwa ajili ya familia zao.

Na ukiripoti kwa wakubwa watakuletea maneno ya uongo na uzushi ambayo heri uende sokoni ya kule yana maana. Uswahihili swahili tu! Muangalie Kova na uswahili wake wa kujibu maswali kiovyo ovyo!
 
Ahsante sana mkulima wa kuku. Ushahidi gani sasa? Mimi ninaushahidi kwamba nimeibiwa... Huo ukweli wa nani ameiba hiyo ni kazi ya polisi.... Tatizo ni kwamba Wezi wamewazidi ujanja polisi kwa mbali na ikifika hapo ni bora ufuate masharti ya wezi wanaoweza kukusaidia kupata vitu vyako kuliko polisi watakaokufanya ukose vyote
 
Wiki tatu zilizopita, walipita kanisani wakati tunaendelea na ibada wakayapitia magari kadhaaa. Kwa sas usi-park gari lako mahali ambapo hakuna ulinzi.
 
Jana nilikuwa nimeegesha kagari kangu sehemu, Ndani ya muda usiopungua dk 15 gari yangu ilikuwa imebomolewa na kuibiwa kila kitu kilichokuwemo ndani yake ikiwepo power window zote pamoja na sight mirror moja ambayo tayari imechorwa namba.... Huu sio utamaduni mgeni hapa Dar. Hivi ni kweli kuwa Polisi wameshindwa kabisa kuzuia aina hii ya wizi? Leo nimeenda gerezani naambiwa nikachukue vitu vyangu kesho leo hawawezi kuuza vitu vya jana.... Wizi wenyewe umefanyika machana wa saa kumi jioni kweupeeee....View attachment 47716View attachment 47718View attachment 47719View attachment 47726

pole sana
 
Back
Top Bottom