Alama alizoacha afande Kirumira zitupe somo jadidi!

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
745
633
Amani ni tunda la haki. Haki inapokuwepo, basi amani hutamalaki. Afande Kirumira, Mohammad, kamanda wa zamani wa Wilaya ya Buyende amekufa kiume na ameacha alama zisizoweza kusahaulika kamwe!

Kabla ya kifo chake, afande Mohammed Kirumira alikuwa mtetezi wa haki za binadamu hasa kupata habari. Hiki ndicho alichokiamini, na amekufa akikisimamia.

Imekuwa ni nadra sana kwenye kumbukumbu zangu kuona wananchi wanaandamana kumlilia askari aliyewatoka, ukizingatia na 'brutality' wananchi wanayoipata kutoka kwa askari hawa. Sikumbuki mara ya mwisho nimeona lini, lakini nachoweza kusema ni kwamba, nimejionea jana wananchi wakilia na kusaga meno kuomboleza kifo cha Afande Kirumira, afande kipenzi cha Waganda. Wamelia kwa uchungu. Wamelaani kwa sauti zisizoweza kunyamazishwa.

Afande Kirumira alijiunga na jeshi la polisi la Uganda mwaka 2006. Alijiunga akiwa na shahada ya Ualimu. Imani yake juu ya haki haikuwa ya kawaida. Na ni imani yake hii ndiyo ilianza kumtia kwenye misukosuko toka mwaka 2014 ambapo alifukuzwa ndani ya jeshi la polisi na kuwa mwananchi wa kawaida, akijishughulisha na kuchomelea vyuma ili apate chochote kitu. Ndipo mwaka mmoja baadae alirejeshwa kazini na kupelekwa mafunzoni na kisha kufikia cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Polisi (Asistant Superintendent of Police) na kuwa kamanda wa polisi wilaya ya Buyende.

Katika hali isiyo ya kawaida, ni nadra sana kuona askari polisi, hasa Afrika, akiwa upande wa raia na kuwa mstari wa mbele kuwatetea. Tumezoea kuona mitama, vipigo vya mbwa koko, unyanyasaji wa askari dhidi ya raia. Hii imekuwa tofauti sana kwa Afande Kirumira. Yeye amekuwa upande wa wananchi. Hivi karibuni alitokea kwenye mahakama moja nchini humo na kukuta waandishi wa habari wakiwa wamezuiliwa kuingia kutimiza jukumu lao. Afande Kirumira akawakusanya wote na kupambana na askari wengine kadhaa ili waachie mlango kuwaruhusu waandishi waingie. 'Injustice should stop! Everything should be reported to the public' Alisikika akisema Afande Kirumira kwa hasira kali.

Inasadikika wauaji wa Kirumira walimkuta akiwa maeneo ya Kalenga Shopping Centre, akiwa ndani ya gari lake na mwanamke anayesadikika kuwa si mke wake. Hoja hii imeshikiwa mabango na serikali ya Uganda, na pengine wanataka kuitumia kuwa sababu ya mauaji yake kwamba Afande aliuawa na wagomvi wake juu ya wanawake. Hii nakataa, na ni nadharia ya kipumbavu ambayo vyombo vya ulinzi vinatakiwa kufikiria. Pengine nikubaliane na Dr. Kaliisa, rafikiye wa karibu, kuwa, kuna kina sababu ya kuamini kuwa afande Kirumira ameuawa kutokana na ukaribu wake na Hon. Robert Kyagulanyi Ssentamu, mbunge wa jimbo la Kadondo, maarufu kama Bobi Wine, ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani anakopatiwa matibabu baada ya 'corporal punishment' ya jeshi la polisi nchini humo. Nakubaliana kabisa na hoja hii. Na sina hata chembechembe ya wasiwasi kuwa, mauaji ya afande Kirumira ni mwendelezo wa upotezaji wa 'critics wa rais Museveni.

Hivi karibuni, wakili wa Bobi Wine, Mmarekani Robert Amsterdam, alisema kuwa, ipo haja kubwa ya serikali ya Marekani kusitisha msaada wa silaha kijeshi kwa serikali ya Uganda kwa sababu, silaha hizo zimekuwa zikitumika kuwaumiza Waganda-kinyume kabisa na malengo ya msaada huo.

Wakili Amsterdam anayo sababu ya msingi. Pamoja na hili, waganda kwa sasa wanatakiwa kuwa wamoja kukomesha ukiukwaji haki huu.

Somo kubwa pia kwa nchi za A. Mashariki, aliloliacha afande Kirumira ni kwamba, haijalishi una cheo gani, simamia haki. Namna wananchi wanavyoomboleza kifo cha afande Kirumira ni dhahiri kuwa, afande alikuwa mtu wa watu. Je, wapo polisi watu wa watu wangapi kwenye jamii zetu?

REST IN PEACE AFANDE KIRUMIRA!
 
sishabikii kuuwawa kwake ila maono yangu yanaonyesha kwamba haikuwa sahihi kuwalazimish jeshi wawaruhusu waandihi habari waingie kweny court ya kijeshi ili hali jeshi limekataa,nimeona clip moja inaonyesha hivyo tena mbaya zaidi akiwa ndani ya uniform,huo unaitwa uhasi/uhaini serkli y waganda ni ya wamoja polisi moj na jeshi,alipaswa kutumia njia nyingine ya kufikisha ujumbe na pia hata huko record zake sio nzuri zidi ya vyombo vya ulinzi na usalama RIP Afande
 
Ngoja nishuke kwenye BRT kwanza ndo nita-comment. Ila najiuliza Alama ipi aliyoiacha? kwenye video clips kadhaa zisizozidi dakika 14? Kulazimisha waandishi waingie mahakama ya kijeshi!
 
Wapigania haki katika hizi nchi zetu za kiafrica huwa wako kwenye risk kubwa mno. RIP kamanda.
 
Pumzika kwa Amani
images.jpg
 
Vyombo vya usalama vina nidhamu yake. Kukiuka nidhamu hiyo siyo jambo la sifa.
=====
R.I.P afande.
 
Back
Top Bottom