Alaa! Kumbe: Sasa nimeamini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Alaa! Kumbe: Sasa nimeamini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MZIMU, Sep 5, 2012.

 1. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Katika vitu ambavyo, sivielewi na vina nishangaza sana katika siasa za Tanzania, ni ushindi wa chama tawala katika chaguzi nyingi zinazo fanyika hapa nchini. Kwa sababu maongezi ya watu wengi wenye akili timamu, huonyesha wazi na kwa mifano kutokuridhika na chama hicho. Na pale watu wanapo ongea, hatokei hata mtu mmoja wa CCM kujitetea.

  Kampeni zao hutawaliwa na rusha roho na bongo fleva kwasababu bila vionjo hivyo, watu hawana taimu wala muda huo. Tofauti na mikutano ya vyama vingine ambavyo hujaza watu bila hata rusha roho au bongo fleva.

  Sasa baada ya uchaguzi, matokeo hua CCM kashinda kwa kishindo. Kitu kingine cha ajabu. Tunatarajia washindi wawe na furaha na washangilie. Tofauti na ushindi wa chama hicho, wanao shangilia mitaani ni kundi kubwa la watoto, mabinti wa kike na vijana dizaini flani hivi wa vitaa.

  Watu wengi hulalamika kua hawa jamaa wanaiba kura. Mpaka ikaja ile hadithi, unamchagua mpinzani lakini tick yako, inajiandika kwa CCM.

  Kwakeli mimi ilikua sipati jibu. Lakini sasa baada ya zoezi la SENSA kwisha, na kutangazwa kua limefanikiwa kwa 95%, lakini ikalazimika kuongeza muda kwa 100%, jambo ambalo limesababisha mauji ya ndugu Daudi Mwangosi. Na constant press release, kwamba zoezi limefanikiwa, ukweli ukiwa idadi kubwa ya waislamu nchi nzima waligomea na wanaendelea kugomea zoezi hilo.

  Inanisikitisha kuona kua, serekali imeshindwa kuwashawishi raia wake katika jambo muhimu kama hili, matokeo yake wanaamua kutumia vyombo vya habari kufanya propaganda dhidi ya raia wake wenyewe kua zoezi limefanikiwa.

  Ninavyojua mimi propanganda hutumika kumzuga adui. Kwa hiyo kwa propaganda hizi, serekali hii imekua na uadui na raia wake wenyewe. Hivyo inalazimika kufanya propaganda kuficha kushindwa kwao.

  Kwa mtaji huu sasa nimamini kua ushindi wa CCM, Tanzania bara(Tanganyika), na Visiwani (Zanzibar), kweli ni wamagumashi.
   
 2. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  It's too late to realized this wenzio tulishasoma alama za nyakati long time ago....
   
 3. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  JIULIZE KWANZA, " too late" ni slogan ya Wakata tamaa and failures. Nili lilijua hili muda mrefu. Lakini as a rational person, nililazimika kubakisha kile wanasheria wanakiita, benefit of the doubts. Lakini sasa nimeamini BEYOND REASONABLE DOUBTS.
   
 4. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  umenifurahisha kaka.kama zoezi lilifanikiwa kwa 95% walitakiwa kuongeza muda kwa 5% ili kukamilisha 100% sasa kuongeza 100% ya muda maana yake wanataka livuke lengo kwa 95% hiyo ina maana kuwa tutamaliza watanzania wote na ikibidi na kenya tuende.

  hii ndiyo tanzania inaunda tume inaongozwa na jaji lakini baada ya majibu upelelezi unaanza na kama kuna hatia kesi inapelekwa kwa hakimu.

  chezea tz weye?
   
 5. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  shangaa wewe ndugu yangu ringo edmund, na hao ni wataalamu wa statistics.
   
 6. Domy

  Domy JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2012
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 4,702
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ulikuwa hujui mpaka leo?.ndo maana wenzio tuko kwenye mapambano ya kukomboa nchi.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kuwa member wa ccm kwa kipindi hiki unatakiwa uwe unapiga dozi ya bangi kila siku kama arv na siku ukiacha kuvuta ujue ndio mwisho wake kukaa ccm.
   
 8. TOFU

  TOFU JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2012
  Joined: Aug 26, 2012
  Messages: 532
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Pole kwako mgeni wa mambo...!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Tungaraza Jr

  Tungaraza Jr Senior Member

  #9
  Sep 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  95% wamehesabiwa 100% extra days to pay makarani wa sensa, Kama mwajua 95% counted kwa nin hao waliokataa kuhesabiwa mkafanya approximations ni kaya ngapi na kwa familia ya kawaida ni watu 6 (Baba, Mama na watoto wa4).

  Mi nadhani kila karani angekuja na idadi ya kaya zilizogoma na kwa makadilio ya watu 6 kwa familia zoezi limekwisha katika muda husika.

  "IT IS ALLOWANCE TIME"-Recurrent expenditure 70% of the 2012/13 budget.
   
 10. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuwa memba, mpenzi au hata kiongozi wa CCM lazima uwe na akili zinazofanana na akili za maiti
   
 11. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #11
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata hivyo umechelewa sana kujua kwa maana katika hali ya kawaida huwezi kushindania kitu ikiwa jopo zima la waamuzi na makamisaa unapanga wewe.katika silika ya ubinaadamu hayupo wa kutoa fair play hapo.ni dhahiri kwa namna moja au ingine dhuluma hutendeka hapo.kwa kumbu kumbu kidogo si unamkumbuka mtu mmoja anaitwa kivuitu lakini hata hivyo hakuhusishwa na vurugu zilizotokea kenya.
   
 12. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #12
  Sep 5, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  cha kufurahisha kwangu ni kwa sababu mtoto wangu wa mwisho ana miaka miwili na hamna hata mtu mmoja anayehusika na ccm kwa namna yeyote ile anamzidi akili.
   
 13. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #13
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kivuitu si alikua Jaji Makame wa Kenya. Hivi yaliishaje? Yeye hakuitwa the hague. Maana wameitwa kule wengine tu.
   
 14. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #14
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Kwaukweli hasa CCM imebaki na wazee, tena wale wasio soma, zumbukuku mambo yako huku, au awe nikiongozi kwa kua wanapata chochote, vinginevyo, ukiona kijana basi yupo kwenye menu.

   
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hata hao vijana waliopo wanajitafutia laana tu na mwisho usio mwema,ila wataweweseka sana mwaka huu na mingine ijayo maana kila wakijaribu wanafeli na kuzidi kujidhalilisha.
   
 16. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #16
  Sep 6, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni kama kumtafuta aliyesababisha mauaji rwanda wakati kagame yupo.
   
 17. h

  hacena JF-Expert Member

  #17
  Sep 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 619
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Is it a Criminal Case?
   
 18. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #18
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Umenifanya cku yangu ikae poa uchunguzi akafanye jaji hukumu akatoe hakimu wa mahakama za mwanzo patamu hapo.
   
 19. babalao 2

  babalao 2 JF-Expert Member

  #19
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,218
  Likes Received: 1,270
  Trophy Points: 280
  Watu tumeona makamanda wa polisi wanatangaza matokeo ya uchaguzi badala ya wasimamizi wa uchaguzi. UKIJIJUA WEWE NI NANI KATIKA NCHI YAKO UTAKUA HURU KABISA.
   
 20. MZIMU

  MZIMU JF-Expert Member

  #20
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 4,080
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  babalao the second, hili lako nalo pia neno.
   
Loading...