Al Shabab tenaaa!

Nilipata kusikia kuwa hawa jamaa ndio wenye majumba na miradi mingi pale Nairobi kutokana na pesa wanazopata kwenye mambo yao ya uharamia na mipango mingi walikuwa wanaifanyia Nairobi,kwa serikali ya Kenya kutangaza vita wakati hawa jamaa wapo mjini na wana kila kitu ni hatari kwa usalama wa eneo husika ndio maana wanaweza kuonesha uwezo wao ndani ya jiji
wako bahari beach na maeneo mengi Porsche mjini
 
Nilipata kusikia kuwa hawa jamaa ndio wenye majumba na miradi mingi pale Nairobi kutokana na pesa wanazopata kwenye mambo yao ya uharamia na mipango mingi walikuwa wanaifanyia Nairobi,kwa serikali ya Kenya kutangaza vita wakati hawa jamaa wapo mjini na wana kila kitu ni hatari kwa usalama wa eneo husika ndio maana wanaweza kuonesha uwezo wao ndani ya jiji

We mpuuzi unacoment nn? Unajifanyaga wajua sanaaaa? Una uhakika gani kama hii habari ni ya ukweli?
 
Ni upuuzi kuamini kwamba eti Kenya wanashambuliwa kwa vile wameingiza majeshi Somalia. Ukweli ni kwamba hayo yalikuwa yatokee hata kama Kenya wasingechukua hatua hiyo. Suluhisho la ushenzi huu ni kwa nchi zote za Afrika Mashariki kuihamishia vita kulekule Somali, kuwasaka (Haswa viongozi wa kikundi cha kishetani hicho na kuwaangamiza. Ethiopia walifanya hivyo kwa kikundi kingine kilichokuwa kinatawala huko ( Si El Shabaab) na sasa El Shabaab wanawaogopa kama ukoma.
Kwangu, haiingii akilini kufikiria eti nchi huru kama Kenya itanyamazia mananyaso ya maharamia waliokuwa wakifanya uhalifu ndani ya nchi yao bila kuchukua hatua yoyote hata kama wangekuwa wanyonge kiasi gani!
Ushauri wangu kwa Kenya ni:
i. Wasiifanye kazi hii nusunusu bali waingie kwa nguvu kamili na kuwazima kabisa. Hilo linawezekana maana Uwezo wanao, nia wanayo na sababu ya kuwaangamiza ipo. Kwa kuanzia tu majeshi yao ya majini yadhibiti kabisa bahari ambayo ndiyo chanzo chao cha mapato. Ihakikishe hata wavuvi hawatii mguu kwenye eneo lao la kujidai na watakaokuwa na kiburi mambo yaishie hukohuko baharini na si kujipendekeza kwa kuwafikisha Mahakamani kama ilivyofanyika hapa.
ii. Idara ya ujasusi ya Kenya ikamate mali walizowekeza washenzi hawa kama majumba, mabenki na mifumo yote ya kuhamisha fedha
iii. Kenya ianzishe Mahakama ya kijeshi itakayowahukumu wahuni hao haraka na kwa usahihi (Kama ilivyofanyika Uganda).
iii. Kwa vile nchi iko katika hali ya kivita wabunge watunge sheria za kuwabana wanaowaonea huruma au wanaoshirikiana nao, kwa mfano yeyote atakayekamatwa na kuthibitishwa kushirikiana na washenzi hao mali zake zikamatwe, afilisiwe na afungwe maisha au ahukumiwe kifo.
iv. Njia kuu za kupitisha silaha za hawa washenzi wanaojificha nyuma ya pazia la uislamu (Na kwa njia hii kuunajisi) ni baharini na mpaka wa nchi hiyo na Eritrea. Yeyote anayetaka kushinda vita hiyo ni lazima ahakikishe anadhibiti njia hizo vilivyo.
v. Uchunguzi wa kubaini mali na amali za wahuni hawa ufanywe Afrika Mashariki pote. Si kazi ngumu sana kuzibaini maana ziko waziwazi Mombasa, Nairobi, Arusha, Dar Es Salaam na hata Mwanza.
Mwisho watanzania wasijidanganye kwamba mashambulizi ya mabaradhuli hawa yataishia Kenya, Uganda na Burundi tu bali hata wao wanalengwa na wanaweza kushambuliwa kama wenzao. Huu ni wakati mujarab wa kuamka, kuunganisha nguvu na kuufuta uvundo huu unaoliaibisha bara letu na haswa Afrika Mashariki.
 
Safari hii lile kundi la Al Shabab limelipua bomu kwenye basi na watu 8 wamepoteza maisha mpaka sasa

Attack near Kenya-Somalia border 'kills four'

Kenyan police secure the scene of an explosion in the Kenyan capital Nairobi 24 October 2011 Police in the capital are on a heightened state of alert
Armed men have attacked a lorry near Kenya's border with Somalia, killing at least four people, reports say.

The lorry was carrying school examination papers when it was attacked in Mandera district, reports say.

Kenya blames Somalia's militant Islamist group al-Shabab for a spate of abductions on its territory.

Al-Shabab denies the allegation and has vowed to take revenge against Kenya for sending troops into Somalia.

Kenyan Red Cross spokeswoman Nelly Muluka-Oluoch told the AP news agency that Red Cross staff who went to the site of the attack reported four deaths.

The attackers fired machine guns and rocket propelled grenades at the vehicle, which was carrying school examination papers, AP says.
Grenade blasts

Kenyan police spokesman Eric Kiraithe described it as a "banditry attack" about 110 km (70 miles) from Mandera town, the Reuters news agency reports.

He said government officials were among the passengers.

Kenya sent hundreds of troops into Somalia on 16 October to attack al-Shabab, which is linked to al-Qaeda.

Al-Shabab has repeatedly threatened retaliatory attacks on Kenya.

On Wednesday, a Kenyan man arrested after two grenade blasts in the capital, Nairobi, admitted in court to being a member of the group.

Elgiva Bwire Oliacha pleaded guilty to carrying out the attacks on a nightclub and bus stop.

One person was killed and 29 others were wounded in the attacks on 24 October.

Security has been stepped up in Nairobi since the blasts, with many residents fearing there could be more attacks, correspondents say.

Last week, the French authorities said a Frenchwoman suffering from cancer who was kidnapped from Kenya by Somali gunmen earlier in the month had died.

Other foreigners abducted from Kenya and being held in Somalia include a British woman abducted from a coastal resort, and a Kenyan driver and two Spanish aid workers seized from the Dadaab refugee camp near the Kenya-Somalia border.

BBC News - Attack near Kenya-Somalia border 'kills four'

Mbona wanasema watu wanne tu?!
 
sioni tofauti kati ya ghadafi na hao alshabab, prof saitoti songa mbele chakaza hadi mogadishu, kisimayu na lamu hatutaki ujinga wa wasomali hapa
 
Well done al shabab.! Kill, kill, kill and kill these rubbish kenyans..!!

Some people are sick...yaani unashangilia kama ugomvi wa majogoo wakati binadamu wenzako wanapoteza maisha 'innocently'!
 
Al shabaab teyari wanaonekana wana mtandao kenya.. Mistake kubwa sana kenya wameifanya kuwavamia.. Wale jamaa mabomu na kujitoa mhanga ni sehemu ya maisha yao.
 
Waache ya wakute na kiherehere chao! wanatumikishwa ujinga America. Maisha ya wazingu ni bora kuliko ya wananchi wao. miaafrica bwana
 
na subiri huo muda maana hawa jamaa walikuwa huko kwao somali wanashambuliana lakini hawa wakenya kwanini wametangaza vita na hao jamaa na kitu chengine hivi ukilinda mipaka yako na bila kuingilia watu wengine unapungukiwa nini mpka sasa sitakaa niamini vita ya kenya na al shabab imesababishwa na al shabab lazima kutakuwa na mkono wa magharibi hapa.
mbona hao walikuwepo kwenye vita tokea zamani lakini kenya walikuwa kimya kilichotuma kukubali vita nini.

nadhani utakua unafaidika na pesa za al shabab
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom