Al Masry vs Simba Sc kuonyeshwa na Tv hizi

tunawatakia Simba SC kila raheli ili wabugizwe 5 bila, na kipondo juu!
 
Jana nimeota simba kampiga mtu3-0

Bado sijaelewa maana ya hii ndoto
Kuna wakati ndoto huwa kinyume! Kule jamaa hawatashika so nina uhakika hatutapewa penati! Naamini hii itakuwa mara ya mwisho kwa timu yetu kupanda ndege! Mana huku bongo mwenyewe anataka nafasi yake! Ha ha ha simba nguvu ndogo!
 
Habar za jioni wadau wa sports,

Mechi ya marudiano kati ya Simba Sc na Al Masri utakaochezwa Jumamosi tarehe 17/3/2018 saa 2.30 usiku saa za afrika mashariki utarushwa live na channel moja ya misri iitwayo DMC Sports.

Nimeona niwajuze channel hii kutokana na malalamiko mengi niliyoyaona kutoka kwa mashabiki wa Simba Sc ambao mpaka leo AZAM TV hawajasema kama watarusha mechi hii na siku zimebaki chache.

Channeli hii inapatikana bure kabisa kwa dish la futi 8 unachotakiwa kufanya ni kutafuta fundi akusetie dish lako kwenye muelekeo sahii wa kupata Nilesat 7 degrees West kisha ajaze frequency basi.

Ni hayo tu wadau..
Haka kauzi katashobokewa sana na wale wake zetu wa pale Jangwani...

Subiri uone...
 
Back
Top Bottom