AL Baradei Kumrithi Mubarak Misri? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

AL Baradei Kumrithi Mubarak Misri?

Discussion in 'International Forum' started by Junius, Oct 7, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kundi la wanaharakati vijana nchini Misri wamemtaka mkuu wa Shirika la Kimataifa la nguvu za Atomiki, Mohamed Al- Baradei kugombea urais katika nchi aliyozaliwa ya Misri.
  Vijana hao kutoka chama cha upinzani cha Wafd, wamesema wameanza kampeni kumuunga mkono Bwa Al Baradei, anayetazamiwa kung'atuka katika nafasi yake ya sasa baadae mwakani.
  Rais Mubarak ambaye sasa ana umri wa miaka 80, ameitawala nchi hiyo kwa miaka 28 na bado hajatamka iwapo atagombea tena urais mwaka 2011.
  Kuna mjadala mkubwa unaoendelea nchini Misri wa mtu gani atakayechukua nafasi ya Mubarak, huku kukiwa na uvumi mwanawe mdogo, Gamal anaandaliwa kuchukua nafasi yake.

  BBC KISWAHILI.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  vijana na mabadiliko,mnasemaje vijana wa Tz, kuna watu wenu wametumikia anga za kimataifa kwa ufanisi mkubwa, akina Prof. Tibaijuka,Amina S Ali n.k, kama hawa si wanaweza kukabidhiwa dhamana fulani fulani hivi huko nyumbani, au vp?
   
 3. Mwawado

  Mwawado JF-Expert Member

  #3
  Oct 9, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 998
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 35
  Mkuu Junius pamoja na nafasi inayoonekana kwa Dr Mohamed Al-Baradei,Lakini Ukweli wa mambo ni kwamba Mtoto wa pili wa Rais Hosni Mubarak,Ndiye ana nafasi kubwa,na karibuni Taasisi zote za Uarabuni na Ulaya zinazojihusisha na mambo ya siasa zinampa nafasi .Mtoto huyo Gamal Mubarak ana umri wa miaka 47 na anafanya kazi kama investment Banker huko London (UK) na nyumbani Misri ana wadhifa wa Katibu Mkuu Msaidizi wa chama kinachotawala Nchini Misri kijulikanacho kama National Democratic Party (NDP).

  Nafasi ya Gamal ilionekana wazi baada ya baba yake kumchagua Dr.Ahmed Nazif,kuwa Waziri Mkuu Julai/2004,Dr Nazif alishawahi kuzungumza katika hadhara (American University in Cairo) kuwa "Gamal ana nafasi kubwa kuja kuwa Rais wa Misri".Dr Nazif ni Rafiki Mkubwa wa watoto wa Rais Mubarak (Alaa na Gamal)

  Gamala anakubalika pia na Mataifa ya Magharibi yakiongozwa na Marekani,amekwishawahi kufanya ziara Nchini Marekani mwaka 2003 na 2006,katika Ziara hizo alikutana na Viongozi wakuu wa serikali ya Marekani akiwamo Dick Cheney,Collin Powell,Condolezza Rice na Donald Rumsfeld.Ukimuacha Gamal watu wengine wanaozungumziwa Nchini Misri kwamba wana nafasi ya kuongoza Nchi hiyo ni waziri wa Ulinzi na Mkuu wa Usalama wa Taifa Nchini humo,lakini wote wawili wana umri mkubwa,wapo katika umri wa miaka 70+

  Rais Hosni Mubarak mwenye umri wa miaka 81 bado hajasema kama hatogombea tena katika uchaguzi utakaofanyika 2011.lakini watu wengi wanasema Rais Mubarak ameonyesha nia ya kustaafu.Mubarak amekuwa Rais wa Misri toka mwaka 1981 baada ya kifo cha Rais Anwar Sadat.
   
 4. Mwazange

  Mwazange JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2009
  Joined: Nov 16, 2007
  Messages: 1,051
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Inawezekana sana mkuu, na ni muhimu kuwaweka karibu our International figures kwenye mambo yetu ya ndani ya nchi katika kusonga mbele kiufanisi....lakini tutawafanyaje akina Lowassa nao, ambao bado wapo kilingeni??
   
Loading...