Akutwa amekufa kanisani kwa Gwajima

Akutwa amekufa kanisani kwa Gwajima

Jana usiku kuna mshirika wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ubungo, alianguka na kupoteza Maisha wakati akifanyiwa Maombi!

Cha kushangaza waumini na wachungaji wa kanisa hilo waliamua kuitekeleza Maiti Mpaka walipopatikana ndugu wa Marehemu na kuuchukua Mwili wa Marehemu,

Majira ya jioni ndugu wa Marehemu alienda kuomba utaratibu wa kanisa, wachungaji walikuwa wanarushiana mpira na kisha kuamua kusema Marehemu alianguka barabarani na wao wakamuokota kama wasamaria Wema tuu.

Mungu Si athumani Marehemu alikuwa muaminifu kwenye zaka(fungu la kumi) na amehifadhi risiti zake zote alizotoa zaka kuanzia Mwaka 2014 hadi July 2017.

Naomba hii iwe changamoto kwa Askofu Gwajima na wasaidizi wake jinsi ya kuthamini waumini wake wa hali ya chini na kuwajali,

Baadhi ya risiti za Marehemu naziambatisha hapa.
24c791dc369fa7030fda121ad295e27c.jpg
d0d836a151be0e4a31766b4760674770.jpg
edfbdf04b3eabc6af96878ceb70dc8eb.jpg
Mmh kichwa cha habari kina walakini mkubwa
 
Usijekuwa umetumwa, yatakutokea puani yule huwa hajaribiwi ujue, nasubiri tu wafuasi wake
 
Aaaaa poleni sana wafiwa ,bwana ni mkuu ,hata hivyo hakuna awezaye kuia kifo ,mimi ,nitakufa na Gwajima atakufa na sote tutarejea kwa Bwana Mungu aliye mkuu na daima
 
Kafara hyo, hapo Mzee g anazidi kuwa maarufu
 
Ujinga wake ndio umemuua, pesa zake badala ya kwenda hospitali anampelekea Gwajima mwenzao anahonga mademu na kununulia madege ughaibuni
 
Ama kweli mganga hajigangi.......anafufua misukule,ameshindwa vipi kumfufua muumini wake?
Umeelewa ulichoandika? Mganga hajigangi unaielewa tafsiri yake? Au bora kuandika tu?
 
Kila mtu kwa wakati wake ataujua ukweli atakapoyaacha maisha Ya hapa duniani hawa washenzi hela yako wanachukua na kukudanganya juu unanunua uongo
 
Mtoa mada amesema huyo ndg aliyepoteza maisha ALIANGUKA NA KUFARIKI WAKATI AKIOMBEWA. Hajasema alikuwa mgonjwa, mbona hizi ni cases za kawaida sana Wangempelekaje au angeendaje hospitalini wakati alikuwa haumwi.Tatizo JF kwasasa ina watu wa ajabu sana maana hawasomi na wakisoma hawatafakari kabla ya kutoa maoni.
 
Receipt makanisani? Sasa iyo si Biashara kabisa. Tra wachukue chao
 
Back
Top Bottom