Akutukanae, hakuchagulii tusi

Akutukanae, hakuchagulii tusi

Ukweli mchungu kati ya mambo ya hovyo aliyotuachia Mwl Nyerere kubwa kuliko yote ni huu muungano feki.
Nyerere katuachia vitu vitatu vya hovyo sana

I) Muungano wa hovyo
II) Katiba ya mwaka 1977 ya hovyo
III) Ujamaa na Kujitegemea.. ambapo hakujipanga na kuangamiza uchumi wa nchi
 
Muungano unazo kasoro zake, kuzipuuza ni makosa. Tangu kuasisiwa kwake utaona shabaha ya waasisi (hususani Mwalimu Nyerere) ilikuwa ni kuelekea serikali moja.

Somewhere along the way CCM wanepoteza uelekeo, wamepuuza malengo halisi ya Muungano ya kuwa na taifa moja na serikali moja.

Mwisho wa siku Serikali ya Zanzibar akaanza kujichukulia mamalaka yalikuwa ya Muungano na kuanza kuleta matatizo lukuki.

Mambo haya tasipofanyiwa kazi kwa dhati, basi muungano wetu ni mbio za sakafuni, utafikia ukingoni.
 
Rudi kwenye uelewa, wakati unaundwa huo muungano, tuliungana kwenye mambo 17 tu, baadaye yameongezeka mpaka 21 tu. Hivyo kwenye mambo au wizara ambazo siyo za muungano, kila upande ushughulike wenyewe. Kuwaweka Wazanzibari kwenye mambo yasiyo ya muungano, ni ujuha ambao hakuna mwenye akili timamu anaweza kukubali. Tanganyika haina uhaba wa watu mpaka ikahitaji mzanzibari kwenye mambo yasiyo ya muungano. Hao wazanzibari kwenye mambo gasiyo ya muungano, ndio wanaosimamia uporwaji wa rasilimali za Tanganyika kwa faida ya wazanzibari. Kama wanataka waingie kila eneo la Tanganyika, wakubali muungano wa Serikali moja. Hapo hakutakuwa na mipaka ya rasilimali wala uongozi au ajira kwa ujumla.
Kama unajua maana ya Muungano wa nchi Moja (Unitary State) sidhani ungeuliza swali hili.
Pili, Hata huko nje nchi magharibi Mambo ya Muungano huongezeka kutegemeana na lengo la Sheria.
Isitoshe, Mambo yasiyokuwa ya Muungano haina maana hayawahusu upande wa pili bali Sheria, kanuni na Usimamizi wake hufanywa na upande husika, bado ni jambo lenu wote.

Mfano, kulingana na Sheria yao huduma za Afya ni BURE! Huku Bara tulitakiwa nasi tumetunga Sheria yetu ilokubalika na Bungeni huduma ya ya AFYA kwa wote itakuwa ya BIMA kwa wote. Ni maamuzi yetu na tutasimamia maamuzi hayo kwa utunzi wa Sheria, kanuni na taratibu zake.

Kwa hiyo ni Sheria mbili tofauti zimetungwa kulingana na Serikali mbili za Janhuri. Kama Afya ingrkuwa Swala la Muungano basi hata Zanzibar wangelazimika kuwa na Bima za Afya au Bara inhrkuwa pia Afya Bure.

Ukienda Zanzibar kupata tiba utalazimika kufuata Sheria, kanuni na taratibu za kule, na Mzanzibar akija Bara anafuata sheria za huku. Kwa hiyo, malalamiko yako nyangekuwa kwa nini Afya sii jamno la Muungano badala ya kulalamika mambo ya Muungano kuongezeka!
 
Muungano unazo kasoro zake, kuzipuuza ni makosa. Tangu kuasisiwa kwake utaona shabaha ya waasisi (hususani Mwalimu Nyerere) ilikuwa ni kuelekea serikali moja.

Somewhere along the way CCM wanepoteza uelekeo, wamepuuza malengo halisi ya Muungano ya kuwa na taifa moja na serikali moja.

Mwisho wa siku Serikali ya Zanzibar akaanza kujichukulia mamalaka yalikuwa ya Muungano na kuanza kuleta matatizo lukuki.

Mambo haya tasipofanyiwa kazi kwa dhati, basi muungano wetu ni mbio za sakafuni, utafikia ukingoni.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia kubwa. Na sii kwamba Serikali ya CCM ilianza kulegalega bali tumekuwa na Viongozi wasiokuwa na Uzalendo pande zote. Iwe CCM, Upinzani na pande zote mbili za Jamhuri.

Baada ya bunge la Katiba ndio nilijua kumbe Kuna watu wana shaka na Uhalali wa Muungano wetu? Walipohoji hati sijui nini. Sasa kama wewe umezaliwa baada ya 1964, halafu unahoji Uhalali wa ndoa ya wazazi wako? Inakuweka wewe wapi kama sii MTOTO wa HARAMU?

Aaah wanasema Mtoto sii Haramu, haramu ni kitanda! Ok kama sio Haramu kwa nini watoto wa nje ya ndoa halali, hawaruhusiwi kurithi mali za wazazi wao? Hapa ndipo tulipofikia.

Hivyo basi Hawa wooote wanaopiga kelele kuhusu Uhalali wa Muungano, wajitambue kwamba wao ni Watoto wa Haramu hawatakiwi hata kuzungumzia ndoa hii wala mali za Tanzania.

Maasalaam
 
Screenshot_20260614_110646_Gallery.jpg
 
Muda wa kubembelezana au kuunufaisha zaidi upande mmoja kwa kutegemea jasho la watu wa upande wa pili, umekwisha. Ninashauri huo muungano wenu uvunjike mara moja ili kila nchi ijitegemee kivyake.
 
Sasa wee sijui Mkurya utakiweza kiswahili cha pwani?
Unaandika bila kufanya uhakiki (proof reading) matokea yake umeacha maelezo marefu yenye makosa ya kiuandishi. Na hili ni tatizo lako la muda mrefu kuandika na kupost bila kuhakiki unachopost. Unapoandika Uzi mama jitahidi kuusoma kabla ya kupost. Kwenye mjadala wa uzi wako wangalau unaweza kuwa na spelling error na sio Uzi mama.
 
Madai ya mwanzo kabisa ilikuwa kutaka muundo wa Muungano wetu uwe wa Shirikisho (Federal Union) Serikali 3, badala ya huu uliopo wa NCHI moja (Unitary State) Serikali2 na walijenga hoja zao kwa kufuata mfumo wa Shirikisho iilihali huo sio mfumo wetu. Inawezekana hawakujua kwamba Muungano wetu wa mwaka 1964 haukuwa wa Shirikisho kama walivyo aminishwa.
Mkuu Mkandara , kwanza niendelee kukushukuru kwa rejeo lako humu jf, japo kwa sasa jf imekuwa sana, lakini idadi ya watu sensible ukilinganisha na ile jf ya zamani, watu sensible wamepungua sana, na kwa vile mwaka huu wa 2026, kwanza nimependekeza nyie wana jf wote waanzilishi wa ile jf ya 2006, mtambuliwe as jf pioneers, mpewe a token of appreciation, michango yenu ina thamani kubwa sana kwa taifa letu hili, asante Mwaka 2026 JF Inatimiza Miaka 20! Tuwakumbuke Wana JF wa Zamani, Tuwaenzi, Tuwarudishe, na Wale ma GT wa Enzi Zile Waurejeshe Moto Kama Ule au ..?

Pili tangu kuasisiwa kwa huu muungano wetu adhimu na adimu, hakuna any public information program kuwaelimisha Watanzania kuhusu huu muungano wetu, hivyo wengi hawaujui, na hoja nyingi tuu za kupinga muungano zinatokana na ignorance!. Dawa ni serikali ikubali kugharimia public education and information program kuwaelimisha Watanzania kuhusu muungano wetu, Watanzania watauelewa. Mfano Watanzania bara wengi wanakereketwa na Wazanzibari kumiliki ardhi Bara, lakini wabara hatuwezi kumiliki ardhi Zanzibar, au ajira za Wazanzibari kwenye serikali ya JMT wakati hakuna mbara kuajiriwa SMZ!, hivyo kwa vile kuna vitu ni special na exclusive kwa Wazanzibari, wao nao wanataka Wabara pia na vitu exclusive na kuwaona Wazanzibari kama ni wageni. Hawajui kuwa baada baada ya muungano, wazanzibari wana haki sawa sawa na Mtanzania mwingine yeyote, zile haki zao za Zanzibar ni over and above!.
Tena baadhi viongozi wanasema wazi wazi kuwa Muungano ule Baraza la Malinduzi walilazimishwa kuukubali lakini haukupata ridhaa yao. Sijui hawa pia walikuwa katika Baraza lile Mpinduzi la kwanza lenhe wajumbe 29 ama nao walihadithiwa.
Hoja hii ni hoja ya kweli kabisa, muungano uliridhiwa na upande mmoja tuu wa muungano, Tanganyika, BLM liliarifiwa tuu na Karume kwa kuwaita mabalozi na kuwaarifu tumeungana na tumeridhia.

Hati za muungano zilizosainiwa tarehe 22 April pale Zanzibar na Nyerere na Karume, zilitaka ziridhiwe na mabunge ya nchi zote mbili, BLM liridhie Hati zile za Muungano ambazo ni international treaty kwa Zanzibar kufanya ratification na BLM litunge sheria ya muungano Zanzibar na Tanganyika we did, hati zile zililetwa Bunge la Tanganyika likaridhia, Tanganyika tukatunga sheria ya muungano, ile tarehe 23 April, na tarehe 25, Karume akatua kwenye Bunge la Tanganyika kubadilisha hati, kilichofanyika ni hakuna ratification yoyote iliyofanyika Zanzibar, wala Zanzibar haikutunga sheria yoyote ya muungano, bali sheria ya muungano ni moja tuu, iliyotungwa na Bunge la Tanganyika.

Kitendo cha Zanzibar kutoridhia muungano, hakuufanyi muungano kuwa halali, kwasababu muungano ni mkataba hivyo hata kama mkataba haukusainiwa, expressly, lakini ukatekelezwa , unahesabika umeridhiwa impliedly by performance, yaani Zanzibar japo haukuridhia muungano expressly by ratification, imeridhia impliedly by perfomance.

Kanuni hii pia inatumika kwenye forced mariages, ndoa ni mahusiano ya consensus, wanandoa wote wawili wanatakiwa kuridhia. Ndoa ambayo mwanandoa hakuridhia ni voidable marriage. Kuna ndoa nyingi mwanamke analazimishwa kuolewa bila ridhaa yake, forced mariages, akiishafika kwa mumewe, anaingiliwa kwa nguvu bila ridhaa yake, yaani anabakwa!, akishika ujauzito na kuamua kusalia kwenye ndoa hiyo huku akitimiza majukumu ya lile tendo, hata kama alilazimishwa, kisheria anahesabiwa ame consent hiyo ndoa, na inakuwa ni ndoa halali by performance, lakini mwanamke yule baada ya kufika kwa mume, akigomea tendo la ndoa kata kata, ndop hiyo inakuwa ni ndoa batili.

Hivyo ndivyo muungano ulivyo kwa Zanzibar, Wazanzibari japo hawakuridhia, lakini wameihudumia hii ndoa ya muungano, by perfomance, wanahesabika wameridhia na muungano ni halali!
Kifupi, Haya ni matusi mazito sana kwa Taifa letu nanhasa katika jamii ambayo tumeishi zaidi ya miaka 60 tukiamini sisi wote ni Watanzania.
Hoja kuwa Zanzibar haukuridhia muungano, sio matusi, it is a fact!.
Ukisikia Wazanzibar wanadai NCHI yao na Watanganyika wanadai NCHI yao. Muungano haramu hauwezi kuunda Serikali ya Shirikisho kwenye Muungano Haramu.
Muungano sio haramu, ni muungano halali hata kama umeingiwa ki haramu, kama ilivyo kwa mwana haramu, ni mtoto aliyetungwa nje ya ndoa na aliyezaliwa nje ya ndoa. Uharamu wa mtoto ni alipotungwa kama hakuna ndoa, tendo hilo ni zinaa, lakini baada ya kutunga mimba haramu, ukaamua kumuoa huyo mwanamke, siku mtoto anazaliwa, anakuwa ni mtoto halali. Muungano uliingiwa kiharamu Zanzibar, hivyo ni momba haramu, lakini baada ya April 26, Tannganika na Zanzibar kuwa ni nchi moja, sheria ile ile moja ya muungano ya Tanganyika, imetosha kuuhalalisha muungano Zanzibar kwasababu sasa ni nchi moja ya Tanzania.
Kama hutuutambui Muungano, tunawezaje kuunda Serikali zozote ndani ya Muungano usotambuliwa? Kama hutuutambui Muungano wetu wala hauna ridhaa yetu, tunataka Serikali 3 za kitu gani?
Kama kuna mtu yoyote anadiriki kusema hautambui muungano!, huyo ni kichaa!, ni mwendawazimu!, na vichaa hao na wendawazimu hao wako wengi tuu. Mimi niliwahi kumshauri Dr Shein Dkt. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii na pia Dr. Mwinyi Ushauri wa Bure kwa Dkt. Hussein Mwinyi: Mfute Kazi Haraka Othman Masoud Kabla Hajaendelea Kueneza Sumu
Namshukuru Mungu wachawi wameanza kutua juu ya paa mchana kweupe. Na kibaya zaidi zile sifa za KiongoI tumtakae, alizosema Mwalimu mwaka 1995 kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Chama chake zimebakia kuwa hadithi nyingine ndani ya Kitabu.

Tuliombee taifa letu, aidha maneno ya Mwalimu yametimia, tunasubiri Utabiri wa Sheikh Yahya Hussein.

Masalaam
Utatimia!
Huu Muungano wetu Adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!
Mungu Ibariki Tanzania
P
 
Back
Top Bottom