Akiwa Kanisani, Ole Sabaya atangaza kuwaomba msamaha aliowakosea

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,314
5,478
Mwanasiasa Lengai Ole Sabaya ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, amewaomba msamaha wote aliwakosea na kusema amewasamehe wale wote waliomkosea.

Amesema hayo katika Kanisa la Ebenezer Restoration Ministry For All Nations Jijini Arusha katika ibada ya shukrani, leo Jumapili Februari 4, 2024.

Sabaya amesema hataendeleza vita na maadui zake, bali anawaachia Mungu. Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mifumo ya haki na usawa nchini.

Ikumbukwe Aprili 5, 2023 Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi ilimwachia huru Sabaya baada ya kukiri kosa la kula njama pamoja na makosa mbalimbali yaliyokuwa yakimkabili.

Pia Sabaya aliachiwa huru kwa kesi nyingine mbili za matumizi mabaya ya madaraka na uhujumu uchumi, zilizoendeshwa jijini Arusha.

Chanzo: Mwananchi
 
Your browser is not able to display this video.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amewaomba msamaha wote aliwakosea na kusema amewasamehe wale wote waliomkosea.

Amesema hayo leo Jumapili Februari 4,2024 katika Kanisa la Ebenezer Restoration Ministry For All Nations, lililopo jijini Arusha katika ibada ya shukrani.

Sabaya amesema hataendeleza vita na maadui zake, bali anawaachia Mungu. Pia amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mifumo ya haki na usawa nchini.

Ikumbukwe Aprili 5, 2023 Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi ilimwachia huru Sabaya baada ya kukiri kosa la kula njama pamoja na makosa mbalimbali yaliyokuwa yakimkabili.

Pia Sabaya aliachiwa huru kwa kesi nyingine mbili za matumizi mabaya ya madaraka na uhujumu uchumi, zilizoendeshwa jijini Arusha.
 
Zile mil 90 alizokwapua mstaafu atazilipa au inakuwaje ??
 
Kama mnaakili basi mmejua kisa ya baba ake kwanini amepewa cheo na yeye kuachiwa akiri ni mari
 
Huyu chui aliyejivika ngozi ya kondoo hana kingine kwenye akili yake zaidi ya kubembeleza cheo ili aendeleze matendo yake maovu,eti na yeye amesamehe! Amsamehe nani sasa wakati yeye ndiyo kaumiza watu wasio na hatia ili kumfurahisha bwana wake Jiwe,tunamsihi mteuzi haya mambo ya kuwarudisha serikalini hawa wauaji sio sawa hata kidogo hata kama na yeye ana uroho wa madaraka lakini asitafute hayo madaraka kwa njia yoyote na kufikiria hayo majambazi yanaweza kumsaidia.
 
Hivi kumbe ukifika mahakamani ukasomewa mashtaka halafu ukakiri kosa inawezekana kuachiwa huru kabisa?
 
Watu washenzi kama hawa China wananyongwa tu nashangaa mpaka sasa yuko uraiani alitakiwa awe amenyongwa au kifungo cha maisha jela
 
Anatafuta kiki ili akawe msaidizi wa mwenezi
 
na wale aliowapora pesa arudishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…