Akinababa Tusitelekeze Watoto wa Kuchepuka

Akinababa Tusitelekeze Watoto wa Kuchepuka

Masulupwete

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2012
Posts
2,366
Reaction score
2,438
Kuna baadhi ya akinababa wamekuwa na tabia ya kuwakataa na hatimaye kuwatelekeza watoto wao hasa wale wanaozaliwa nje ya ndoa zao (waliozaa na michepuko).

Kwa uchunguzi wangu, mara nyingi mungu huwa hawatupi watoto wa aina hii. Na mara nyingi watoto huja kuwa wakombozi wa familia baadaye.

Kuna mmoja huyu ni jamaa yangu kabisa. Yeye alipata watoto 5 ndani ya ndoa na wengine 3 nje ya ndoa. Huyu jamaa yangu aliwakataa na kuwatelekeza hawa watoto wa nje ya ndoa.

Kinachotokea sasa jamaa umri umesogea anahitaji msaada wa watoto. Wale watoto 5 wamekula kona hawana habari naye na badala yake sasa anatunzwa na wale watoto 3 aliowakataa huko nyuma.

Wababa tusikatae watoto.

Mtoto hausiki kwa namna yoyote na ugomvi wa wazazi.

Mtoto ni rasilimali ya baadae.

Kitanda hakizai haramu.
 
Tatizo wanawake nao mmekuwa wajuaji sana kipindi hiki, mnakosana kidogo tu anakwambia eti "hata tukiachana bado nalipa, nina uwezo wa kumtunza mwanangu"
Kama kawaida sisi wanaume hatuna mambo mengi, mapema kabisa tunakufungashia vilago na magunia yako yote.
Unafika mtaani mambo yanakuwa ndiyo sivyo, mtoto anakuwa wa mtaani, wewe unaanza kuwa mdangaji.
 
Wanawake wengi siku hizi pia wanakitabia cha ajabu sana,mumepishana anakwambia "huyu mtoto sio wako" mwanaume unabaki njia panda huyu mtoto ni wangu au kweli sio wangu?
Ukichanganya na hofu ya kulea mtoto asiye wako mtu huyooo anakula kona,kumbe maskini wa Mungu ni mtoto wako kabisaa!
 
...
IMG-20190826-WA0007.jpeg
 
Cha msingi wanawake muache kutegeshea mimba kabla ya ndoa, namuache kuwatega waume za watu kisha kuzaa nao ili kuwafanya watoto vitega uchumi vyenyu [emoji108][emoji108]
 
Wanawake saingine huwa wanaangushana wenyewe kwa wenyewe,
Yani unakubali kutembea na mume wa mtu bila kusita [emoji87][emoji87]

Je ungekuwa wewe ndiye uliyeolewa ungejisikiaje kufanyiwa hivyo?

Usilopenda wewe kufanyia usimfanyie mwenzio!
 
Kwanza unatekelezaje mtoto wako...

Mi nilishasema mwanangu Ni mwanangu hata km huyo mtoto nilimpata na mwanamke kwa one night stand.... Kikubwa awe mwanangu.
 
Hii Ni kwa sababu wanaume tumejikuta tunatekeleza interest za wanawake kuliko majukumu yetu ya ubaba.
Baba hawezi kutelekeza mtoto ambaye anajua alichomeka na kumwaga ndani na matokeo ndio huyo mtoto.
Unapotekeleza matakwa ya mkeo na mwili wako haujakubali madhara yake ndio hayo.
Wanawake daima Ni wabinafsi kwenye vya kwao tu.
Atakuchomekea mtoto lakini akisikia una mtoto na mwanamke mwingine hataki umtunze Ila wa kwake ndio unamtunza.
Na wanaume wengi wamejikuta wakilea watoto wa wenzao huko kwenye ndoa zao na kuwaacha watoto wao halisi wakiteseka.
Hawa wake zetu wanachepuka Sana humu wanamoshinda. Tena hata Kinga hawatumii. Mwanaume Ukizaa nje usikwepe kumlea huyo mtoto!!
Hata kwa kujistretch mwenyewe!!
 
Yani mwanaume umeoa, ukaamua kufanya uasi kwa kufanya umalaya,
Huo umalaya wako ukaona hautoshi ukaamua kuweka alama ya kudumu ya umalaya wako!

Mwanaume kuzaa nje ya ndoa ni alama ya kudumu kwa vizazi hata vizazi kuonesha kuwa ulikuwa muasi na malaya!
 
Na mpaka unasingiziwa kuwa huenda ni mwanao bado haisaidii maana hadi mwanamke akusingizie au akuchomekee kuwa ni mwanao maana yake ulishawahi kujamiana nae huyo mwanamke !
 
Back
Top Bottom