Akina dada wengi wana ugonjwa wa kulia shida

Akina dada wengi wana ugonjwa wa kulia shida

Karot

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2017
Posts
1,159
Reaction score
1,316
Salaam wakuu..
Toka mwaka uanze sijadondosha thread hapa, naomba ruhusa yenu nitiririke kidogo. Na hii naomba akina dada mchangie kwa sana ili nipate kujua ugonjwa wenu unasababishwa na nini.

Unakuta una date na mwanaume ndani ya siku tatu unaanza kumuangushia shida kede kede hali ya kuwa kabla hamjaonana sijui ulikua unahudumiwa na nani...
Naongea nikiwa na uzoefu nalo na pia tayari linishanikuta...

Jinsi nilivo date na mdada halafu akataka kunigeuza ATM ndani ya siku tatu...

Nilianzisha mahusiano nae siku ya kwanza ikapita ya pili nayo free kimbembe siku ya tatu...
Nilianza kuambiwa sina hela ya chai na huo mtindo ulitakiwa uwe endelevu, akanambia gas imeisha nikamwekea limemaliza hili nikaambiwa kodi ndani ya wiki hiyo hiyo. Nikajua hapa kinachofata nitafilisiwa ikabidia nitunge uongo ili angalau nipumuwe angalau mwezi.

Kilichonishangaza ni kwamba na mimi niliomba game nikajibiwa bado mapema... Sasa hapo na mimi nikapata sababu, alikua akiniomba kitu namjibu bado mapema akawa ananuna.
Nikaamua kumwacha aende maana nilijua hapana litakalokuwa.

Kwenu akina dada kwanini mnakuwa hivi? Hamjui kula na kipofu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora hata wewe siku tatu,
Mimi baada ya masaa manne ya kupeana namba na kuanza kuchat nikaambiwa mwenye nyumba anataka kumfukuza sababu hajalipa pesa ya umeme na maji kwa miezi mitatu hivyo nimlipie siku hiyo hiyo kabla hajafukuzwa kesho yake.

Ugumu wa maisha tu hakuna mtu anayependa kua omba omba.
 
Mkuu unakubali kuwa wewe ni kipofu??

Ukishadate na a girl mkuu,jiandae tu kwa yote hayo
 
Bora hata wewe siku tatu,
Mimi baada ya masaa manne ya kupeana namba na kuanza kuchat nikaambiwa mwenye nyumba anataka kumfukuza sababu hajalipa pesa ya umeme na maji kwa miezi mitatu hivyo nimlipie siku hiyo hiyo kabla hajafukuzwa kesho yake.

Ugumu wa maisha tu hakuna mtu anayependa kua omba omba.
Mkuu ID yako ni Culture gal bila Shaka ni KE Imekuwaje tena kuombwa hela ya umeme na maji au mm ndio niko nyuma ya wakati?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukioa;

Unalipa pango ( kodi ) ya nyumba

Unalipa gharama za umeme

Unalipa gharama za maji

Unalipa ada za watoto shule

Unalipa gharama za mkeo salon, unamgharamia simu na vocha na mavazi

Unalipa gharama zote za matumizi ya ndani kama chakula, malazi na mavazi ya familia

Unalipa gharama za matibabu ikitokea mwanafamilia kaugua

Utaratibu huu hauibuki tu toka hewani, ni utaratibu uliojengeka tangu enzi za kale huko hivyo umeshajengeka katika mifumo ya fahamu tangu utoto hadi ujana na ukubwa kisha uzeeni.

Kumudu majukumu yote hayo kwa mwanaume sio kazi ndogo na mjengeko wake hauji tu ukubwani. Namna unavomudu kuendesha mahusiano yako tangu ujana ndivyo hivyo hivyo utakavyomudu hata utakapoamua kuanza kuwa na familia kwa maana ya kuoa na kuwa na watoto.

Wazazi wangu walinifunza mara zote kwamba mwanaume ukitoka nyumbani ni vema unaporudi walau uwe na chochote kitu mikononi hata kama ni kidogo kwaajili ya familia.
 
Bora hata wewe siku tatu,
Mimi baada ya masaa manne ya kupeana namba na kuanza kuchat nikaambiwa mwenye nyumba anataka kumfukuza sababu hajalipa pesa ya umeme na maji kwa miezi mitatu hivyo nimlipie siku hiyo hiyo kabla hajafukuzwa kesho yake.

Ugumu wa maisha tu hakuna mtu anayependa kua omba omba.
Babe halafu na mie nilikuwa na shida kama hii hii yani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom