Mpwa hiyo ni kweli kabisa. Umesahau na umma, vijiko na tule tuvijiti twa kuchokonoa meno. Ukitaka kujua, tembelea makabati ya vyombo ya mashosti. Utakuta glasi tofauti tofauti kibao. Ngoja waje kina Carmel, FL1, Msindima, MJ1, Lily Flower, JS, VC ZD na
Chris,
Hatupingi mradi kupinga tu.... ukiona lasemwa ujue lipo.Mimi binafsi niliwahi kuona glass zilizoandikwa TTC ( Tanzania Tourist Corporation) kwa familia moja niliitembelea zamani. Glass hizi zilikuwa zinatumika katika mahoteli ya kitalii kama Bahari Beach, Kunduchi Beach, New Africa, n.k.
Pia niliwahi kusikia mtu mmoja mkubwa tu mwanaume aliwahi kuadhirika baada ya umma, visu na vijiko kudondoka alipokuwa anatoka katika hotel moja maarufu ya kitalii enzi zileeee za mwalimu.Dume hili lilificha cutlery hizo kwenye soksi! Hvyo basi si lazima vifichwe kwenye mapochi ya kina dada/mama bali hata soksi za akina kaka na baba!Vile vile...
Kuna watu huchukua vitu kutoka mahotelini kama mataulo na hata shuka.Niliwahi kushuhudia Mzungu akitolewa nishai kwa kuiba taulo katika hotel moja ya kitalii Arusha.
Wengine huiba vitu kutoka kwenye ndege kama glass za daraja la kwanza, na freshening products ( colognes etc) Hizi ni tofauti na zile toilet bags zinazotolewa kama complimentary kutegemeana na daraja.
Kuna wengine nao wakija nyumbani kwako lazima wanyanyuke na kitu... hii imewahi kunitokea ila siwezi kusema kama ni mwanamke au mwanaume alifanya hivyo.
Kwa kifupi nadhani hizi ni tabia za watu....WAWE WANAWAKE AU WANAUME.