Akina dada budi wabadilike kwa hili

jmnamba

Senior Member
Mar 31, 2012
156
25
Akili ya kudhani kuwa wanaume wanaume almost sote twapenda ama kuvutiwa na wanawake weupe! Urembo uliopewa Mungu hajakosea haileti maana kutumia mkorogo nk ili kubadilisha rangi ya ngozi yako! Sijui kama huwa yanaangaliwa madhara kwanza ama uzuri kwanza... Siku hizi imeingia hadi alie na weupe kidogo anajazia awe mzungu kabisa! Haipendezi kabisa. Tunawacheka moyoni wanaofanya hivyo hii tabia haipendezi.
 
...kuna wale wenzetu wanatoa ng'ombe nyingi sana kwa wanawake kama hao...labda wanachangia...tehe!..
ila sio ishu...
 
Tabia hii ni ushamba na kujinyanyapaa, huwezi acha rangi yako ya asili yenye kila kitu na kuingia gharama kwa rangi bandia na yenye madhara. Wenye ngozi nyeusi laiti kama wangekuwa wanajua kuwa rangi nyeupe ni yenye matatizo na inayohitaji uangalizi wa hali ya juu wasingejaribu kuharibu asili yao, nawapa pole waathirika wa mawazo mgando hayo.
 
Akili ya kudhani kuwa wanaume wanaume almost sote twapenda ama kuvutiwa na wanawake weupe! Urembo uliopewa Mungu hajakosea haileti maana kutumia mkorogo nk ili kubadilisha rangi ya ngozi yako! Sijui kama huwa yanaangaliwa madhara kwanza ama uzuri kwanza... Siku hizi imeingia hadi alie na weupe kidogo anajazia awe mzungu kabisa! Haipendezi kabisa. Tunawacheka moyoni wanaofanya hivyo hii tabia haipendezi.

Umenena vema. Tabia hii naichukia sana!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom