Akina Butiku wapo wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akina Butiku wapo wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Aug 10, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Kwa jinsi walivyoongea kwenye kongamano lao sikutegemea kama hawa jamaa wangekuwa kimya hivi.
  Mbaya zaidi walikuwa wanaongea fact, Mzee Makamba akawaita WEHU!
  Nilitegemea wangeshaonyesha msimamo wao wa kutoiunga CCM mkono waziwazi ili kubadilisha timu ya wezi na kuiweka timu ya waadilifu serikalini.

  Hapa ndipo ninapoamini kuwa SIASA haiendeshwi bila unafiki!
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!! Umeshawahi kula ndimu mbele ya mpuliza tarumbeta??? basi ndicho CCM walichofanya kwa hawa wakuu,
   
 3. Nungunungu

  Nungunungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2010
  Joined: Feb 13, 2007
  Messages: 312
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapo chadema kupitia gazeti la Raia Mwema!
   
 4. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #4
  Aug 10, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wapo hao viongozi si unajua siku hizi CCM wamejifanya nasi kujifanya ni wanviburi sasa sijui kile kipindi cha mwalimu walikuwa ni bendera fuata upepo au leo hao wazee wakiwaambia sio hivi oooh mbona nyie enzi zenu hamkusahihisha hivi au vile sasa imekuwa malipizano au nyie mlioko madarakani kama mliona wao walikosea na sasa si mlekebishe tuwaone mkikosolewa kubalini. tatizo viongozi wa sasa hawaambilikiki kabisa ukiwambia neno linatoke sikio la pili tena kwa speed ya ajabu kweli kweli, ati wao ndio wao jamani mmmh.

  Me nadhani ni vyema tu hao wazee wakae kimya kabisa tuli na wajionee kandanda la hao CCM viongozi wa sasa maaana hawa viongozi hawataki kabisa kuingiliwa wala kushaurika kabisa ng'oooo
   
 5. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Labda hawajaiona hiyo "timu ya waadilifu" na zaidi sana "iliyo tayari kutawala nchi".
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Butiku yupo. Afya yake haijawa nzuri siku za hivi karibuni. Kafanyiwa operesheni lakini nasikia anaendelea vizuri. Tusiwe wepesi kuhukumu.
   
 7. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Wafanye nini wazee wa watu? Walishajisemeaga wakamaliza, mawazoni mwao nadhani walitegemea labda ile move inge-spark reaction from the crowd (public) lakini wapi bwana.
  Nani hata alitishia (kutishia tu) kufanya maandamano ya kuwaunga mkono?
  Wabongo (wasomi na kinyume chake) woote kimyaaa.
  Nchi hii tunahitaji Rawlings (au hata Kagame) wetu ili tunyooke na kuanza kuwa na mitizamo ambayo ni tangible.
  Slaa anaweza kujaribu (na nitampigia kura kwa vile hakuna aliye bora mwingine kwa sasa), lakini sina uhakika he is as steely as those two I have mentioned.
   
 8. M

  Masonjo JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2010
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 2,725
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Na viongozi wenzake watakuwa akina nani?
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kiongozi anakuwa moja, wengine ni wasaidizi tu. Uraisi hauna ubia bali una washauri tu ambao si lazima uwasikilize - The buck stops with the President, upo ? Kiongozi anapovurunda anatakiwa awajibike na si kuwatafuta wa kuwatupia lawama kama akina Lowassa au Karamagi, hapana.
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180

  Isije ikawa ndio mambo ya Sheikh Yahya kuwa yeyote atakayekwenda kinyume na mkwere ataadhibika; maana baada ya lile kongamano pia tulisikia Sinde warioba nae akawa mahututi akapelekwa South!! Si mlisikia kuwa mara baada ya DR. Slaa kuchukua fomu jamaa alikimbilia Msoga na baada ya siku mbili Dr. akavunjika mkono eti bafuni; lakini safari hii hata mchinje kondoo ngapi hamuachiwi mpaka kieleweke!!
   
 11. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Sasa utampigiaje kura mtu usiye na hakika naye?
   
 12. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Sijui ni lini wadanganyika tutaacha kuwa washirikina au kuamini ushirikina! Ni aibu
   
 13. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #13
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  ........kwa sabau ni bora kuliko aliye madarakani
   
 14. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #14
  Aug 11, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,543
  Likes Received: 2,252
  Trophy Points: 280
  Wapo sana na wanaona ila watasemea wapi wakati wapo nje ya pango??hawapewi hata nafasi yakujihusisha na shughuli zozote za chama wamekuwa kama mimi nawewe!!!wamebanwa unacheza na hicho chama???:eyeroll2:
   
 15. M-mbabe

  M-mbabe JF-Expert Member

  #15
  Aug 11, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 4,988
  Likes Received: 3,737
  Trophy Points: 280
  Mag3 amelijibu hili na sidhani kama kuna haja ya kuongeza kitu....
   
 16. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #16
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  wacha wakae kimya, nasikia JK kawapiga stop kujenga kikwangua anga pale haribu na ikulu, sasa unategemea watakuwa upande gani, tusubili wakati wa campain
   
 17. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #17
  Aug 11, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Sh. Yahya hana lolote anatisha tu, alishindwa hata na pweza kutabiri mshindi wa World cup.
   
 18. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #18
  Aug 11, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mara hapo viongozi washirikina watakapoondolewa kwenye madaraka!! Uliona wapi mkuu wa nchi anapata ushauri wa waganga wa kienyeji a' la Sangomas jinsi ya kutawala nchi na nchi ikaendelea?
   
Loading...