1. Ukiweza kubuni jambo liwe ni biashara,afya na chochote kile kitakachoweza kutatua shida za jamii wewe= una akiliJamani,mimi naamini kujifunza hakukuishia darasani,na sipendi kufanya mambo kimazoea.Kuna hii kitu nimekua nikisikia tangu mdogo,AKILI.Je ni nini?Je ni ufahamu?Inapimwaje?Shule kwa mfano,yule anaefaulu masomo huonekana ana "akili" lakini ukija mtaani unamkuta ni mlevi,mnyanyasaji,mkatili,mpenda fujo n.k,je huyu kweli ana akili?Au ubongo ni akili?Nijuavyo mimi ubongo ni kifaa anachotumia mtu kufikiri.Sasa akili iko wapi?Inakaa mwilini?Je ni eneo lipi inakaa?Au ufahamu ndio akili,Kama ni ndio ufaham ni akili?Hebu fungukeni mtusaidie sisi wenye kutanzwa na hii kitu!
Jibu lako tosha kabisaaa mkuumkuu eiyer,
akili ni ule uelewa,ufahamu na uwezo wa mtu kutafakari na kutumia maarifa aliyonayo kutoa suluhu ya matatizo mbalimbali(solution to different problems) hapa ieleweke kuwa tatizo si (negative thing) ila kama kitu kihitajicho kutatuliwa.
mfano mwanafunzi anapokuwa kwenye mtihani anakumbana na things which need solution. atatumia uelewa ufahamu na uwezo wake wa tafakuri kutoa suluhu kwa kadri inavyompasa.
akili ni imaginary kama ilivyo thought,yani huwezi ukapasua ubongo ukapima au kuona akili. akili hupimwa kwa kadri mtu anavyoweza kuleta suluhu ya mambo mbalimbali,mfano anaulwiza kitu ama anapaswa kufanya jambo analifanya kwa ufanisi na uhakiki.kwa wakati stahiki, akili hutofautiana baina ya watu.
sasa tunapokuja katika katika mtu mwenye akili kufanya matendo mabaya ni hivi huyu anaweza akawa ana ufahamu mkubwa ama uelewa mkubwa katika kitu fulani lakini sio katika kitu kingine kwa maana nyingine hakuna mwenye akili katika kila kitu. na tabia maadili na akili vyaweza visiende sambamba.
Akili ni Mind set.Mjadala ni mzito kweli kweli.
Naona tunachangia matokeo ya kazi ya akili hatujafikia lengo la swali.
Akili ni nini?????