Ewe mzazi, mkinge mwanao dhidi ya gonjwa hili la akili

Nyenyere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
14,770
10,650
UTANGULIZI
Wakuu, poleni Na mnyukano wa CORONA. Leo nina hoja ndogo lakini ni muhimu mno kwa wanajamii. Licha ya tishio la korona ni lazima maisha yaendelee.

Kwa kawaida ukiona kichaa anakula jalalani hushangai, ana tatizo la akili. Hata kama utajaribu kumrejesha nyumbani ale chakula cha kawaida bado atatoroka na kurudi jalalani kusaka riziki. Huo ni ulemavu wa ubongo ambao umeharibu kabisa mfumo wa kawaida wa binadamu.

Ndivyo ilivyo kwa wale wote wanaojihusisha na mapenzi KINYUME NA MAUMBILE. Nasikitika kusema hawa nao ni VICHAA, wana magonjwa ya akili hata kama hawaambiwi ukweli huu. Ukiona mtu anapewa chakula safi mezani kilichoandaliwa kwa ajili ya kuliwa (uke) halafu asiridhike akatamani chakula cha jalalani (sehemu ya haja kubwa) basi kuna fyuzi zimekatika kwenye ubongo wake!! Sio jambo la kawaida mtu kutamani sehemu ya kutolea uchafu (jalala) halafu akajisikia kufurahia mlo na kuwa na amani kabisa!! Aibu kubwa mno.

Tena wako wale ambao wao wakiona wanaume wenzao ashki zinawashika vibaya, hawa wana kichaa kilicho komaa. Usithubutu kumkanya mtu wa namna hii, ataweza hata kukudhuru. Yaani mwanamume mwenye akili timamu avutiwe na matako ya mwanamume mwenzie kiasi akose usingizi!! Halafu bado watu wa namna hii tunaishi nao kwenye jamii zetu tukiwaona wako kawaida? HAWA WANAPASWA KUWA MIREMBE DODOMA.

Kwa sababu ugonjwa huu umeanzia kwa wale waliotushikia akili zetu basi wamejaribu kuuhalalisha na sisi huku tunaitikia TAWIRE. Tumekubali kuishi na wagonjwa hawa na hata kuiga tabia zao za kula chakula jalalani. Leo hii mwanamke asiyetoa nyuma anaonekana kituko kwani hilo si mjadala tena, wala hakuna anayeshangaa kusikia mama fulani anatoa nyuma. Bali inakuwa ajabu ya karne pale inaposemwa kuna binti ni mgumu kutoa nyuma. Wanawake kwa kiasi kikubwa wanaambukizwa ugonjwa huu kiurahisi sana kwa sababu ya tamaa.

SABABU KUU YA UATHIRIKA HUU
Hapa naomba tujadili kama wazazi walezi. Kuna ukweli ambao wengi ama hatuufahamu ama tumeamua kuupuuzia: matatizo haya ya akili yamekuja sambamba na televisheni na internet. Kama utavuta Kumbukumbu miaka kadhaa nyuma utaona jinsi gani jamii nzima ilichukia mno ufedhuli huu na haukuwa tatizo katika jamii. Ujio wa TV na mtandao umeleta ujuzi mpya sambamba na ugonjwa wa akili.

Mzazi unapomruhusu mwanao kutumia muda wake kuperuzi mtandao unamwandaa kuugua magonjwa ya akili. Ziko kurasa nyingi njema tu mfano za masomo, hizo ni kweli zaweza kumsaidia, lakini si jukumu lake kuingia mtandaoni kuzisaka mzazi ukiwa haupo kumsimamia. Naweza ongea kama niliyepitwa na wakati lakini liko neno hapa:

Katika ukristo biblia inasema imani huja jwa KUSIKIA, na kusikia kwa NENO LA MUNGU. Sentensi hiyo iko sahihi katika mazingira yote kabisa. Imani maana yake ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo. Mtoto anafundishwa kwamba jambo fulani ni tamu, zuri na la kawaida kabisa. Haya anayapata huko anakokuwa mbali na wazazi wake. Ndio maana ya imani chanzo chake ni KUSIKIA. Anaanza kwanza kuzisikiliza sauti za marafiki na watu wengine wagonjwa wa akili, wanamjaza ujinga. Kwa hiyo ukimtazama kwa nje utaona kuwa hana tatizo kabisa, ni mwadilifu na mtulivu. Lakini kumbe moyoni amejazwa shauku ya kutafiti mambo ya hovyo akiamini ni mema na mazuri.

Kusikia kwa Neno la Mungu - hebu hapo sema kusikia huja kwa neno la mzazi. Utaona tayari msemo huu una maana kila mahali. Mzazi usipokuwa karibu na mwanao ukampa uhuru wa kuperuzi hovyo mtandaoni hakika atafanya tafiti zake. Humo lazima atakutana na kirusi hatari ambacho hushambulia neva za ubongo. Pale atakapoona mambo ya chumbani tu, basi ufahamu wake utahama naye hatokuwa binadamu wa kawaida. Kufuatia umahiri wa waigizaji hao wa mtandaoni, atashikwa na shauku ya kujaribu ajionee mwenyewe. Ndio maana nasema usimruhusu mwanao awe KING OF SOCIAL MEDIA katika umri ambao jema huliona baya na baya kuliona jema.

Haya, wewe mzazi umekuwa makini na sasa unamfungulia kurasa za mitandaoni unazotaka azipitie, kisha unazima net mpaka ahitaji tena. Vipi kuhusu TV? Mwanao ndio mshika rimoti, channel zake ni Clouds, Channel 5, Wasafi media, Bongo muvi. Waweza kudhani hizi hazina madhara, lakini leo nakuambia, si kwa kuharibu biashara za watu, bali kusema iliyo kweli. Usikubali mwanao awe mtumwa wa huu ujinga!! Huku atalishwa ujinga na hawezi kamwe kujifunza uhalisia wa maisha. Hayo mamiziki 24/7 ni kuwafundisha mapenzi na kwamba kutokuwa na boy/girl friend ni dhambi. Unadhani mwanao atajisikia yuko kawaida kama hana rafiki wa kumliwaza? Bongo movie imegeuka tasnia ya ngono iliyobarikiwa na BASATA!! Yaani hadithi zao zote ni kuwafundisha watoto kuwa na marafiki opposite sex na wawe wanatafunana! Mlinde mwanao kabla hajapatwa na gonjwa la akili.

Sasa mambo huanzia huko kisha watoto hufanya tafiti zaidi, kutaka kujua na upande wa pili kuna raha gani!! Hapo ndipo wa kiume huingiliwa na wa kike hutoa nyuma. Imani chanzo chake ni kusikia, sasa kama mwanao hasikii neno lako wewe kama mungu wake, basi atasikia ya kwenye TV na mtandao.

UFANYE NINI KAMA MZAZI
Ukiwa mzazi makini, hakikisha mwanao anabaki kuwa mtoto tu. Mtoto hapangi anachotaka bali anapangiwa. Achana kabisa na habari za haki za watoto, sijui kujumuika na wenzao, kujichagulia channel n.k. Epuka kuwa mdau wa haki za watoto.

Mtoto abaki kuwa mtoto tu kwa vipi? Wewe mzazi ndiye mwenye maamuzi yote, ukiona mwanao anaanza kukupinga katika mambo ambayo ni ya msingi kwake basi ujue anasikiliza sauti za nje. Mtoto ana uchaguzi mmoja tu, ni ama aendelee kuwa mtoto akae nyumbani ama awe mtu mzima mwenye maamuzi binafsi aondoke akajitegemee. Mtoto ataanza kuwa na maamuzi yake mwenyewe pale anapokuwa na mji wake, period. Usimruhusu kamwe awe na maamuzi binafsi kwenye mji wako. Hapo ni kwako, watoto ni wapitaji tu, usiwageuze wawe wenye mji, vinginevyo wewe ni boksi!!

Usiruhusu mwanao awe mtaalamu wa kusimulia kila toleo la bongo movie na bongo fleva. Usijigambe kwa sababu mwanao ni gwiji la miondoko ya ngwasuma. Usiruhusu kabisa mwanao ajazwe ujinga kwa kumwacha huru kwenye TV. Huo sio mji wake!! Hapo ni kwako wewe mzazi, wakati wake yeye bado!! Unaanzaje kumruhusu mtoto ajichagulie nguo za kununua? Yaani mtoto anakwenda kusuka saluni bila maelekezo ya mzazi, anaongozwa na kile alichokiona kwenye TV!? Kiujazacho moyo wa mtu ndicho kimtokacho!! Moyo ukijaa kiduku utatoa kiduku siku ya kunyoa. Halafu utasikia mzazi eti anamwambia mwana, shauri yako walimu watakuchapa shuleni!! Hivi wewe ni mzazi kweli??

Yako mengi lakini niombe tusiwaache watoto wetu wapatwe na gonjwa la akili. Mzazi katili hutoa watoto bora (sio mnyanyasaji bali anayewakatili watoto kufanya mambo ya kijinga). Usitafute kupendwa na mwanao akuone kama mshikaji wake, wakati wa utoto lazima awe makini kwani anajua akijichanganya kidogo tu, kazi anayo. Kisha uje uone atakapokuwa mtu mzima atakavyo kupenda maradufu. Hakuna kitu kinachomharibu mtoto kama UPENDO WA KIJINGA. Vitoto vingi vinatafunwa mtaani kwa sababu ya upendo mkubwa wa wazazi kwao. Wamewapenda kiasi cha kuwapa watoto uhuru wa kutosha. Ukifika nyumbani haifahamiki mzazi ni nani na mtoto ni nani. Wote ni wenye mji, ujinga wa ajabu kweli.

Next time nitaongelea experience yangu kwa shule mbili ama tatu za sekondari zilizo mitaa yangu ambazo zimegeuka kuwa madanguro.

Mwenyezi Mungu akulinde dhidi ya CORONA.

Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
siku ambayo nilishuhudia mtoto like 5years hivi wakike amelawitiwa na kuwekwa udongo huko nyuma then ameanza kutoa wadudu niliumia na kuwaza mengi mkuu..hawa mshana Jr anawaitaga hayawani

Sent using Jamii Forums mobile app
Binafsi siwezi vumilia hali hiyo. Ni unyama uliopitiliza. Mtu anaanzaje kumtamani mtoto mdogo namna hiyo? Huo ni mtindio wa ubongo. Sasa jamii imetazama upande mmoja tu wa mtoto lakini haioni kwamba hata wanaofanya kinyume na maumbile wana matatizo ya akili


Sent from my SM-A720F using Tapatalk
 
Binafsi siwezi vumilia hali hiyo. Ni unyama uliopitiliza. Mtu anaanzaje kumtamani mtoto mdogo namna hiyo? Huo ni mtindio wa ubongo. Sasa jamii imetazama upande mmoja tu wa mtoto lakini haioni kwamba hata wanaofanya kinyume na maumbile wana matatizo ya akili


Sent from my SM-A720F using Tapatalk
Kweli mkuu tena mikoa mikubwa matukio kama haya yapo mengi nadhani watu wanastress sana na ndo ukichaa wenyewe unaanzia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom