Akili za watanzania na mambo yapitayo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akili za watanzania na mambo yapitayo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwanamageuko, Mar 11, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Ukianzia kwenye DECI... UTAPATA PICHA kisha uchaguzi.... UTAPATA PICHA. Itazame DOWANS.... UTAPATA PICHA...Ukifikiria ya Shehe Yahya Hussein UTAPATA PICHA! Kisha tazama vema maandamano ya Vyama vya siasa na WANAFUNZI.... UTAPATA PICHA! kwa sasa jambo linalovuma na kutikisa masikio na fikra za WATANZANIA... ni babu wa LOLIONDO! watu wamesahaulishwa... taabu na mashaka yao... watu hawajiulizi wala kutaka kudadisi.... (DIABLE!!! watu wanasahau ya kwamba UTAMU WA PIPI NI MATE YAO! Watu hawatazami yanakoanzia wala hawataki kupima matokeo ya mwisho... Ni nyimbo zipitazo ambazo kwa akili za watanzania wanazicheza bila kujua mdundo wake.... na ili kupatikana vema basi wale wanaoitwa vigogo ni mashuhuda! hapo ndiposa kina sisi tunapoingizwa king!!

  Baada ya wengi kufika kule na kukwama huduma kutokana na ughali wa maisha ulioko pale sasa wanasema serikali imewatekeleza! kana kwamba serikali ndio iliyowapeleka kule ama kuwatuma huko! NI AKILI ZA WATANZANIA KUTAKA KUFANYIWA KILA KITU!! Ipo siku watataka serikali au wafadhili WAWAPENGE NA KUWAFUTA KAMASI!! HATUJAWA TAYARI KUJITUMA NA KUJUA NINI MATATIZO YETU.... TUKO TAYARI KUHAMISHWA KWENYE MADA ZA MSINGI KWA MAMBO YA MPITO!

  Ndio maana utaona watu wananeemeka na kutajirika kwa sababu wanaaminiwa kwamba wao ndio ufumbuzi wa maisha kwa wengine!! (hapo suala ni mahesabu tu!) Kama hatukuamka leo... sijui... sijui... maana waliotarajiwa kuwa kwenye maandamano ya kupinga bei za umeme na dowans leo wako Loliondo! Waliotakiwa kuwa kwenye vikao vya RCC leo hii wako kwenye ziara za maandamano! Hii ndio Tanzania!!! Wala hakuna anaehoji, tupo kama kondoo wa kafara!!!

  Si lengo langu kupinga ama ama kusema wanaoyafanya yale wamekosea La! Wako sahihi kwa sababu kinachomponya mtu ni imani yake. Ndio maana mpaka leo wapo wanaopona malaria kwa krorokwini na fancidar haziwaponyi!! Ndio maana wapo wanaoamini utajiri na maisha bora yanatokana na kufanya kazi kwa bidii wakati wengine wakienda kwa kina Shehe Yahya na Kakobe! Wengine wakiona kwamba kuiba ndio njia sahihi na ya haraka hawa wezi haijalishi ni wale wa mifukoni ama waliobatizwa jina tukufu la UFISADI! ili waondokane na jina baya la WEZI! ndio maana leo mtu akiwa na kitambi anaitwa FISADI!!! ni akili za KITANZANIA!!!

  Inatia uchungu kufikiria...

  Mwishowe ukishayafikiri hayo yote utajua kama WATANZANIA HAWAJADATA BASI WAMEROGWA!! Akili zao zimedumazwa kama si matatizo ya miongo kadhaa basi ni ukosefu wa elimu uliokubuhu... Nenda Kenya na Uganda nchi jirani na si mbali zaidi ya hapo utapata picha hii: Kila baada ya nyumba tatu kuna aina fulani ya shule kama si chekechea, shule ya msingi au sekondari kama si hivyo patakuwepo aina fulani ya chuo cha taaluma fulani, lakini njoo Tanzania kila nyumba tatu kuna Lodge kama si baa, grosari au guest house!!

  TAZAMENI NANYI NDUGU ZANGU....
  TUMETOKA WAPI NA TUNATAKA KWENDA WAPI?
   
Loading...