Kwa kweli Elimu ya sasa ijikite kwenye kuwaelimisha vijana namna ya kujiajiri na kutokuchagua kazi, vijana wengi wasomi wanadharau baadhi ya kazi! wako tayari kuwa ombaomba kwa ndugu jamaa na marafiki kuliko kujiajiri katika fursa ndogo ndogo, mfano ofcn kwangu nilikuwa na msaidizi ambaye ndio kwanza amemaliza chuo 2014, mwanzoni lengo lilikuwa ni kumuajiri lakini baadaye ikaingia fitna na siasa ajira ikadunda, mimi sikumuacha, zikaingia fitna ili aondoke niliakikisha anabaki kwa sababu alikuwa msaada sana lakini pia ninamuadmire sana, Tofauti na wasichana wengine wa rika lake anajituma kwenye biashara, kila biashara anafanya! lakini pia alikuwa kwenye network marketing ambayo ilikuwa inamsaidia na kwenye kazi zangu ofisini alikuwa ananisaidia vizuri, hivyo kila alipotaka ruhusa mradi kazi zinapopungua nilikuwa simnyimi. Kila wakati nilipoona kazi mitandaoni na kwenye magazeti nilimuonyesha,nilimpasia fursa nyingi nyingi, huwezi amini interview zote alizoitwa alifaulu. Ikawa kuchagua kazi tu, akachagua ile ambayo itaendeleza career yake upesi.
WITO: Ukiwa kitaani usichague kazi kila fursa unayoiona changamkia.