Akili za wanavyuo bhaana!

Akili za wanavyuo bhaana!

Mtaani kuna fursa kibao za kutengeneza pesa....kinachowafanya wazidi kufulia ni kutuzarau sie tusio soma hata pale tunapowapa idea nzuri tu za kimaisha...hasa kwa haya maisha ya mtaani ambayo hayana formula........mtu yupo radhi hata kukaa home hata miaka kumi akingoja kuajiriwa.....wakati kijijini kwao mashamba yao yamegeuka kuwa mapori....
Kweli braza elimu ya mtaa ndio nguzo mama.
 
Kwa kweli Elimu ya sasa ijikite kwenye kuwaelimisha vijana namna ya kujiajiri na kutokuchagua kazi, vijana wengi wasomi wanadharau baadhi ya kazi! wako tayari kuwa ombaomba kwa ndugu jamaa na marafiki kuliko kujiajiri katika fursa ndogo ndogo, mfano ofcn kwangu nilikuwa na msaidizi ambaye ndio kwanza amemaliza chuo 2014, mwanzoni lengo lilikuwa ni kumuajiri lakini baadaye ikaingia fitna na siasa ajira ikadunda, mimi sikumuacha, zikaingia fitna ili aondoke niliakikisha anabaki kwa sababu alikuwa msaada sana lakini pia ninamuadmire sana, Tofauti na wasichana wengine wa rika lake anajituma kwenye biashara, kila biashara anafanya! lakini pia alikuwa kwenye network marketing ambayo ilikuwa inamsaidia na kwenye kazi zangu ofisini alikuwa ananisaidia vizuri, hivyo kila alipotaka ruhusa mradi kazi zinapopungua nilikuwa simnyimi. Kila wakati nilipoona kazi mitandaoni na kwenye magazeti nilimuonyesha,nilimpasia fursa nyingi nyingi, huwezi amini interview zote alizoitwa alifaulu. Ikawa kuchagua kazi tu, akachagua ile ambayo itaendeleza career yake upesi.
WITO: Ukiwa kitaani usichague kazi kila fursa unayoiona changamkia.
Dawa ni kufanya ajira yoyotee.. huku ukisubiri kazi ya ndoto yako.
 
Daah me ndoto yangu ilikuwa "nimalize chuo, niajiriwe, nimchukue mchumba angu tuishi nyumba nzuriiii" muda haudanganyi aisee, nilimaliza 2013 nikakosa hata tempo nikakomaa shamban mpakan kiteto na wilaya ya kongwa, nilikuwa kaz yangu kuhesabu maiti za wakulima na wafugaji kila asubuh...hatimaye nikaajiriwa, nalipa kodi nyumba ya "daraja la kati" na sina mpango wa kuoa.
 
Ni vizur kuwa na ndoto. Ila usiwe na matumaini makubwa ya kumtegemea mtu au ofisi. Bora uwe na malengo binafsi.
 
Hivi unadhania kusoma ni mchezoo, yan hapo madesa yamezidi thats why wanafunzi wengi wanakuwa na hamu ya kuajiriwa
 
kaazi kweli kweli..imebidi nishushe pumzi ndeeefu baada ya kusoma huu uzi na comments za wadau...alichokisema mleta mada ni kweli tupu kbs juu ya ndoto za wanachuo,I was one among those daylight dreamers,but now I can experience the reality of after school life. Ya Allah tusaidie!
 
Watu sio kwamba hawana fikra za kujiajiri!!! Wanazo saana, TATIZO NI MTAJI WA KUANZA KUJIAJIRI NDUGU. NINGEPATA MTU WA KUNISAIDIA KUPATA MTAJI, MBONA NINGEKUWA NIMESHA JIAJIRI
Wazo lako ndo mtaji wako,kama unajiamini ktk hicho unacho taka kukifanya anza na ulicho nacho badaye timia namba za simu ulizo nazo ktk simu yako kiimarasha mtaji wako.maana si rahisi kws mtu asiyekufahamu kukupa support kwa kitu asicho kiona.
 
Hahaha... ukiwa nje ni rahisi sana kumwona wa ndani anakosea na kumdharau. Na kusema ingekua mimi ningefanya. ila ingia wewe ufanye utaona ugumuu wake. Nahisi anajifunza jambo sasa. Akufuate umpe ushauri wa kusogeza maisha.
Nakumbuka kabla sijaweza kujiingizia kipato nilikuwa nikiwapiga ndugu na jamaa mizinga hasa mama wakiniambia hawana hela nilikuwa naona wananibania sasa ndo najua kwa nini.
Maisha yana changamoto hasa kwa mifumo ya kiafrika ambapo unafika mpaka miaka 25 hujui hata ni unahitaji kufanya maishani mwako
 
Hahahahah

Halafu wakati wa kuzunguka na bahasha hata upake lotion gani unapauka

Body spay ila bado jasho kila mahali litakutoka!
 
Hii hali si ya kufurahisha ni ya kuhudhunisha na kusikitisha pamoja na ukweli kuwa elimu inakupa uwezo wa kuzikabili changamoto lakini bado hatupaswi kuwalaumu watu kwa matarajio makubwa why? kwasababu wao hawajakuta na hali hiyo zaidi ya kuisikia kwa wale waliokumbana nayo. una haki ya kuwashangaa lakini kama una busara huwezi wacheka. kwanza mi nawapongeza pengine na wewe ungekuwa unawaza vitu vidogo vidogo usingekuwa hivyo. let people think big and rich. watafika vipi hiyo ni kazi ya kichwa. wenzetu walioendelea wana tatizo la ajira lakini sio kama kwetu. pamoja na kuwepo tatizo hilo wanathubutu kuwalipa posho raia wao na hakuna excuse na solution ndogo ndogo. lazima tukubali sio kila taaluma ni rais kujiajiri na sio kila mtu anaweza kuthubutu kuwa mjasiliamali. hii nchi ni changa na inahitaji wataalamu ili iende mbele inauma engineer,doctor,mwanasheria,mwalimu na wengine wakose ajira wakati waliopo kwenye ajira mmoja anatoa huduma kwa wananchi zaidi ya 10000. tutafika kweli hapa
 
Kumbe unajua nchi ni changa. engeneer una ajiriwa nini? Fungua kampuni za ujenzi, ufundi hauitaji ajira. Hakuna anaezuiliwa kuwa na matamanio makubwa.,ila yasiwe ya kutegemea kutoka kwa fulani au serikali au taasisi.,kuwa na matarajio yako utayofanya makubwa.
 
Kuna kijana mmoja alianza biashara kwa kutumia mtaji wa mkopo wa elimu alioupata kwa kuuza nguo za kijanja kwa wenzie na mitaani kwa washkaji zake mpaka anamaliza alikuwa ameshasimama kimtaji na hivi sasa anamiliki maduka kadhaa ya nguo na hapa jijini hajui kuomba kazi yeye anaendelea na biashara zake na ndoto zake ni kubwa ajabu.
 
Thats is what needed. Sio kumtegemea mtu makubwa fanya makubwa.
 
WANAVYUO Bhaaaana!!!
Jana Nilienda Kumtembelea Rafiki Yangu Pale IFM nikajikuta nakuwa na siku ya Furaha hasa nilipozisikia story zile zile za wanachuo kumbe story za WANAVYUO karibu wote ni zile zile

Sijui ukiwa chuo akili Inakuwaje hata!
Yaani Unakuwa Unawaza Kumaliza, Kupata kazi, Kupewa kitengo alafu Uanze Kupiga Pesa hahaha huu muda wa kutafuta kazi hauesabii na wala huna plan nao wakati ndio muda mgumu na mrefu mno hata kuliko kufanya kazi
Chuo bhaaana! Yaani ukiwa unasoma Unaona kama vile wengine wanakosea ni mambulula hawajui wayafanyayo wewe ndio mjanja tena unayaona maisha ni mazuri tu yaani huwazi kufeli interview, kukatwa jina, kuchelewa pannel, kukosa wa kukushika mkono, kupata link yenye ajira lakini kila ukibofya vigezo huna, kufanyiwa figisu na hujuma kwenye last audition, kupoteza kumbukumbu ya tarehe ya interview, kufeli training na kadhalika.

Ukiwa chuo unawaza Kumaliza na kupata kazi kama ni mvulana unawaza kuwa na gari nzuri, kuipimp vizuri, kuifunga music system ya maana kumiliki mtoto mzuri na kuchukua mkopo wa nyumba huku LAPF umepewa mkopo wa kujikimu yaani unayachukulia maisha mepesi kuliko hata idea za BONGO MOVIE

Yaani nimezifurahia sana hizo story zenu za Alinacha tena nilimsikia mmoja akisema; "Flani kamaliza hapa mwaka jana kaenda South kasoma sijui nini kwa miezi mi3 karudi CRDB wamemchukua anakula mkwanja acha mchezo, mimi nikimaliza chuo sitaki hata kukaa nyumbani naanza harakati za kutafuta kazi
Nilipowasikia hivyo nilicheka sana nikajua hata watasema tutajiajiri kwenye kilimo ama kwingineko eti watatafuta kazi hahaha

Hivi Kwenye kutafuta kazi kuna harakati kweli au ni kujidanganya?
Utafanyia wapi harakati kwenye interview au kwenye kutuma CV online?
Kiukweli nilipokuwa nawasikiliza nilikumbuka mengi sana kuhusu chuo natamani niwe naenda CHUO mara kwa mara kusikiliza hizi ndoto zao za mchana alafu niwatafute miaka miwili baada ya kugraduate nione % za matunda za harakati hizo
SIJUI HAWAJAJUA KUNA WENGINE WAMETUMA CV KWENYE MAKAMPUNI MPAKA IMEFIKIA WAKATI TANGAZO LA AJIRA LINAPITA AKILICHEKI HIYO KAMPUNI TEYARI WANA CV YAKE.....
JUMAPILI NJEMA.

Usikate tamaa ukipata nafasi tumia. Pia usiwe na matarajio makubwa sanaa na elimu.
Kumbe ulikuwa IFM,mimi niko Block D.Natamani sana nikutafute ili unifundishe ndoto sahihi za kuota,,,,,,,,,,,,,,,huku tunaambiwa ukiwa muhasibu hukosi milioni tatu kwa mwezi,sijui ni kweli?
 
Mtoa Mada wee Ni wale wale Mkatisha watu tamaa Kila binadam Ana plans kichwani na ndoto Kwa nn umdiscourage sasa unapomsdicourage unapata nini.
 
Nimesoma Kila kitu ila kumbka kila mtu Ana malengo yake japo inategemea uwezo, nafasi,muda na mazingira na wale watu wanaomzunguka mtu husika so Acha kila stop discouraging acha apambane kulimga na hvo vigezo hapo juu then baadae muda utazungumza wenyewe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom