Mtatuzi_
Member
- Jun 26, 2016
- 12
- 10
Binti mmoja mwanafunzi wa chuo akiwa ndani ya pantoni akivuka kutoka Magogoni kuelekea upande wa Kigamboni alimuona mwanaume Handsome akiwa ndani ya gari yake nzuri. Bila wasiwasi yule binti akamfuata mwanaume yule na Kumwambia; "Hey awww you look handsome...i like you"
Yule mwanaume akiwa na wasiwasi fulani aksshusha kioo cha gari kidogo kumwambia yule binti; "Mdogo wangu, mapenzi siyo kitu kizuri kwako kwa wakati huu, nakuona umetoka chuo bila shaka, wewe bado ni msichana mdogo kuwa na tabia kama hii. Tafadhali sana nenda nyumbani au sijui Hosteli na usome kwa bidii, wachana na mapenzi soma ili uje ufanikiwe katika maisha."
Baada ya kusema hayo, Yule mwanaume akatoa note book yake na kuanza kuandika huku akisema; "Nakuandikia hapa baadhi ya maneno ya busara na muongozo katika maisha yako. Hutakiwi kuwa cheap kiasi hiki mdogo wangu. Nakuomba sana ukasome haya kabla ya kulala"
Akampa ile karatasi na kufunga kioo cha gari mpaka juu. Yule msichana alirudi Hosteli kwa aibu kubwa na usiku kabla ya kulala akafungua ile karatasi ili aisome.
Karatasi ilisomeka hivi;
"Wewe kipofu nini? Humuoni Mke wangu yupo kwenye kiti cha abiria amekilaza amelala? Hii ni namba yangu nipigie muda wowote isipokuwa asubuhi sana na usiku. Hata hivyo na mimi
nimekupenda sana. Bila shaka hautaniangusha."
Wanaume na akili za Mwendo kasi.!