David M Mrope
Senior Member
- Jul 13, 2021
- 115
- 75
AKILI YANGU ni tafakari zenye maneno machache ya kuhamasisha katika maisha ya kila siku.
Sehemu ya kwanza
👉MAISHA HAYANA FOMULA
Msemo huu humaanisha katika maisha hakuna anayeijua kesho yake na akaweza kuiandaa. Wote tunaishi kwa kubahatisha. Hivyo ni vizuri kuishi kwa kuyatazama malengo madogo madogo na kuyatimiza.
👉MAISHA NI MFANO WA KIOO
Msemo huu humaanisha kwa namna ile unavyo yatazama maisha ndivyo yatavyo kuonesha. Ukifumba macho nayo yanafumba. Ukifumbua nayo yanafumbua. Kumbe katika maisha kila mtu huwa na kioo chake.
👉MAISHA NI KAMA MSHUMAA
Huwa tunaungua tukijitahidi kuwapatia nuru watu wengine. Tunajitoa sadaka ili vizazi vyetu viishi katika furaha. Tunaisha,tunaungua lakini bado hatukati tamaa.
👉MAISHA NI MFANO WA DEBE
Kweli katika maisha usivyokuwa na kitu,utaonekana mropokaji yaani kelele tupu. Kitu kinaweza kuwa elimu,pesa n.k. Jitahidi sana usiwe debe,tafuta ujuzi wako tulia.
👉MAISHA NI MFANO WA UMEME
Hutokea ghafra bila kutegemea,kisha huondoka ghafra bila kutegemea. Msemo huu wa maisha unatukumbusha kuwa watu wa maandalizi wakati wote.
DAVID M MROPE
SUA