Akili mbovu ya vijana wa kizazi hiki kufikiria wakatapa teuzi kwa kusifia viongozi

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Kuna tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.

Katika kitabu kimoja cha uongozi nilikisoma kwa uzuri sana. Kinasema kiongozi mzuri hujipambanua kwa kuwa kweli na kutenga muda kipanga mipango yake ya muda na kusoma na kujielemisha, lakini kizazi hiki hakina hulka ya kujisomea kabisa. Kizazi hiki kimegubijwa na starehe zaidi kuliko kazi na ubunifu.

Uchawa umekuwa mwiba na ajira rasmi ya vijana. Kuna wakati kila mtu anapambana kuwa chawa wa viongozi, kila kujali na kujikita kubuni namna mbalimbli ya uzalishaji mali na kuhudumia jamii.

Hii akili mbovu ya vijana na wasomi itapeleka kuliua Taifa la Tanzania.
 
Kuna Tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao Hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.
Jus' like that 👇👇 nakala imfikie.. cc Lucas mwashamba choiceVariable Faizafoxy covax Lord denning and co
 
Attachments

  • IMG_20221017_200817.jpg
    IMG_20221017_200817.jpg
    103.1 KB · Views: 2
Kuna Tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao Hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.
M|kuu wala usipepese macho, sema; vijana wa ccm a.k.a. machawa bin kunguni.
 
Ndo shida yenu. Tukitumia uhuru wetu kutoa maoni mnadhani tunataka uteuzi. Wengine tuna kipato kikubwa kuliko hiyo mishahara ya vyeo vya uteuzi ndo mana tuko huru kusifia panapofaa na kukosoa pale panapofaa.

Acheni kuishi kwa kukariri
Jus' like that 👇👇 nakala imfikie.. cc Lucas mwashamba choiceVariable Faizafoxy covax Lord denning and co
 
Ndo shida yenu. Tukitumia uhuru wetu kutoa maoni mnadhani tunataka uteuzi. Wengine tuna kipato kikubwa kuliko hiyo mishahara ya vyeo vya uteuzi ndo mana tuko huru kusifia panapofaa na kukosoa pale panapofaa.

Acheni kuishi kwa kukariri
Lord denning acha unafiki!! Mfano issue ya DP world kuna vifungu hata mtoto atajiuliza huu uwekezaji usio na kikomo ni htr lkn wew na genge lako mnashangilia na kusema hakuna tatizo!!👇👇👇
 
Attachments

  • 1687761662681.jpeg
    1687761662681.jpeg
    182.2 KB · Views: 2
Ni miongoni mwa tabia inayochukiza haswa, na mara nyingi ni kusifu tu kwanini hawatoi dosari pia ili kujenga.
 
Lord denning acha unafiki!! Mfano issue ya DP world kuna vifungu hata mtoto atajiuliza huu uwekezaji usio na kikomo ni htr lkn wew na genge lako mnashangilia na kusema hakuna tatizo!!👇👇👇
Sasa ndugu. Inategemea tafsiri na uelewa wa huyo mtu.

Mimi na uanasheria wangu nimesoma mkataba na nimeona hauna mapungufu. Hoja nyingi zinazotolewa ni hofu tu za watu ila haziko katika mkataba kama mkataba as mapungufu ya kimkataba.

Sasa nikisimamia msimamo wangu na mimi nimekuwa chawa?
 
Lucas Mwashambwa ni mfano hai wa vijana wa ovyo kuwahi kutokea hapa nchini
Sawa nashukuru maana najuwa wewe huwa unachuki binafsi na mimi. Kikubwa lazima tufahamu kuwa kutofautiana mitazamo ni jambo la kawaida katika mijadala,na hili hiyo ni hatua njema katika maendeleo ya fikira kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Tunachopaswa kufanya ni kukosoana kwa hoja na siyo matusi au lugha za kudhalilishana na kuvunjiana heshima,.Tuvumiliane katika mijadala na tusilazimishane sisi sote kufanana mitizamo na namna ya kufikiri,tusilazimishane na kutaka kuimba nyimbo sawa kama makasuku
 
Sasa ndugu. Inategemea tafsiri na uelewa wa huyo mtu.

Mimi na uanasheria wangu nimesoma mkataba na nimeona hauna mapungufu. Hoja nyingi zinazotolewa ni hofu tu za watu ila haziko katika mkataba kama mkataba as mapungufu ya kimkataba.

Sasa nikisimamia msimamo wangu na mimi nimekuwa chawa?
Siping maoni yako, but kwel manguli akina Shivji,. Mzee WARIOBA, BUTIKU, LISSU mpaka viongoz wa dini wapo wrong against that facts?
 
Sawa nashukuru maana najuwa wewe huwa unachuki binafsi na mimi. Kikubwa lazima tufahamu kuwa kutofautiana mitazamo ni jambo la kawaida katika mijadala,na hili hiyo ni hatua njema katika maendeleo ya fikira kwa maslahi mapana ya Taifa letu.Tunachopaswa kufanya ni kukosoana kwa hoja na siyo matusi au lugha za kudhalilishana na kuvunjiana heshima,.Tuvumiliane katika mijadala na tusilazimishane sisi sote kufanana mitizamo na namna ya kufikiri,tusilazimishane na kutaka kuimba nyimbo sawa kama makasuku
Hiyo hela waliyotumia wazazi wako kukusomesha bora wangefugia nguruwe tu.
FB_IMG_1690164586210.jpg
 
Wasafi
Clouds fm
Maulidi kitenge cha wask
Stive nyerere
Wasanii wa bongo piano sio fleva ilishakufa.
Wahuni na wezi toka uswasi sasa wanaimba visingeri.
Bongo movie bajeti milioni 2
 
Kuna tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.

Katika kitabu kimoja cha uongozi nilikisoma kwa uzuri sana. Kinasema kiongozi mzuri hujipambanua kwa kuwa kweli na kutenga muda kipanga mipango yake ya muda na kusoma na kujielemisha, lakini kizazi hiki hakina hulka ya kujisomea kabisa. Kizazi hiki kimegubijwa na starehe zaidi kuliko kazi na ubunifu.

Uchawa umekuwa mwiba na ajira rasmi ya vijana. Kuna wakati kila mtu anapambana kuwa chawa wa viongozi, kila kujali na kujikita kubuni namna mbalimbli ya uzalishaji mali na kuhudumia jamii.

Hii akili mbovu ya vijana na wasomi itapeleka kuliua Taifa la Tanzania.
Awamu ya tano wengi walitusua kwa mtindo huu.
 
Ndo shida yenu. Tukitumia uhuru wetu kutoa maoni mnadhani tunataka uteuzi. Wengine tuna kipato kikubwa kuliko hiyo mishahara ya vyeo vya uteuzi ndo mana tuko huru kusifia panapofaa na kukosoa pale panapofaa.

Acheni kuishi kwa kukariri
Kama utakaa kusifia utumbo hufai kuwa kiongozi. Kwenye uongozi Kuna kitu kinaitwa authentic. Hakikisha tena hakikisha tena hakikisha kila mdomo wako unaongea kitu sahihi tena kimefanyiwa utafiti.
 
Sawa nashukuru maana najuwa wewe huwa unachuki binafsi na mimi. Kikubwa lazima tufahamu kuwa kutofautiana mitazamo ni jambo la kawaida katika mijadala,na hili hiyo ni hatua njema katika maendeleo ya fikira kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Tunachopaswa kufanya ni kukosoana kwa hoja na siyo matusi au lugha za kudhalilishana na kuvunjiana heshima,.Tuvumiliane katika mijadala na tusilazimishane sisi sote kufanana mitizamo na namna ya kufikiri,tusilazimishane na kutaka kuimba nyimbo sawa kama makasuku
Tatizo vijana wa ccm wao kuchambua na kuchanganua mambo hawajui!
Hawataki kuhoji, maadam kitu kimetoka wa wakubwa wao kazi yao ni moja tu "NDIO"
Ndio maana nchi imekuwa shamba la bibi, viongozi wanatudharau na kufanya wizi na ufisadi watakavyo!
Badilikeni vijana wa ccm nchi inafilisiwa na wanasiasa wenu! Mtakuja kuwaambia nini vijana wetu? Wake up you idiot
 
Kuna tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.

Katika kitabu kimoja cha uongozi nilikisoma kwa uzuri sana. Kinasema kiongozi mzuri hujipambanua kwa kuwa kweli na kutenga muda kipanga mipango yake ya muda na kusoma na kujielemisha, lakini kizazi hiki hakina hulka ya kujisomea kabisa. Kizazi hiki kimegubijwa na starehe zaidi kuliko kazi na ubunifu.

Uchawa umekuwa mwiba na ajira rasmi ya vijana. Kuna wakati kila mtu anapambana kuwa chawa wa viongozi, kila kujali na kujikita kubuni namna mbalimbli ya uzalishaji mali na kuhudumia jamii.

Hii akili mbovu ya vijana na wasomi itapeleka kuliua Taifa la Tanzania.
Huwa najisikia aibu sana mtu ambaye nyumbani tunamuita baba alafu unamuona kwenye Tv anamsifia mwanaume mwenzake, ni aibu kwa kweli.
 
Kuna tabia ya vijana bila hata kupewa chochote huibuka na kusifia viongozi hata ambavyo hastahili. Hii imekuwa kero kwa baadhi ya viongozi ambao hawana hulka ya kutaka sifa wamekuwa wakijitenga nao.

Katika kitabu kimoja cha uongozi nilikisoma kwa uzuri sana. Kinasema kiongozi mzuri hujipambanua kwa kuwa kweli na kutenga muda kipanga mipango yake ya muda na kusoma na kujielemisha, lakini kizazi hiki hakina hulka ya kujisomea kabisa. Kizazi hiki kimegubijwa na starehe zaidi kuliko kazi na ubunifu.

Uchawa umekuwa mwiba na ajira rasmi ya vijana. Kuna wakati kila mtu anapambana kuwa chawa wa viongozi, kila kujali na kujikita kubuni namna mbalimbli ya uzalishaji mali na kuhudumia jamii.

Hii akili mbovu ya vijana na wasomi itapeleka kuliua Taifa la Tanzania.
WAO NI KURAMBA VIATU VYA VIONGOZI UJINGA MTUPU
 
Back
Top Bottom