Akawaambia, “Nawaachia mumshughulikie…..!”

Akawaambia, “Nawaachia mumshughulikie…..!”

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,441
IMG_3595.jpg


Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 1987. Nilikuwa ninaishi na kaka yangu mkoani Arusha. Ni mwaka huo ndipo kaka yangu alipohamishiwa mkoani Tanga. Tulipofika Tanga tulipata nyumba maeneo ya Kisosora.

Nyumba hii ilikuwa na pande mbili. Upande mmoja alikuwa anaishi mwenye nyumba na familia yake na upande mwingine ndio huo tuliopanga sisi. Nilikuwa nimetafutiwa kibarua cha muda katika kiwanda cha kutengeneza saruji nikisubiri kufanyiwa mipango ya kuendelea na chuo. Kwa kazi yangu hiyo nilikuwa naondoka nyumbani asubuhi na kurejea usiku saa nne au tano usiku.

Nyumba hiyo ilijengwa kwa njia ambayo mtu akiwa upande mmoja wa nyumba anaona upande wa pili. Yaani mimi nikiwa uani kwetu naona kile kinachoendelea uani kwa mwenye nyumba wetu. Kwa hiyo ilikuwa rahisi kuwajua vizuri wanaoishi mle ndani, pamoja na kurudi kwangu usiku karibu kila siku.

Nilikuwa nawaona asubuhi kila siku na hata usiku, nikikuta hawajalala bado. Kati ya wale waliokuwa wakiishi kwenye familia ile, kulikuwa na binti mmoja mzuri sana. Huyu binti alionekana mtu wa dini sana kwa mavazi na hata salimia yake. Nikiwa uani kwetu, nilikuwa naweza kusalimia au kusalimiwa, kwani ua ulitengwa kwa ‘fence' ya waya tu.

Nilikuwa na kawaida ya kumsalimia zaidi yule binti kuliko wengine na nilimtamani sana kwa kweli. Siku moja ibilisi alinituma nimwandikie barua ya mapenzi na asubuhi moja nikampatia barua hiyo kupitia kwenye fence.

Alipoipokea aliificha haraka, nikajua ametamani kitendo kile. Mle kwenye barua nilimwomba tukutane kwenye Hoteli moja ambayo ilikuwa na vyumba vya kulala wageni siku ya Jumamosi ambayo mwenye nyumba, ambaye nilikuwa sijafahamu ni nani kwake, huwa anasafiri kwa shughuli zake kwenda Muheza. Nilimwandikia kwamba nimempenda sana.

Kesho yake ambayo ilikuwa ni Ijumaa, mwenye nyumba aliniita asubuhi kabla sijaenda kazini. Nakumbuka siku hiyo kaka yangu alikuwa amesafiri kwenda Arusha kuiona familia yake ambayo bado ilikuwa imebaki Arusha akifanya mipango ya uhamisho wa mkewe aliyekuwa mwalimu na watoto ambao ndio kwanza walikuwa wanasoma elimu ya msingi.

Nilishangazwa na kushtushwa na wito ule nikajua labda bomu limelipuka. Nilipoenda alinitambulisha kwa yule binti kuwa ni mkewe mdogo. "Siku mlipohamia hapa wewe na kaka yako hakuwepo kwa hiyo nimependa tu umfahamu, msije mkapigana vikumbo huko mitaani." Alisema.

Akili yangu bado ilikuwa kwenye mwili, sikutaka kutafakari hata kidogo. Niliporudi kutoka kazini usiku nilimkuta yule binti akiwa uani peke yake, nilimsalimia kisha nikamkumbusha ile ahadi yetu. Alishtuka kidogo, kisha akaniuliza, "lakini si unajua mimi ni nani kwa huyu Mzee mwenye nyumba."

"Ndio najua, kwani kuna tatizo gani, mie kijana mwenzio unadhani nitakuwa sawa na huyo mzee wako ambaye ameshajichokea?" Nilimjibu huku nikijifaragua….. Yule binti hakujibu kitu aliguna tu. Ili kujihakikishia kama ndege kaingia mtegoni au bado, nilimuuliza kama tumeelewana, na yeye bila kumung'unya maneno alijibu kuwa ameelewa……….

Kweli kesho yake ulipofika muda wa saa nne asubuhi nikafika kwenye ile Hoteli. Ile kukanyaga tu ndani ya ile Hoteli mtu mmoja ambaye alivaa kama mhudumu aliniuliza kama mie ndiye fulani. Nilimjibu kuwa ndiye mie. yule mhudumu alinijuza kwamba bi fulani ananisubiri chumba namba 12. Kwanza nilishtuka kwamba, kwa nini yeye ndiye achukue chumba, lakini nikajiambia, labda ni kwa sababu ni mke wa mtu hakutaka watu wajue kama yuko pale.

Nilimuomba yule mhudumu anielekeze kilipo hicho chumba na yeye bila kusita alinipeleka na kunionyesha kisha akaondoka. Ibilisi wa ngono alishanivaa na mwili ulishajiandaa kwa jambo hilo na nilikuwa na furaha ya ajabu kwamba sasa naonja ladha ya binti wa ki Tanga, ladha adhimu inayosifika ukanda huu wa pwani. Niliusogelea mlango na kugonga. Mlango ulifunguliwa. Macho yangu yaligongana na ya yule msichana.

Kwa tamaa yangu nilikwenda moja kwa moja nikitaka kumvamia na kumbusu, lakini alinikwepa, mara ghafla mlango wa chumba ulifunguliwa. mbele yangu alikuwa yule mhudumu aliyenielekeza kilipo kile chumba, mzee mwenye nyumba yetu na minjemba miwili iliyoshiba. Yule mzee mwenye nyumba alimshika mkewe na kusema, "Nawaachia huyu kijana mumshughulikie, hebu twen zetu mke wangu."

Yule msichana alinitizama juu hadi chini na kuniambia kwa kunong'ona, "nyama wee, miye siyo Malaya." Alitoka na mumewe akiniacha nikiwa nimeduwaa. Nilipowatizama wale manjemba wawili, niliwaona wakivua fulana zao, nikajua ngondo igwa…., ‘Hapa sitopona.' Nilijisemea moyoni. Akili yangu ilifanya kazi haraka na kwa kasi ya umeme nilimrukia kichwa njema mmoja aliyesimama mlangoni tukaangukia nje, ni bahati mlango ulikuwa haujafungwa.

Niliponyanyuka sikusimama, break ya kwanza ilikuwa ni kituo cha mabasi yaendayo mikoani, nikapanda basi na kuja Dar. Kuanzia siku hiyo mtu akiniambia twende Tanga natamani nimdunde. Sijakanyaga mji ule hadi leo……………..

Salaam hizi zimfikie Babu DC Dark City, hii ndio sababu ya kukataa mwaliko wako wa kuja huko Tanga mwaka jana………….. LOL
 
Aiseeee pole sana bwana mtambuzi ilibaki kidogo uwe asusa ya majamaa.
 
Haaa! Mtambuzi,,
Nenda tu Tanga,wa pale Chumbageni hawatakuitia mume!
Du,,uaminifu wa ndoa wa aina hii,,unabaki katika simulizi
 
Last edited by a moderator:
Mbona umemaliza story fasta..!!? una uhakika hujasahau kitu mzee mwenzangu Mtambuzi...!?? hebu kumbuka vizuri afu uje tena
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom