Akamatwa akiuza kichwa cha mke wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Akamatwa akiuza kichwa cha mke wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Mar 19, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Akamatwa akiuza kichwa cha mke wake


  na Ali Lityawi, Kahama


  [​IMG] JESHI la Polisi wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga linamshikilia kijana Tano Sita Katinda mkazi wa kijiji cha Mwamala wilayani Nzega mkoani Tabora aliyekamatwa akiuza kichwa cha mke wake pamoja na viungo vingine vikiwemo matiti mawili na sehemu za siri!
  Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Diwani Athuman, alisema Katinda alikamatwa na polisi katika eneo la benki ya CRDB tawi la Kahama akitaka kuwauzia viungo hivyo polisi waliokuwa kwenye lindo.
  Kwa mujibu wa kamanda huyo, Katinda alikamatwa jana majira ya saa 3.00 asubuhi baada ya kufika katika benki hiyo akidai anauza nyama ya nguruwe iliyokuwa kwenye mfuko wa sandalusi hali ambayo kila mtu aliyekuwa katika eneo hilo kubaki kushuhudia kilichokuwa kikiendelea.
  Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kufika hapo askari aliyekuwa kwenye lindo pamoja na wenzie baada ya kuiangalia nyama hiyo iliyodaiwa kuwa ni ya nguruwe cha ajabu waliona kichwa cha binadamu kikiwa pamoja na viungo hivyo na ndipo walipomweka chini ya ulinzi.
  Kwa mujibu wa kamanda huyo wa polisi, awali kijana huyo alionekana kwenye eneo la stendi ya mabasi maeneo ya CCM Kahama akiuza viungo hivyo ndipo alipoelekezwa kwenda kuuza kwa maaskari waliokuwa katika lindo la benki za CRDB na NMB huku watu hao wasijue kijana huyo amebeba nini katika furushi lake.
  Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kufika benki ya NMB aliwaambia maaskari hao kuwa anauza kitimoto lakini walimjibu kuwa wao ni Waislamu hawaitumii nyama hiyo huku wakimwelekeza kwenda kwa askari waliokuwa wakilinda benki ya CRDB ndipo alipokamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi cha wilaya.
  Alisema kijana huyo baada ya kukamatwa alikiri kuwa viungo hivyo vilikuwa ni vya mke wake aliyemtaja kwa jina la Kabula Luziga (18) mkazi wa Itobo, wilayani Nzega.
  Baada ya kijana huyo kuulizwa, alisema alimuua mkewe usiku kwa kutumia panga baada ya kumvizia akiwa amelala huku kiwiliwili cha mwili wa marehemu Luziga akikiacha katika chumba chake nyumbani kwa Babu yake aliyemtaja kwa jina moja la Mwanandilila huko katika kijiji cha Mwamala wilayani Nzega, mkoani Tabora.
  Kamanda alisema baada ya kumhoji kijana huyo alidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kusikia matangazo kwenye redio moja ya mjini Kahama kuwa viungo hivyo vinahitajiwa na kuna wateja wa kununua ndipo alipoamua kumuua mkewe.
  Athuman alisema jeshi lake linaendelea na upelelezi ikiwa ni pamoja na kumchunguza kijana huyo kuona kama akili yake iko sawa na jana mchana kikosi cha maaskari polisi kiliondoka kuelekea Mwamala wilayani Nzega kuona kiwiliwili cha marehemu Luziga.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  ushirikina ndiyo unaotuletea umasikini wa kutupwa................................kila aaminiye kwenye ushirikina anajithibitishia yeye mwenyewe ya kuwa hamjui Mwenyezi Mungu.....................................................
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Lakini mimi nina mashaka na akili ya mtuhumiwa, huenda akawa na matatizo ya kiakili.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Bhange!X3
  Chunga sana mwanao asije kutumbukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya!
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Mar 19, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Atakuwa na matatizo ya akili huyo!
   
 6. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #6
  Mar 19, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli kabisa!
   
 7. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #7
  Mar 19, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Duh! Poleni sana Watanzania, hii hasimuliki kabisa.
   
 8. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #8
  Mar 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Akili ya huyu kijana inatakiwa ichunguzwe sawa sawa maana katika hali ya kawaida asingekuwa anatembeza kichwa hicho kama karanga hadi kwa askali polisi bila kuhofia kukamatwa. Amepita na kichwa na viungo vingine sehmu nyingi sana ambazo kwa mtu mwenye akili ya kawaida kabisa asingediriki kupita huku akinadi eti anauza kitimoto. Poleni sana ndugu wa Kabula Luziga kwa kumpoteza mpendwa wenu. Sina uhakika kama mlikubali kumruhusu mtoto wenu aolewe na kijana huyo mkiwa mnajua kuwa hana akili zilizo sawa au hakuwa hivyo wakati mnaruhusu hayo au ni binti yenu ndo aliyependa.
   
 9. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 20, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Sawa sawa kabisa, maelezo yaliyotolewa yanabainisha kabisa kuwa kijana huyo ni mgonjwa wa akili:
  1. Alisikia matangazo redioni kuwa viungo hivyo vinauzwa (Hallucinations)
  2. Alikwenda kuwauzia polisi viungo vya binadamu ( lack of insight)
  3. Aliamini kuwa aliyosikia redioni ni sahihi (delusion)
  lakini kwa ujinga tuliyorithishwa kwa kunyimwa elimu bora na CCM, bado mamillioni yetu tutaamini kuwa alikuwa mchawi!!!!
   
 10. c

  chetuntu R I P

  #10
  Mar 20, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyo kijana alikuwa na akili timamu kabisa, baada ya kufanya mauaji akapata kichaa cha muda. Mauaji ya wanawake hayataisha huku, ushirikina ni mwingi sana. Mtu ana mang'ombe kibao kumbe kazika viungo vya binadam katikati ya zizi. Wanatumia kupata utajiri.
   
 11. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #11
  Mar 20, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  dah! Mungu amlaze Marehemui pema pepon, Amin, mm anhis kijana huyu ana matatizo ya akil maana katika mazingira ambayo huyu kamanda wa polis anayazungumzia ni dhahiri mtuhumiwa angekuwa na akil timamu asingeenda kwa askari kumuuzia huo furushi aliliokuwa amebeba
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2011
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  kama nimeisoma vizuri wakati mtuhumiwa akitoa sababu ' kwamba alisikia redioni kuwa kuna hitajiko la viungo hivyo' sasa ni redio gani inaweza kutangaza uchizi huo
   
Loading...