Ajitapa kutengua ndoa ya bosi wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajitapa kutengua ndoa ya bosi wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by kilimasera, Apr 15, 2011.

1. kilimasera

kilimasera JF-Expert Member

#1
Apr 15, 2011
Joined: Dec 2, 2009
Messages: 3,073
Likes Received: 17
Trophy Points: 135
MSICHANA Jacklin [24] mkazi wa Kinondoni jijini Dar es Salaam amejitokeza na kutoa ushuhuda mbele ya wanawake kwa kujisifia kuvunja ndoa ya bosi wake kwa kujiita ni mwanamke wa kuigwa katika jamii.
Hayo aliyasema katika hafla fupi ya kumfunda mwali wa kike maarufu kama “Kitchen Party” iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita huko maeneo ya Kibaha mkoani Pwani.

Msichana huyo alitoa ushuhuda huo kwa kuwafundisha wanawake waliokuwa na tabia ya kuwaachia kila kitu wasichana wao wa kazi na hivyo kujenga tabia ya kutozishughulikia nyumba zao.

Akitoa mada aliyoiita "mwanamke bora" alifafanua neno hilo na kujipa mfano yeye mwenyewe alivyokuwa bora katika familia ya mume wake wakati alipokuwa akifanya kazi za ndani kabla hajaweza kuolewa na mwanaume huyo.

Alisema kuwa” jamani wanawake wenzangu tujitahidi kuangalia nyumba zetu sio tunawaachia wasichana wa kazi kila kitu hiyo ni hasara jamani, unaweza ukahatarisha ndoa yako”

“Mimi nilikuwa msichana wa kazi za ndani miaka miwili iliyopita bosi wangu wa kike alikuwa hashughuliki na nyumba yake kabisa na kuniachia kila kitu mimi na yeye ilikuwa kila kukicha anakwenda kwenye shughuli zake na akitoka anaranda na huwa anarudi usiku na wala alikuwa hana hata muda wa kumungalia mume wake na hata mtoto wake alikuwa hamshuhulikii".

Aliendelea kwa kusema kuwa tabia hiyo ilimchosha mume wa mwanamke huyo ambaye alikuwa sio msemaji na kila anapomkanya alikuwa hamsikii kabisa.

Mume wa mwanamke huyo alichoshwa na vitendo vya mke wake vya kutokumjali hata hajui mke wake kama anajua kupika ama la kwa kuwa alikuwa hashughuliki na mapishi.

"Hivyo mume huyo alinitaka mimi niondoke kwa muda kwa kuwa mke wake alikuwa hajishughulishi kwa kuona alikuwa na msaidizi".

Katika hali hiyo mwanamke huyo hakukubaliana na kitendo cha kumuondoa msichana huyo na kumwambia mtoto angepata shida na kumtaka msichana huyo asiondoke

Hali hiyo iliendelea na baadae baba huyo alidai alimtaka kumuoa msichana huyo kwa kuona kuvutia na utendaji wake kazi lakini msichana huyo alidai hakuafiki kabisa kwa kumlindia heshima bosi wake wa kike.

Hata hivyo mwanaume alimlazimisha amuoe na alituma washenga nyumbani kwa msichana huyo kwa lengo la kumuoa bila ya mke wake kujua na hatimaye alipomaliza hatua za awali alimtaka msichana huyo amuage mke wake kuwa anahitajika nyumbani kwao mkoani Morogoro kwa muda wa siku mbili ili akamuoe.

Hata hivyo bosi wake hakufahamu hilo alimruhusu na kumsihi asizidishe siku tatu arudi na alipoenda kwao alienda kuolewa na mume wa mwanamke huyo na aliporudi alimtambulisha mke wake kuwa kuanzia sasa msichana huyo ni mke mwenzake.

Ndipo mwanamke huyo alianza vurugu za hapa na pale akimtaka mume wake ampe talaka ili ampishe aweze kuishi na msichana huyo.

Na hatimaye mwanamke huyo alidai talaka kinguvu na aliweza kuondoka nyumbani hapo.

‘Jamani tutunze nyumba zetu, tuwatunze waume zetu, tutunze watoto wetu na si kuwaachia wasichana wa kazi kila kitu mtavunja nyumba zetu’ alimalizia msichana huyo

Hata hivyo baadhi ya wanawake ukumbini hapo walivutiwa na msichana huyo huku wengine wakiwa wanamlaani kwa kitendo chake cha kuvunja ndoa ya mwanamke mwenzake bila hata huruma.

2. Lambardi

Lambardi JF-Expert Member

#2
Apr 15, 2011
Joined: Feb 7, 2008
Messages: 10,313
Likes Received: 5,605
Trophy Points: 280
Mmmmmmmm kazi ipoo!!!mbona hatari sana??

3. kilimasera

kilimasera JF-Expert Member

#3
Apr 15, 2011
Joined: Dec 2, 2009
Messages: 3,073
Likes Received: 17
Trophy Points: 135
ndio hivyo yanatokea hayo!

4. M

Mary Glory Senior Member

#4
Apr 15, 2011
Joined: Mar 20, 2011
Messages: 126
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
hili nalo ni la kujisifia kweli????i think huyo mwanamke anakosea sana.

5. NATA

NATA JF-Expert Member

#5
Apr 15, 2011
Joined: May 10, 2007
Messages: 4,516
Likes Received: 16
Trophy Points: 135
Hajakosea kama nyie waume zenu mnawadharau na kuwaona wakaida kuna watu wanawatamani.

kuna rafiki yangu pia anafanya kampuni ya kigeni ametamba kumchukua mke wa boss yake pia na kumlewesha maloves upo hapo.
MMME WA HUYU DEMU MALAYA MNO! \
NA NI WANCHI JIRANI

6. Msarendo

Msarendo JF-Expert Member

#6
Apr 15, 2011
Joined: Jan 29, 2011
Messages: 9,135
Likes Received: 3,327
Trophy Points: 280
Duuh! Kazi ipo hapo.

7. m

mbongopopo JF-Expert Member

#7
Apr 15, 2011
Joined: Jan 24, 2008
Messages: 1,112
Likes Received: 9
Trophy Points: 135
Lakini hii ni kweli wanawake wengi esp wasichana wa enzi hizi wanajisahau na kujali pesa na kazi zao na ndio majibu haya yanatokea

Ila mwanaume nae bomu alijishushaaaaaa nae lazima atafanyiziwa kwani kalazimisha ndoa kukomoa mkewe

Wengine wanajuta as wanaruka mkojo kukanyaga mavi

8. Babu Lao

Babu Lao JF-Expert Member

#8
Apr 15, 2011
Joined: Nov 2, 2010
Messages: 2,056
Likes Received: 9
Trophy Points: 135
Hakuna hatari yoyote mpendwa.... mwenye mali alizubaa mjanja kakwapua ha ha haaaa safi sana!!!:lol:

9. Likasu

Likasu JF-Expert Member

#9
Apr 15, 2011
Joined: Jan 18, 2011
Messages: 694
Likes Received: 94
Trophy Points: 45
Leo mmeamua kutumwagia ya kwenye vyi kitchen party, haya leteni mambo, na zile habari za kinu je !!?

10. bacha

bacha JF-Expert Member

#10
Apr 15, 2011
Joined: Aug 19, 2010
Messages: 4,336
Likes Received: 4
Trophy Points: 135

bora wewe umeliona hili!!!!!!!

11. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#11
Apr 15, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Kaazi kweli kweli!Mlioolewa fanyeni kazi msije mkaibiwa na nyie!

12. Mbu

Mbu JF-Expert Member

#12
Apr 15, 2011
Joined: Jan 11, 2007
Messages: 12,729
Likes Received: 187
Trophy Points: 160
...mpaka sasa najifikiria nimsifu huyu dada, au nimdharau.
Yataka moyo mwanamke kutoa ushuhuda wa namna hiyo mjue?
...tena kwenye kitchen party! duhh,...ndoa hizi!

13. M

Mkare JF-Expert Member

#13
Apr 15, 2011
Joined: Dec 21, 2010
Messages: 495
Likes Received: 0
Trophy Points: 0
Ila kuna ambao wanafanya kila kitu mpaka hata wanabeba waume zao migongoni na kwenda kuwaogesha na bado wanalizwa... Haya mambo hayana formula kabisa. Ni kuomba Mungu tu

14. Mpui Lyazumbi

Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

#14
Apr 15, 2011
Joined: Sep 1, 2010
Messages: 1,853
Likes Received: 146
Trophy Points: 160
Ni nini maana ya ndoa?

15. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#15
Apr 15, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Well kwa kesi kama hii ni mtu kutumia nafasi yake kama mke ipasavyo.

16. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#16
Apr 15, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,508
Likes Received: 2,249
Trophy Points: 280

mkare,weeh hujui hata kwenye mpira watazamaji wanajua kuliko kocha na wachezaji?mzigo wa mwenzio kanda la sufu!
lizzy mamii,nakuombea kwa Mungu,akupe mume mzuri tena wa chaguo lako.umtunze vizuri baada ya miaka 10 uje na ushuhuda humu jinsi ulivyodhibiti wadokozi na vibaka eeh.

17. C

Caroline Danzi JF-Expert Member

#17
Apr 15, 2011
Joined: Dec 19, 2008
Messages: 3,629
Likes Received: 56
Trophy Points: 145
Narudia kusema "UAMINIFU" ni ndiyo nguzo ya ndoa na mapenzi kwa ujumla. Unajua kama hakuna uaminifu hakuna upendo, kukiwa na upendo bila uaminifu hakuna kitu. Nahisi tu huyu kiumbe akiwa siyo mwaminifu hata ungekuwa unafanya malovee kuliko makungwi atatoka nje kwenye kutafuta wale wasiojua.

Mapenzi ni Uamiinifu siyo vinginevyo. Kweli kuna kipindi wanawake tunajisahau sana, imagine mume anarudi nyumbani mapema akijua mke upo walau umpe chai ya jioni, wewe umo kwenye mihagaiko ya umbeya na biashara zisizo na uelekeo. Sasa yule HG yeye yupo kufanya kila kitu, ukiomba chai iko tayari, maji ya kuoga yako tayari, hivi kweli wewe mwanamke ingetokea house boy akafanya mambo kuliko mumeo si ungeelekeza majeshi huko.

Wadada badilika sana tuwape heshima waume zetu, hata kama si wazuri kama tunavyofikiri.

Ndiyo maoni yangu leo. Lets cross fingers and pray tuwe fair yale tusiyoweza kuvumilia tukifanyiwa basi tusifanye instead tufanye yale yanakubalika kiroho.

18. Lizzy

Lizzy JF-Expert Member

#18
Apr 15, 2011
Joined: May 25, 2009
Messages: 22,224
Likes Received: 244
Trophy Points: 160
Hahahaha asante mpendwa kwa kunitakia hayo yote!Too bad sitaki mume... ningeweza kubahatika kweli kweli!

19. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#19
Apr 15, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,508
Likes Received: 2,249
Trophy Points: 280

jamani,wakati nimemuambia kakangu aingie jf ili akuanzie mbio?kuna siku ulikuwa unasema unataka wa kukubadilisha jina utumie lake,nikakuweka kwenye maombi na kumstua kakangu.i take u very serious bana,ngoja nimuambie akung'ang'anie,pm 12 kwa siku.

20. King'asti

King'asti JF-Expert Member

#20
Apr 15, 2011
Joined: Nov 26, 2009
Messages: 27,508
Likes Received: 2,249
Trophy Points: 280

Loading...