Ajirusha mbele ya lori baada ya kusalitiwa kimapenzj

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Jamaa mmoja mjini Naivasha nchini Kenya amejitoa uhai baada ya kugundua kuwa mpenzi wake alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na rafiki yake wa karibu.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo, Samuel Kimani, jamaa huyo aliruka mbele ya lori lililokuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Nairobi siku ya Ijumaa.

Taarifa za The Standard Ijumaa Februari 22,2019 zinaeleza kuwa jamaa huyo aliacha kijikaratasi kwenye mfuko wake ambapo alikuwa ameelezea sababu yake kujitoa uhai ambapo alimlaumu mpenzi wake kwa kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao wa kimapenzi.

Alidai kuwa aliamua kuchukua hatua hiyo baada ya mpenzi wake waliopanga kufunga ndoa kwa pamoja kumsaliti kwa kushiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu.

"Alielezea kwenye kijikaratasi hicho jinsi alivyokutana na mpenzi wake na wawili hao walikuwa wanapanga kufunga pingu za maisha hivi karibu ila alimpata mpenziwe akishiriki mapenzi na rafiki wake wa karibu," Kimani alisema.

" Marehemu aliwaonya wawili hao dhidi ya kuhudhuria mazishi yake kwani ni wao walimpelekea yeye kujitoa uhai," Kimani aliongezea.

Afisa mkuu wa Naivasha Samuel Waweru alithibitisha kisa hicho na kusema mwili wa mwendazake ulipelekwa katika chumba cha kihifadhi wafu cha hospitali ya kata ndogo ya Naivasha.

Malunde
 
there were so many fish in the sea besides her why committing suicide instead of looking for another ?
 
This generation though. Full of people who are mentally & emotionally weak. Mtu anajiua coz ya mapenzi duh! Inasemekana kuwa wanaume ni stronger than women kumbe ni .
 
This generation though. Full of people who are mentally & emotionally weak. Mtu anajiua coz ya mapenzi duh! Inasemekana kuwa wanaume ni stronger than women kumbe ni .

Wanaume gani!!!hao wa kikenya mnaojipigia makwenzi.

Angalia haka maskini,kameshindwa hata kukutafuta wewe
 
Back
Top Bottom