Serikali imeshatamka kuwa waalimu wa arts wameshatosha ma hakuna upungufu tena, sasa mnataka muajiriwe ili muende mkafanye nini mashuleni??. Shule nyingi hivi sasa ukizitembelea unakuta kuna waalimu wanaofundisha kiingereza na kiswahili 20. Shule ina jumla ya wanafunzi 300, hiyo ni form 1 mpaka 4. Sasa katika hali kama hii kuendelea kuajiri si ni kulitwisha taifa mzigo usiokuwa na tija.
Waalimu wala msilalamike sana, tatizo la ajira hapa nchini lipo siku zote, kaeni mtafakari, ondoeni ile mentality mliyoondoka nayo vyuoni ya kusubiri kupangiwa kituo cha kazi, amkeni kwenye huo usingizi wa pono mliolala, muanze kufanya shughuli za kujitegemea kama vijana wanaomaliza taaluma nyingine. Vinginevyo mtaendelea kusubiri kitu ambacho hakipo na kujikuta mnapoteza muda mwingi ambao mngeutumia katika kujikwamua kiuchumi.