Ajira za Ualimu 2015/2016 zinatoka lini?

Ajira za Ualimu 2015/2016 zinatoka lini?

Status
Not open for further replies.
Rais Jakaya Kikwete leo amezindua Sera
ya mpya ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 ambapo kwa mujibu wa
sera hiyo, pamoja na mabadiliko
mengine miaka ya kupata elimu ya awali
imepunguzwa kutoka miaka miwili hadi
mwaka mmoja.
Sera hiyo pia inapunguza umri wa
kuanza darasa la kwanza kuwa miaka
mitano badala ya miaka saba na
muundo wa elimu utakuwa ni
1+6+4+2+3+ badala ya 2+7+4+2+3+ ili
mhitimu amalize mzunguko wa masomo
kwa muda mfupi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo
uliofanyika katika shule ya sekondari
Maji ya Chai iliyoko Kiwalani jijini Dar
es salaam, Rais Kikwete amesema kuwa
lengo kuu la sera hiyo ni kuifanya
Tanzania ifikie lengo lake la kuwa Taifa
lenye uchumi wa kati ifikapo mwaka
2025.
Rais Kikwete amesema kukua kwa
uchumi na ongezeko la watu nchini
kumezua changamoto nyingi, hivyo ni
lazima elimu inayotolewa ikidhi
matatakwa ya mabadiliko huku akiitaka
wizara ya elimu kuwa na utaratibu wa
kitabu kimoja cha kufundishia kwa kila
somo nchi nzima.
Amesema kwamba utaratibu unaotumika
sasa kila shule kuwa na kitabu chake cha
kufundishia ni chanzo kikuu cha watoto
kufeli.
Rais Kikwete pia amezindua maabara za
shule za sekondari kitaifa ambapo
amesema katika kutambua umuhimu wa
elimu nchini bajeti ya wizara ya elimu
imeongezeka kwa asilimia 20.
Akizindua maabara kitaifa Rais Kikwete
amewataka viongozi ambao
hawajakamilisha ujenzi wa maabara
katika maeneo yao kuongeza juhudi
kwani kipindi cha miezi sita
alichoongeza kitaisha akiwa madarakani
hivyo hatasita kuchukuwa hatua ikiwa
ni pamoja na kuwafukuza kazi au
kutengua uteuzi.
Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi
Mh Shukuru Kawambwa amesema lengo
la kuanzisha sera hiyo ni kuhakikisha
watoto wa kitanzania wote wanapata
elimu bila ubaguzi na kwamba sera
imebainisha maeneo ambayo serikali na
wadau watayawekea mkazo zaidi ili
kutoa elimu bora.
Akitoa taarifa ya ujenzi wa maabara za
shule za sekondari mkoani Dar es
Salaam mkuu wa mkoa huo Bw Said
Mecky Sadick amesema maabara 281
zenye thamani ya shilingi bilioni 10.9
zimejengwa huku mkuu wa wilaya ya
Ilala akitoa taarifa ya ujenzi wa
maabara ya kisasa iliyotumika kuzindua
maabara zote nchini.
 
Haya hapo kuna mahali kumeandikwa kwamba Raisi ataajiri walimu 32 elfu?

tuache kutunga mambo bila ushahidi coz tunapotosha umma
 
Kawa-Mbwa kakata mzizi wa fitina. Walimu wa arts wapo wengi mpaka wa ziada. Mf katoa shule za Tabora manispaaa.


source ITV tz habari tar 13/02/2015. 20:05

unachokisema una uhakika nacho?? maana mm ni mkazi wa tabora manispaa...na hali ya huku tabora naifahamu vzr sana
 
Kama halikuzungumzwa tena waziri husika alikuwa on the spot manake mwaka huu ni ha.....
 
Kawa-Mbwa kakata mzizi wa fitina. Walimu wa arts wapo wengi mpaka wa ziada. Mf katoa shule za Tabora manispaaa.


source ITV tz habari tar 13/02/2015. 20:05

kutoa mfano eti shule ya tabora ina wanafunzi sitini na walimu 20 je tabora ndio inameza tanzania yote?
wewe na kawambwa wako fanyeni utafiti tena kwa kuingia huko mikoa mingine ndio utajua walimu wametosha au bado.
 
lusungo kwa hiyo tuwe na uhakika wa ajira?? dah kuna ndugu yangu yy nfo kwanza yupo mwaka wa pili education...sijui itakuaje huko mbele

huyo hawezi kupata kabisa mana ajira za awamu ya mwisho ndio hizi tu zenye vibali 32elfu. Mtafutie biashara mapemaaa japo wanafundishwa stadi za kazi mavyuoni.
 
Nimeanza ufugaji wa kuku wa kienyeji, bado sija survey soko la kuku wa kienyeji likoje.

Kama kuna mtu mwenye uzoefu na hili anishauri, pros and cons etc.

By the way, nimeanza na Jogoo mmoja, ila natarajia kuongeza kuku within a week, projections ni kuwa na kuku 1,000, hapo ndio nianze kuuza, matarajio yangu ni kuuza via interent - hapa nalenga watu wa DAR, ambao wako bize, I can do delivery maofisini within city center, na baadae kuweka vituo vya kufanya pickup wakati watu wanarudi home jioni, e.g Mwenge Junction, Morocco Petrol Station, etc. Malipo via M-Pesa, SMS banking pia na mahoteli.

Sitarajii faida ya haraka, naomba ushauri kwa wale walifanya biashara hii, au wanajua mtu wa karibu aliyeifanya.
 
Mambo ya ufugaji peleka idara ya kilimo humu ni maswala ya ajira kwanza serikalini kwanza unazidi kutuzinguaaaaa KASIGAZI
 
Dar yani umeniboaaa sana wewe unaleta biashara zako kwenye maswala muhimu haswa ktk kipindi kigumu kama hiki?

hakika ningekua karibu yako ningekufanya kitu kibaya
 
Dar yani umeniboaaa sana wewe unaleta biashara zako kwenye maswala muhimu haswa ktk kipindi kigumu kama hiki?

hakika ningekua karibu yako ningekufanya kitu kibaya

Nilikuwa nakupa mbinu za kujiajiri, ajira hakuna mwaka huu, huo ndo ukweli
 
Nani kakudanganya kuwa ajira hakuna?

Wewe ndo afisa habari wa wizara ya elimu?
kama ajira hamna siwangesema wakubwa wenyewe?
acha kuvunja watu moyo
 
waziri kasema tatzo LA walimu lipo ila litafanyiwa ufumbuzi ilikukizi mahtaj ya Sera ya elimu.ila tatzo kubwa ni walimu wa sayansi..hii hakumaanisha kuwa walimu wa arts wanatosha'''''';""""""*****hivyo kasema baada ya miaka3 tatzo LA upungufu wa walimu litakuwa limekwisha In sh a all ah 99% hivyo ajra zpo wadau Ln ztatoka. rediio viuno znakisia mwez huu
 
SERIKALI imetangaza kuwa itaanza kutoa elimu ya sekondari bure kuanzia Januari 2016, ili kila Mtanzania awe na elimu ya kidato cha nne katika miaka ijayo.
Imesema sambamba na kutoa elimu ya sekondari bure, sera mpya ya elimu na mafunzo inaelekeza utaratibu wa kupanga ada kwa shule binafsi ili kupunguza malalamiko ya wazazi ya kulipa fedha nyingi kwa elimu za awali.
Uamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Rais Jakaya Kikwete, wakati akizinduzi Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, ambayo ni matokeo ya kuhuishwa na hatimaye kufutwa kwa Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996, Sera ya Taifa ya Elimu ya Juu ya mwaka 1999 na Sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa Elimu ya Msingi ya Mwaka 2007.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika katika Shule ya Msingi Majani ya Chai iliyopo Kipawa, Rais Kikwete alisema sera hiyo ni mwanzo wa nguvu mpya ya kuendeleza elimu kitaifa na kimataifa, hivyo lazima iwe kielelezo cha utashi wa kupanga mikakati ya kuinua elimu nchini.
Alisema ukombozi wa elimu ni nyenzo ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati, hivyo ni jambo la lazima kuhakikisha kila mtoto anapata elimu ya kidato cha nne.
“Baada ya uzinduzi huu, kuanzia mwaka ujao tunataka kuondoa ada za shule za sekondari ili mtoto anayeanza asilipe Sh 10,000 wala Sh 20,000, ili miaka saba ijayo tuhakikishe kila mtu ana uwezo wa kufika form four (kidato cha nne), lengo tufike mahali elimu ya msingi iishie kidato cha nne,” alisema Rais Kikwete.
Alisema ili kukamilisha mpango huo, shule za msingi nchini zinapaswa kujiandaa kujenga shule za sekondari na wenye dhamana ya utekelezaji wa kazi hiyo wahakikishe kila mtoto anapata elimu ya awali kabla ya kujiunga na shule ya msingi.
“Lengo ifikapo mwaka 2025 Tanzania iwe nchi ya kipato cha kati, pato la wastani liwe dola 3,000, kwa sasa tupo katika dola 977, naamini miaka kumi ijayo tutafikia hapo kwa sababu ya mabadiliko na zana ambazo zitahitajika katika elimu, hakuna maendeleo bila elimu,” alisema Rais Kikwete.
Ada shule za binafsi na mitaala
Akizungumzia ada zinazotozwa na shule binafsi, Rais Kikwete alisema sera mpya ya Elimu na Mafunzo inasisitiza elimu ni huduma, hivyo utaratibu wa kupanga ada kwa shule binafsi ni lazima uzingatiwe ili kupunguza malalamiko ya wazazi kulipa fedha nyingi kwa watoto wa elimu za awali.
“Zipo kindergarten (shule za awali) zinatoza ada kubwa kushinda chuo kikuu, mtu mtoto anakwenda kuchezacheza tu analipa milioni mbili, wakati chuo kikuu unalipa Sh mil 1.5. Sijadharau shule zao, lakini tuangalie na kiwango cha elimu kinachotolewa,” alisema Rais Kikwete.
Alisema shule binafsi zinazotaka kutoza ada kubwa zinapaswa zithibitishe kiwango cha ubora wa elimu wanayotoa na wamiliki wa shule wanapaswa wakumbuke kuwa elimu ni haki ya mtoto, hivyo wanapaswa kujiepusha kutoza ada kubwa na ubaguzi wa elimu na huduma za elimu.
Aidha, Rais Kikwete alisema kupishana kwa mitaala ya kufundishia kunaelezwa katika sera kuhitaji mwongozo katika kila somo na kutumika kitabu kimoja cha kufundishia kwa shule zote ili kuondoa tofauti za utoaji wa elimu.
“Hatuwezi kuruhusu utaratibu wa kutumika kwa mitaala ya nchi nyingine, huwezi kuwa Tanzania halafu ukatumia mtaala wa Cambridge, wakati huo ni mfumo wa nchi nyingine.
“Hatuwezi kuwa na shule ambayo ina kitabu chake wanakuja wanafanya mtihani au wakiteuliwa kutunga mitihani wanafunzi wote wanafeli tunaanza kulaumu,” alisema Rais Kikwete.
Alisema mwongozo huo hautakataza matumizi ya vitabu vingine vya kujifunzia, isipokuwa kitabu kitachochaguliwa ndicho kitachotumika kutungia mitihani.
Alisema sera pia inatoa mwongozo wa kusimamia ubora wa elimu, kwakuwa hakuna nchi isiyokuwa na changamoto katika masuala hayo.
Matumizi ya kompyuta
Kuhusu matumizi ya kompyuta, Rais Kikwete alisema Serikali imeanza kufikiria kugawa kompyuta mpakato kwa kila mwanafunzi anayesoma elimu ya sekondari ili kukidhi mabadiliko ya sera ya elimu.
Alisema kompyuta hizo sasa zimeanza kutumiwa na walimu ili waweze kuwa na utaalamu wa kutosha katika ufundishaji.
“Mheshimiwa Kawambwa, naomba tufanye hili kabla sijaondoka, tuhakikishe wanafunzi wanatumia kompyuta shuleni,” alisema Rais Kikwete.
Ujenzi wa madarasa na maabara
Akizungumzia ujenzi wa madarasa na maabara, Rais Kikwete alisema serikali ilianza kujenga shule za kata kabla ya kuajiri walimu wa kutosha, lengo likiwa kuhakikisha yanakuwepo mazingira mazuri ya kusomea.
“Tulipoanza kujenga shule za kata watu waliziita yebo yebo, wakawa wanatucheka, lakini nikasema acha tuanze hata tukiwa hakuna walimu basi kufuli ziwepo.
“Nasema kama kuna mahali watoto wanasomea chini ya mti au kwenye mbavu za mbwa basi kuna matatizo ya kiuongozi.
“Nimegundua ukiwatisha watu mambo yanaenda, mara ya mwisho nilisema ujenzi wa maabara mwisho mwezi Juni, ukifikia muda huo kama kuna shule itakuwa haina maabara wahusika wanapaswa kuwajibika,” alisema Rais Kikwete.
Tatizo la walimu na changamoto za utoaji elimu
Rais Kikwete alisema hakuna nchi ambayo haina changamoto katika suala la elimu, isipokuwa changamoto hizo zinatofautiana.
“Asilimia 20 ya Bajeti ya Serikali ni elimu na mikopo imeongezeka vya kutosha, shule za msingi, sekondari na vyuo vimeongezeka ukilinganisha na awali, hivyo ni dhahiri kuwa tunapiga hatua pamoja na changamoto zilizopo,” alisema Rais Kikwete.
Alisema tatizo la walimu wa sanaa limemalizika na kwa sasa serikali ina mkakati wa kuondoa uhaba wa walimu wa sayansi katika shule za sekondari.
“Tumefikia hapo kwa jitihada hizi tunazoendelea kuzionyesha, watu wasione vyaelea, vimeundwa, sera tatu za elimu ya msingi, sekondari na ufundi ndizo zimetufikisha hapa, hakuna nchi ambayo imemaliza changamoto za elimu, nchi zote zina mijadala ya kuendeleza elimu,” alisema Rais Kikwete.
Uzinduzi wa sera hiyo ulienda sambamba na uzinduzi wa maabara tatu zilizopo katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai.
Kauli ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Awali akimkaribisha Rais Kikwete, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, alisema sera hiyo italeta mabadiliko ya kiuchumi na kutatua changamoto za elimu kikanda, ambazo zitaongeza fursa ya rasilimali watu.
“Ili tufikie malengo kwa mwaka 2025, ni wakati muafaka baada ya sekta ya elimu kufuatilia utaratibu mpya ili kuleta mazingira mazuri kufikia malengo ya Matokea Makubwa Sasa (BRN),” alisema Dk. Kawambwa.
Kauli ya Rais wa CWT
Naye Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba, alisema sera ni matamko ambayo hutolewa, lakini yanakuwa na changamoto za kuyafanyia kazi.
“Bado sijaisoma lakini kwa uzoefu wangu, sera huwa ni matamko, yanaweza yakatekelezwa au yakaachwa, sera yoyote itatekelezwa kama vigezo vyote vimezingatiwa katika elimu, hivyo lazima kuwa na walimu bora, zana za kufundishia pamoja na malipo mazuri ya walimu. Kama hayo yatatokea basi itatekelezeka,” alisema Mukoba.
Sera hiyo imezinduliwa huku kukiwa na malalamiko mbalimbali ya udhaifu katika Sekta ya Elimu, ikiwa ni pamoja na hoja iliyowahi kutolewa bungeni na Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, aliyedai kuwa Tanzania haina mitaala ya elimu na kwamba nchi haijawahi kuwa na mitaala ya elimu tangu ipate uhuru mwaka 1961.vip hapo kwenye bolded waalimu wa masomo ya sanaa na sayansi ya jamii!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom