Mi nlishagive up na AJIRA PORTAL. Ishu iko hivi. Unajuwa namba nne za mwanzo za NIDA kwa kawaida huwa zinawakilisha mwaka wa kuzaliwa ila mimi kwangu kwenye ile namba mwaka wa kuzaliwa unaonekana ni mkubwa ( NIDA WALIKOSEA) sasa nikawafuata NIDA wakaniambia kuwa haiwezi kuleta shida kwenye kitambulisho cha taifa maana namba itabaki kuwa namba tu na kwenye miaka kutakuwa na miaka yangu halisi na hakutakuwa na tatizo lolote lile so hawakubadilisha. so nime give up na kuomba kazi ajira portal maana wao wameamua kuzitreat zile namba nne za mwanzo kama mwaka wangu wa kuzaliwa kwa hiyo kila kazi ninayoomba naambiwa kuwa umri umezidi sana (yaani mkubwa sana) so sijaqualify kwa hiyo kazi.

