Kujiajiri kuna liability na kupata zaidi maana yake ni kujiongeza zaidi. Kumbuka kwenye kujiajiri jua na mvua vyote ni halali yako

!
Ukiambiwa utafute 1.5M kwa mwezi kwa kujiajiri ukiwa kama Jobless ambaye huna hata tsh.100 ya mtaji unafikiri itakuchukua muda kiasi gani? Siku hufungui biashara jua sikuhio huingizi hata tsh.100
Ila kuajiriwa jua na mvua ni juu ya boss wako wewe alimradi umesaini siku jua utapata 1.5M yako bila kelele kila ifikapo kati ya tarehe 27-30!
Ajira tamu mkuu hasa ikiwa na maslahi mazuri. Its less stressing kama biashara kwa mtazamo wangu. Biashara inakuwa relaxed ukiwa na mtaji mkubwa yani ndio utafaidi biashara ila kwa hii mitaji yetu ya laki 1 na nusu tutaishia kuuza pweza barabarani tu mwisho utimuliwe na migambo wavunje meza.