Ajira na kazi(kisheria) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira na kazi(kisheria)

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by PrN-kazi, Mar 10, 2011.

 1. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Tanzania kumekuwepo na mtindo wa Watu binafsi na Makampuni mbalimbali kuajiri wafanyakazi pasipokufuata mashariti yaliyowekwa na serikali kupitia sheria za kazi(ELRA No.6 na LIA No.7 za 204)

  Wafanyakazi wengi wamekua wakiangaika na kuteseka kwa kufanya kazi ngumu, kwa muda mrefu na kwa ujira(mshahara) mdogo kinyume na viwango villlivyowekwa na Bodi ya mishahara kwa kila sekta husika.

  Cha ajabu , kwa upande wa mwajiri binafsi utakuta mambo yake yanaenda vizzuri n lkn wafanyakazi wake wanahaaa hawapati ujira wao kwa muda muhafaka na hata wakiupata haukidhi ahaja kwani unakuwa uko chini ya kiwango. Na kwenye makampuni uko ndo basi, manyanyaso ni mtindo mmoja.

  Jitihada za kina zinafanyika kunusuru hali hii, ila kutokuwepo na ushirikiano ktkati ya vyombo husika na wadau kuna pelekea tatizo kujizatiti miongoni mwa waajiri.

  Usimamizi wa sheria kwa nyuma naweza kusema labda ulikuwa si mzuri, kwa sasa mambo yamebadilika; wasimamizi wako macho na wanafatilia na ndo maana nimeamua kuyasema haya:: mwajiri shariti aendane na Sheria za kazi zinavyosema, la sivyo Haki ya kuajiri au kuanzisha kampuni kwa minajiri ya kuwa na wafanyakazi haitakuwepo bila kuzingatia sheria za kazi (ELRA No 6 na LIA. No 7 za 2004)
   
 2. H

  Hambaza New Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati wadau wa masuala ya ajira walijaribu kulivalia njuga suala la kuandikishana mkataba kati ya muajiri na muajiriwa wa,sekta,binafsi, mfano mmiliki wa daladala au taxi na dereva, lakini sijui jitihada hizo zimefikia wapi hadi hivis sasa...! Nadhani suala hili lina umuhimu wake.
   
 3. LUSAJO L.M.

  LUSAJO L.M. JF-Expert Member

  #3
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 223
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nadhani hili suala halipo zaidi kwa Waajiri hata waajiriwa wanacgeza nafasi kubwa sana katika kulifanikisha hili. Katika sekta binafsi asilimia kubwa ya waajiriwa wako wakijali zaidi kipato wanachopata na kusahau haki zao za msingi. Ntatolea mfano kampuni moja ambayo wao wanawalipa wafanyakazi mishahara mizuri lakini mishahara ambayo kodi na NSSF ni kama asilimia 30 ya mshahara mtu anapokea. (Kama unapokea TZS 1,00,000/= basi katika official records unaandikiwa TZS 300,000/=).

  Na hili linafanyika kwa uwazi kabisa lakini tokana na tamaa tuliyonayo na kuangalia manufaa tunayoyapata katika wakati uliopo na kusahau kwamba kuna haki zetu za kimsingi ambazo tunazipoteza kwa tamaa zetu za kijinga.
   
Loading...