Ajira kwa vijana- heko lowassa kwa kuona mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajira kwa vijana- heko lowassa kwa kuona mbali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saggy, Jan 31, 2011.

 1. s

  saggy Senior Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili Januari 30,2011 mwaka 2010 iliandikwa makala ambayo pamoja na mambo mengine ni Tamko la Waziri Mkuu mstaafu mheshimiwa Edward Lowassa kuhusu tatizo sugu la ukosefu wa Ajira na hsa kwa vijana ni Bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote!

  Kwa wapenda maendeleo wezangu tuchukue nafasi hii kumpongeza Lowassa kwa ujasiri wake mkubwa,ni kweli tatizo la Ajira ni kubwa kwa sasa,maelfu ya wanafunzi wanahitimu na hawapati kazi na wanaranda mitaani na hakuna jitihada za dhati zilizochukuliwa kua adress tatizo hili.

  Moja ya sababu lilyochangia tatizo hili ni uwiano mdogo uliopo kati wa ukuaji wa sekta za uzalishaji wa huduma na mali na mendeleo ya Elimu,sekta binafsi haijakua kiasi cha kutosha kuajiri maelfu ya Vijana wanaomaliza vyuo vya Elimu ya juu,serikali pekee haiwezi kuajiri watu na hili limejitokeza pia katika mataifa ya Marekani na Asia.

  Heko Edward Lowassa kwakuwa umeiona shida yetu Vijana
   
 2. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 466
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Too little, too late.

  This guy had been in the system for almost 30 years. Kwani hakulina hilo hasa alipokuwa waziri mkuu? Wakati watu wanaimba kuwa elimu inavurugwa, walikuwa busy kuandaa watoto wao kushika hatamu kwa kuwapeleka Ulaya kusoma! Kukawa na elimu ya waTZ na ya vigogo. Wakiwa majukwaani wanasifia mafanikio, ukipinga wewe ni mpinzani huelewi.

  Wanakurupuka na kutengeneza wamachinga kwa kuwajengea "complexes" badala ya kuanzisha VETA nyingine za kuchukua wanaofeli Std 7 na Form 4. Inanikumbusha wimbo wa Lucky Dube "They wont build no hospitals, all they build is prison reserves; they wont build schools any more, all they buld is prison reserves". Tunaweza kusema hawataki kujenga shule bali machinga complexes.

  Hawajengi barabara, wanaanzisha "Three way kwenye barabara za two way".

  I am sorry, these guys are nothing but opportunists like hyenas. NOBODY IS SERIOUS
   
 3. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,523
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Sahihisho kidogo Lowasa si waziri mkuu mstaafu nialiyejiuzulu!
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,411
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 280
  Ndio sawa mh Lowassa kasema kwa maneno, ila uwezo wa kufanya kwa vitendo anao.

  KWanza aanze na kuachia wananchi kati ya ranchi zake anazoshikilia au basi afanye uwekezaji wa maana ili aajiri vijana.

  Pia katika fedha alizonazo, awekeze nchini kama akina kenyatta na Moi, wao wamewekeza kenya, wanalipa kodi na wameajiri wakenya angalau....
   
 5. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 5,944
  Likes Received: 536
  Trophy Points: 280
  Ebooo niliposoma Paragraph ya kwanza nilijua naenda kukutana na Paragraph inayotaja idadi ya vijana aliowasaidia kwa kuwapatia kazi somewhere!! Kwa upande wangu sioni kama anasitahili pongezi zozote kwa namna yoyote zaidi ya Lawama kwa sababu katika kukaa kwake madarakani angewajibika vema na kutumia raslimali za nchi hii kwa manufaa ya wananchi wote angekuwa amesaidia, lakini kwa hili sioni kama anastahili pongezi zozote napata wasi wasi wa initiator wa hii post kuwa inawezekana ni mmoja wa watu wake wachache wanaojaribu kumtengenezea njia nyembembe asiyoweza kupenya 2015.

  Tuangalie Pongei jamani si kila kitu cha kupongeza eti kwa sababu ya Personal interest!!, Mbona sijasikia ukilaumu kwa juhudi zake za makusudi kuliingiza taifa kwenye matatizo yanayoturudisha nyuma kwa zaidi ya miaka 7 kwa kulipa kulipa madeni tusiyostahili ya Dowans!! Yapo madhambi mengi yanayofunika huo ugoro anaopongezwa!!!! Jipanguse kaka hizo za pongezi sizo hastahili!!!!!!!
   
 6. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,053
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  I concur with you 1,000,000%.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,828
  Likes Received: 576
  Trophy Points: 280
  angekuwa anaona mbali asingeingiza nchi kwenye mikataba ya kifisadi na kampuni zao za kifisadi za Richmonduli na Dowans.

  Anataka Urais 2015 huyo.

  Werevu tunalijua hilo.

  Mtu mwizi anahisi, bila chembe ya aibu kutaka kugombea Urais?

  mimi nafuatilia vizuri na kwa karibu sana harakati zake za kuusaka Urais wa JMT
   
 8. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mh. Eduard Lowassa mi nnavyoona angekaa kimya maana alijiuzulu mwenyewe.Na si kwamba alipenda kujiuzulu bali hoja zilimbana akazidiwa akaona duuuu! hiii sasa noma ngoja niseme nimejiuzulu labda Watanzania watamuona kafanya la maana aaa wapi hakuna Mtanzania aliyelala ulimwengu wa leo.
   
Loading...