Ukosefu wa ajira kwa Vijana: Lowassa atabiri vita Tanzania... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukosefu wa ajira kwa Vijana: Lowassa atabiri vita Tanzania...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BONGOLALA, Jan 13, 2011.

 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  EL amesema hayo mwanza alipokua mgeni rasmi kuchangia kanisa katoliki, kukosekana kwa ajira kwa vijana ni bomu linalotarajia kulipuka wakati wowote hivyo kusababisha vita nchini.

  Kuna vijana 2.5m wasio na ajira!

  ==========
  UPDATED:

  Na mwandishi wa FikraPevu.com

  Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (MB), amesema kwamba, amani iliyopo hapa nchini ipo mashakani kutoweka, kutokana na wimbi kubwa la vijana kutokuwa na ajira maalumu, hivyo Serikali inapaswa kuweka mikakati madhubuti ya kuzalisha ajira nyingi kwa vijana.

  Amesema, kati ya nguvu kazi ya taifa inayokadiriwa kufikia milioni 25 kwa sasa, kati yake milioni 17.5 ni vijana ambao kimsingi wanakabiliwa na ukosefu wa ajira maalumu, jambo ambalo Serikali inapaswa kulipatia ufumbuzi haraka sana ili kulinda amani ya nchi isiyumbe au kutoweka kabisa.

  Lowassa, aliyasema hayo leo Jijini Mwanza, wakati alipokuwa akizungumza kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa Katoliki, Parokia ya Nyakato Jimbo Kuu la Mwanza.

  Lowassa ambaye pia ni mbunge wa Monduli na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM taifa alisema, hali hiyo inachangiwa na uchumi duni wa nchi ikiwa ni pamoja na sera mbovu za elimu zisizozingatia uhitaji wa soko la ajira na vijana wengi kutotaka kuchukuwa masomo ya sayansi na hisabati ambayo yana fursa kubwa ya kupata ajira.

  Kiongozi huyo ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo iliyokusanya sh. milioni 200 na kuvuka lengo la sh. milioni 120, alisema kwa sasa tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana hapa Tanzania limefikia zaidi ya asilimia 30, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 21 wa tatizo hilo linalozikumba nchi zote za Bara la Afrika.

  "Siku zote nimekuwa nikisema nchi yetu inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana. Hali hii isipopatiwa ufumbuzi na Serikali, amani ya nchi yetu inaweza kuyumba.

  "Kati ya vijana 850,000 wanaoingia kwenye soko la ajira baada ya kumaliza masomo yao ya msingi, sekondari na vyuo, ni asilimia tano tu ndiyo wanapata ajira katika sekta rasmi isiyo ya kilimo. Na hii ni hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu", alisema Lowassa ambaye alichangia sh. milioni 11 katika harambee hiyo.

  Kwa mujibu wa Lowassa ambaye alionekana kushangiliwa kila wakati pale jina lake linapotajwa, vitendo vya rushwa vinavyoonekana kuota mizizi katika sehemu za utoaji ajira rasmi Serikalini na kwenye taasisi za umma, ndiyo chanzo kikubwa cha matatizo kama hayo.

  Sababu nyingine alizozitaja Lowassa zinazochangia kukosekana kwa ajira kwa vijana nchini ni pamoja na sera mbovu za ajhira na mitaala ya elimu isiyokidhi mahitaji ya soko la ajira Bara la Afrika na duniani kwa ujumla.

  "Kutozingatia mabadiliko ya kiuchumi, kibiashjara, kisiasa, kijamii na kiteknolojia nchini, Afrika Mashariki, Afrika na dunia nzima ndiyo inayozalisha yote haya mabaya", alisema Lowassa ambaye alionekana kuwa kivutio kikubwa kwenye harambee hiyo.

  Awali, Makamu Baba Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, Askofu Richard Makungu aliwaonya watu wanaowanyooshea vidole wenzao, na kusema vitendo hivyo si vizuri hata kidogo, kwani watu hao wakichunguzwa nao wana mabaya yao, na wala hata choo majumbani mwao hawana kabisa.

  Askofu Makungu alisema, vitendo vya kulalamika lalamika ama kwa kuilalamikia Serikali, ofisa, kiongozi au mtu fulani huo ni sawa na ufedhuli mtupu, na kwamba Watanzania waache kusonta vidole watu, ili taifa liweze kupata taranta kutoka kwa Mungu.

  Hata hivyo, alisema ujio wa Lowassa katika harambee hiyo ni mzuri sana, na alisema kwa vile kanisa hiolo limejengwa kwa tofali moja moja, basi na waumini wa kanisa hilo watakuwa tofali moja moja kwa Lowassa.


  CHANZO: FikraPevu | JamiiForums' News Site
   
 2. s

  saggy Senior Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2008
  Messages: 153
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika gazeti la Tanzania Daima Jumapili Januari 30,2011 mwaka 2010 iliandikwa makala ambayo pamoja na mambo mengine ni Tamko la Waziri Mkuu mstaafu mheshimiwa Edward Lowassa kuhusu tatizo sugu la ukosefu wa Ajira na hsa kwa vijana ni Bomu ambalo linaweza kulipuka wakati wowote!

  Kwa wapenda maendeleo wezangu tuchukue nafasi hii kumpongeza Lowassa kwa ujasiri wake mkubwa,ni kweli tatizo la Ajira ni kubwa kwa sasa,maelfu ya wanafunzi wanahitimu na hawapati kazi na wanaranda mitaani na hakuna jitihada za dhati zilizochukuliwa kua adress tatizo hili.

  Moja ya sababu lilyochangia tatizo hili ni uwiano mdogo uliopo kati wa ukuaji wa sekta za uzalishaji wa huduma na mali na mendeleo ya Elimu,sekta binafsi haijakua kiasi cha kutosha kuajiri maelfu ya Vijana wanaomaliza vyuo vya Elimu ya juu,serikali pekee haiwezi kuajiri watu na hili limejitokeza pia katika mataifa ya Marekani na Asia.

  Heko Edward Lowassa kwakuwa umeiona shida yetu Vijana
   
 3. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Too little, too late.

  This guy had been in the system for almost 30 years. Kwani hakulina hilo hasa alipokuwa waziri mkuu? Wakati watu wanaimba kuwa elimu inavurugwa, walikuwa busy kuandaa watoto wao kushika hatamu kwa kuwapeleka Ulaya kusoma! Kukawa na elimu ya waTZ na ya vigogo. Wakiwa majukwaani wanasifia mafanikio, ukipinga wewe ni mpinzani huelewi.

  Wanakurupuka na kutengeneza wamachinga kwa kuwajengea "complexes" badala ya kuanzisha VETA nyingine za kuchukua wanaofeli Std 7 na Form 4. Inanikumbusha wimbo wa Lucky Dube "They wont build no hospitals, all they build is prison reserves; they wont build schools any more, all they buld is prison reserves". Tunaweza kusema hawataki kujenga shule bali machinga complexes.

  Hawajengi barabara, wanaanzisha "Three way kwenye barabara za two way".

  I am sorry, these guys are nothing but opportunists like hyenas. NOBODY IS SERIOUS
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Sahihisho kidogo Lowasa si waziri mkuu mstaafu nialiyejiuzulu!
   
 5. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,628
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Ndio sawa mh Lowassa kasema kwa maneno, ila uwezo wa kufanya kwa vitendo anao.

  KWanza aanze na kuachia wananchi kati ya ranchi zake anazoshikilia au basi afanye uwekezaji wa maana ili aajiri vijana.

  Pia katika fedha alizonazo, awekeze nchini kama akina kenyatta na Moi, wao wamewekeza kenya, wanalipa kodi na wameajiri wakenya angalau....
   
 6. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Ebooo niliposoma Paragraph ya kwanza nilijua naenda kukutana na Paragraph inayotaja idadi ya vijana aliowasaidia kwa kuwapatia kazi somewhere!! Kwa upande wangu sioni kama anasitahili pongezi zozote kwa namna yoyote zaidi ya Lawama kwa sababu katika kukaa kwake madarakani angewajibika vema na kutumia raslimali za nchi hii kwa manufaa ya wananchi wote angekuwa amesaidia, lakini kwa hili sioni kama anastahili pongezi zozote napata wasi wasi wa initiator wa hii post kuwa inawezekana ni mmoja wa watu wake wachache wanaojaribu kumtengenezea njia nyembembe asiyoweza kupenya 2015.

  Tuangalie Pongei jamani si kila kitu cha kupongeza eti kwa sababu ya Personal interest!!, Mbona sijasikia ukilaumu kwa juhudi zake za makusudi kuliingiza taifa kwenye matatizo yanayoturudisha nyuma kwa zaidi ya miaka 7 kwa kulipa kulipa madeni tusiyostahili ya Dowans!! Yapo madhambi mengi yanayofunika huo ugoro anaopongezwa!!!! Jipanguse kaka hizo za pongezi sizo hastahili!!!!!!!
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  angekuwa anaona mbali asingeingiza nchi kwenye mikataba ya kifisadi na kampuni zao za kifisadi za Richmonduli na Dowans.

  Anataka Urais 2015 huyo.

  Werevu tunalijua hilo.

  Mtu mwizi anahisi, bila chembe ya aibu kutaka kugombea Urais?

  mimi nafuatilia vizuri na kwa karibu sana harakati zake za kuusaka Urais wa JMT
   
 8. L

  LUMBAKALA Senior Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 147
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh. Eduard Lowassa mi nnavyoona angekaa kimya maana alijiuzulu mwenyewe.Na si kwamba alipenda kujiuzulu bali hoja zilimbana akazidiwa akaona duuuu! hiii sasa noma ngoja niseme nimejiuzulu labda Watanzania watamuona kafanya la maana aaa wapi hakuna Mtanzania aliyelala ulimwengu wa leo.
   
 9. Captain22

  Captain22 JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Kwa mara nyingine tena Edo amerudia kauli yake juu ya tatizo la ajira kwa vijana kuwa ni bomu linalosubiri kulipuka. Amezungumza hayo akiwa kwenye harambe ya kanisa huko Mwanza.
   
 10. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Hata yaliyotokea mbeya ni rasha rasha za hilo bomu la ukosefu ajira kwa vijana.
   
 11. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  .....Kama YOHANA MBATIZAJI...... kikikiki
   
 12. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,154
  Trophy Points: 280
  Lowassa anataka kuingia ikulu kwa mtutu?
   
 13. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  miaka 10 na mkapa.

  miaka 2+ na 'msanii'

  hilo bomu halikuwapo? au zile mvua za 'kufua' ziliishia wapi?

  kwanza amechangia bei gani kwenye harambee?
   
 14. B

  Bundajo JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  He was once in the JK's team and he ended up in embezzling public funds which prompted his embarassing exit.
   
 15. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,179
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  Lowassa lazima amkane Kikwete na mambo yake yote ndiyo tutamfikiria hata kuwa balozi wa nyumba kumi mwaka 2015.
   
 16. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2011
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lowasa is very intelligent politically.

  Now anataka kutumia mtaji wa vijana. Kama mwanasiasa anataka tuamni kuwa yuko very concened na "vijana".

  VIpi Kuhusu wazee amabao walitumikia serikali na makampuni binafsi na pension zao wanazopata sasa wanaishi maisha ya ajabu. Au sababu wazee hawana uwezo wa kurusha mawe.

  Labda walio karibu yake wamuulize hilo bomu la ajira kwa vijana limeanza hasa kutengenzwa mwaka gani?
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  People have a gut to call this fund raising speacilist and talk politics? Naona CMG amejiingiza rasmi kumpa shavu huyu bwana. Bila yeye jana ingekuwa ngumu kuwa Mwanza. Anyway,siasa nazo wakati mwingine zimejaa vichekesho
   
 18. L

  LATTICE BOND JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2011
  Joined: May 30, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lowassa is a matured politician!

  alishauri ccm na CDM wakae arusha ili kurinda hadhi ya jiji la Arusha - Akapingwa kwa matusi na dharau matokeo yake jambo dogo sana la mumuondoa yule diwani batili limesababisha mgogoro ambao unakaribia kuwa out of control!

  Hivi sasa ameshauri juhudi za maksudi zifanyike kuondoa tatizo la ajira kwa vijana - anaanza kuambiwa anatafuta urais ndio sababu anasema hayo!! watu wanaosema hayo wanaona kabisa jinnsi miji mikubwa ya Tanzania ilivyojaa pet traders kazi ambazo zingefanywa na wazee wasio na nguvu badala yake zinafanywa na vijana wenye nguvu!
   
 19. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 1,764
  Trophy Points: 280
  nampenda sana lowassa is so interligent amesoma arama za nyakati
   
 20. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #20
  Nov 13, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Baada ya uchaguzi mkuu wa chama 2012 tunamaliza kesi kwa kumpa u chifu wa Kabila la wasukuma pale Bujora EL 2015 CCM.
   
Loading...